Serikali kutangaza ajira mpya 32,000 wiki ijayo, Afya na Elimu kunufaika zaidi

Nasoma comments zenye watu wenye WIVU, CHUKI na ROHO MBAYA.

Sisi ndio Waswahili🀣🀣
 
Kwa hiyo kwenye elimu na afya ndo kaona uhaba wa watumishi, siyo? huyu mama hajui kwenye sekta karibu zote za serikali kuna uhaba mkubwa wa watumishi baada ya kufyeka watumishi kwenye lile zoezi lao la kionevu na kuishia kuajiri watu kiduchu tangu kipindi cha jiwe. Huyo naona kaletwa hapo kwa ajili ya kupiga propaganda na kukwamisha maslahi ya watumishi ikiwemo kupanda madaraja na nyongeza za mishahara, hana jipya.........​
 
Nilidhani wataajiri hata laki 2 hivi kumbe elfu 32 pekee?
 
Naona safari hii wizara ya Utumishi wa Umma(Sijui ndo inaitwa hvyo🀣🀣) pamoja na waziri wake wamejistukia na wameamua kudirect kabisa hadi siku/wiki ambayo watatangaza hizi Ajira mpya na waziri wa Utumishi amesema Leo kuwa Ajira zitatoka wiki ijayo.

Ila wadau tunataka tujue kuwa zitakuwa za kada tofautitofauti AU ndo kama ilivyozoeleka tu kuwa Serikali hii inaajiri watumishi wa Afya & Elimu tu sisi na haya makozi yetu mengine kama Engineering ya umeme, maji, ujenzi, Kilimo, mifugo, maendeleo ya jamii, uhasibu tuendelee tu na Mfungo wa Ramadhani Huku tukimuomba Mungu angalau ikikaribia 2025 nasi tukumbukwe?
 
Ngoja tusubiri muongozo.
 
Tunatarajia nafasi hizi ziwe za wizara zote na taasisi zote za serikali.
 
Pia ukumbuke huwenda zika gawanywaπŸƒπŸ’ƒπŸƒπŸ’ƒπŸƒπŸ’ƒπŸƒπŸ’ƒπŸƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸƒπŸƒ
 
Propaganda..subirini mfurahishwe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Daaah, kiukweli hakuna Fair, just imagine kuna jobless wa vitivo mbalimbali alafu Kila siku zikitoka Ajira tunasikia ni Afya na Ualimu.. inatusikitisha sana, Sasa sijui hawa wa Afya na Ualimu ndo wanaowapigia kura miaka yote.

Frankly tunaelewa hizo ni sekta nyeti sana ndani ya Taifa letu.. Ila kwenye Ajira 32000, wanaweza kugawa hata hizo 10,000 zikawa za faculty tofauti ili tugawanegawane kidogo
Ngoja tusubiri muongozo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…