Serikali kutangaza ajira mpya 32,000 wiki ijayo, Afya na Elimu kunufaika zaidi

Serikali kutangaza ajira mpya 32,000 wiki ijayo, Afya na Elimu kunufaika zaidi

Waziri Jenister Mhagama akitoa kauli ya Serikali bungeni kuhusu upungufu wa watumishi nchini, amesema Rais ameridhia na kutoa kibali cha kuajiri watumishi 30,000 na wiki ijayo atazitangaza.

Waziri Jenister Muhagama: Nasimama hapa kwa heshima kubwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninaomba niwaarifu waheshimiwa wabunge, mheshimiwa Rais na Serikali yake wametambua tatizo hili la uhaba wa watumishi na hasa kwenye miradi ya sekta ya afya na sekta ya elimu na hivyo basi, mheshimiwa Rais ametoa kibali, ahadi ya Serikali katika mwaka huu wa fedha ilikuwa tuajiri watumishi elfu 44.

Tayari Serikali ilikwisha kuajiri watumishi wapya na watumishi wa ajira mbadala 12,000. Niwathibitishie wabunge, mheshimiwa Rais ameridhia na wiki ijayo nitatoa tangazo Rasmi la ajira 32,000 na utaratibu wa ajira hizo na mgawanyo wake katika sekta ambazo zinaongoza kwa uhaba wa watumishi, maelezo yote nitayatoa wiki ijayo.

===========================

Serikali imeyangaza kuwa itataoa ajira za watumishi 32,000 ambapo miradi ya afya na sekta ya elimu ndiyo watakaokuwa wanufaika wakubwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Jenista Mhagama ameyasema hayo Bungeni leo Aprili 6, 2022.

“Kumekuwa na hofu kuhusu sekta ya elimu na afya, naomba niwaarifu kuwa Rais na Serikali yake wametambua tatizo la uhaba wa watumishi hasa kwenye miradi ya afya na sekta elimu, ahadi ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha ilikuwa tuajiri watumishi 44,000.

“Tayari Serikali imeshapitisha watumishi wapya 12,000, naomba niwathibitishie kuwa Rais ameridhia na wiki ijayo tutatoa tangazo la ajira 32,000 mpya. Utaratibu na mgawanyo wake, maelezo yote nitayatoa wiki ijayo,” – Jenista Muhagama.
Nasoma comments zenye watu wenye WIVU, CHUKI na ROHO MBAYA.

Sisi ndio Waswahili🤣🤣
 
Kwa hiyo kwenye elimu na afya ndo kaona uhaba wa watumishi, siyo? huyu mama hajui kwenye sekta karibu zote za serikali kuna uhaba mkubwa wa watumishi baada ya kufyeka watumishi kwenye lile zoezi lao la kionevu na kuishia kuajiri watu kiduchu tangu kipindi cha jiwe. Huyo naona kaletwa hapo kwa ajili ya kupiga propaganda na kukwamisha maslahi ya watumishi ikiwemo kupanda madaraja na nyongeza za mishahara, hana jipya.........​
 
Nilidhani wataajiri hata laki 2 hivi kumbe elfu 32 pekee?
 
Naona safari hii wizara ya Utumishi wa Umma(Sijui ndo inaitwa hvyo🤣🤣) pamoja na waziri wake wamejistukia na wameamua kudirect kabisa hadi siku/wiki ambayo watatangaza hizi Ajira mpya na waziri wa Utumishi amesema Leo kuwa Ajira zitatoka wiki ijayo.

Ila wadau tunataka tujue kuwa zitakuwa za kada tofautitofauti AU ndo kama ilivyozoeleka tu kuwa Serikali hii inaajiri watumishi wa Afya & Elimu tu sisi na haya makozi yetu mengine kama Engineering ya umeme, maji, ujenzi, Kilimo, mifugo, maendeleo ya jamii, uhasibu tuendelee tu na Mfungo wa Ramadhani Huku tukimuomba Mungu angalau ikikaribia 2025 nasi tukumbukwe?
 
Naona safari hii hii wizara ya Utumishi ya Umma(Sijui ndo inaitwa hvyo🤣🤣) pamoja na waziri wake wamejistukia na wameamua kuadirect kabisa Hadi siku/wiki ambayo watangazaji hizi Ajira mpya.
Ila wadau tunataka tujue kuwa zitakuwa za kada tofautitofauti AU ndo kama ilivyozoeleka tu kuwa Serikali hii inaajiri watumisy wa Afya & Elimu tu..?
Ngoja tusubiri muongozo.
 
Tunatarajia nafasi hizi ziwe za wizara zote na taasisi zote za serikali.
 
Pia ukumbuke huwenda zika gawanywa🏃💃🏃💃🏃💃🏃💃🏃💃💃💃🏃🏃
 
Propaganda..subirini mfurahishwe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Daaah, kiukweli hakuna Fair, just imagine kuna jobless wa vitivo mbalimbali alafu Kila siku zikitoka Ajira tunasikia ni Afya na Ualimu.. inatusikitisha sana, Sasa sijui hawa wa Afya na Ualimu ndo wanaowapigia kura miaka yote.

Frankly tunaelewa hizo ni sekta nyeti sana ndani ya Taifa letu.. Ila kwenye Ajira 32000, wanaweza kugawa hata hizo 10,000 zikawa za faculty tofauti ili tugawanegawane kidogo
Ngoja tusubiri muongozo.
 
Back
Top Bottom