Serikali kutangaza ajira mpya 32,000 wiki ijayo, Afya na Elimu kunufaika zaidi

Serikali kutangaza ajira mpya 32,000 wiki ijayo, Afya na Elimu kunufaika zaidi

Naona safari hii wizara ya Utumishi wa Umma(Sijui ndo inaitwa hvyo🤣🤣) pamoja na waziri wake wamejistukia na wameamua kudirect kabisa hadi siku/wiki ambayo watatangaza hizi Ajira mpya na waziri wa Utumishi amesema Leo kuwa Ajira zitatoka wiki ijayo
Ila wadau tunataka tujue kuwa zitakuwa za kada tofautitofauti AU ndo kama ilivyozoeleka tu kuwa Serikali hii inaajiri watumishi wa Afya & Elimu tu sisi na haya makozi yetu mengine kama Engineering ya umeme, maji, ujenzi, Kilimo, mifugo, maendeleo ya jamii, uhasibu tuendelee tu na Mfungo wa Ramadhani Huku tukimuomba Mungu angalau ikikaribia 2025 nasi tukumbukwe..?
Soma hapa 👇

Screenshot_20220406-152348.png
 
Daaah, kiukweli hakuna Fair, just imagine kuna jobless wa vitivo mbalimbali alafu Kila siku zikitoka Ajira tunasikia ni Afya na Ualimu.. inatusikitisha sana, Sasa sijui hawa wa Afya na Ualimu ndo wanaowapigia kura miaka yote..!!!
Frankly tunaelewa hizo ni sekta nyeti sana ndani ya Taifa letu.. Ila kwenye Ajira 32000, wanaweza kugawa hata hizo 10,000 zikawa za faculty tofauti ili tugawanegawane kidogo
Kbsa shombe uko sahih hata elfu tano tu watupe ss wa koz mbadala tupigane vikumbo pale utumishi

Tra wamenitema kiz vyeti .brela na self nao wakanitema

Sas tunaomba ktk hizo za week ijayo tupate mgao angalau elf tano HV tukapambne na taifa kulijiilenga
 
Serikali imetangaza kuwa itataoa ajira za watumishi 32,000 ambapo miradi ya afya na sekta ya elimu ndiyo watakaokuwa wanufaika wakubwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Jenista Mhagama ameyasema hayo Bungeni leo Aprili 6, 2022.

“Kumekuwa na hofu kuhusu sekta ya elimu na afya, naomba niwaarifu kuwa Rais na Serikali yake wametambua tatizo la uhaba wa watumishi hasa kwenye miradi ya afya na sekta elimu, ahadi ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha ilikuwa tuajiri watumishi 44,000.

“Tayari Serikali imeshapitisha watumishi wapya 12,000, naomba niwathibitishie kuwa Rais ameridhia na wiki ijayo tutatoa tangazo la ajira 32,000 mpya. Utaratibu na mgawanyo wake, maelezo yote nitayatoa wiki ijayo,” – Jenista Muhagama.

Tazama Video hapa>>>
 
Mchanganuo

Walimu 15000
Afya 10000

Hizo 7000 mtagawana huko.

Msisahau kuna vyombo vya ulinzi na usalama navyo bado vinahitaji ajira mpya sana tu. Magereza namba moja

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Sisi ambao tunazururazurura Huku Halmashauri nyingi na wakuu wa idara tunaelewa.. wewe hujui lolote, So usinisumbue mkuu kama hutaki pita kushoto na sikulazimishi ukubali nikisemacho
Toa mfano, ni sekta ipi inauhaba zaidi ya Afya na Elimu ?!
 
Hongera kwa serikali ya CCM ya awamu ya 6 kwa utekelezaji wa ahadi
 
Waziri Jenister Mhagama akitoa kauli ya Serikali bungeni kuhusu upungufu wa watumishi nchini, amesema Rais ameridhia na kutoa kibali cha kuajiri watumishi 30,000 na wiki ijayo atazitangaza.

We need katiba mpya kwa hakika....
 
JK aliweza kuajiri kwa vitendo maelfu ya wahitimu kila mwaka. Ila hawa wengine, inahitaji uwe na moyo wa chuma kuwaamini.

Maana wana maneno mengi matamu midomoni mwao, kuliko vitendo.
 
Bi mkubwa akifata nyayo za bwana mkwere kwenye suala la ajira, 2025 hata akienda vacation Hawaii nampa kura yangu 100%
 
Back
Top Bottom