Serikali kutoa ufafanuzi nyongeza ya mishahara, yaomba wafanyakazi watulie
Wakuu umofia kwema!
Baada ya Jana kupigwa na kitu kizito, serikali nayo imetoa tamko linaloashilia kuwepo kwa Ahadi mbele yake, chama cha wafanyakazi nao wanaonekana kukusudia kukaa mezani kufanya michongo na serikali.

Hakuna madaraja, hakuna madaraja mserereko hakuna kupanda kwa mshahara.

Woga sio jadi yetu! Ongezeko la mishahara ni haki yetu. Turudi kwenye haki ya kikatiba ya mgomo na maandamano makubwa. Hatuna sababu ya kufundisha, kutibu watu ama kusukuma mitambo kwa mishahara ya kinyonyaji.

Alisema mwalimu nyerere "wafanyakazi muungane, hakuna cha kupoteza isipokuwa minyororo yenu"

Ongezeko la Asilimia 100 ni lazima, tuliyotayari kwenda Kula tausi tujuane. Nitaongoza msafara
Hahaha.......kandoto katamu!
 
Kwanza hata bila serikali kutoa ufafanuzi inaeleweka kuwa 23.3% ni nyongeza ya mtu anayelipwa kima cha chini kabisa cha mshahara na wala si nyongeza ya asilimia hiyo kwa wote! Mbona ingekuwa hivyo serikali ingefilisika mwezi mmoja tu! Pili, bajeti ilishapitishwa, hivyo hakuna litakalobadilika zaidi ya haya niliyoandika hapa! Labda subirini nyongeza ya miaka inayofuata lakini siyo mwaka huu wa fedha!
Watu wagumu sana kuelewa.
 
Wakuu umofia kwema!
Baada ya Jana kupigwa na kitu kizito, serikali nayo imetoa tamko linaloashilia kuwepo kwa Ahadi mbele yake, chama cha wafanyakazi nao wanaonekana kukusudia kukaa mezani kufanya michongo na serikali.

Hakuna madaraja, hakuna madaraja mserereko hakuna kupanda kwa mshahara.

Woga sio jadi yetu! Ongezeko la mishahara ni haki yetu. Turudi kwenye haki ya kikatiba ya mgomo na maandamano makubwa. Hatuna sababu ya kufundisha, kutibu watu ama kusukuma mitambo kwa mishahara ya kinyonyaji.

Alisema mwalimu nyerere "wafanyakazi muungane, hakuna cha kupoteza isipokuwa minyororo yenu"

Ongezeko la Asilimia 100 ni lazima, tuliyotayari kwenda Kula tausi tujuane. Nitaongoza msafara
Ukiniletea unyoya wake tu na wala si nyama nitajua jeshi la Polisi limebadilika chini ya IGP Wambura
 
Mara ngapi afedheheke kinachomkera wameongeza posho wao wakubwa huku chini maumivu ubinafsi wa Hali yajuu aa Hawa viongozi, waogope jamani, tozo Kila Kona, gharama za maisha zimepanda. Kwani si angekaa tu kimya kuliko Nye Nye Nye nyingi afu unakuta 12600 upuuzi mtupuu!!

Nimemchukia huyu maza na vibaraka wake!!
Haijalishi unamchukukia kiasi gani , she is your president, Hadi mwaka 2030,jiandae kisaikolojia,

By the way mtu hawezi ishi na kuwa na Maisha Bora kwa kutegemea vitu vya kupesa, mshahara ni sawa na kitu Cha kupewa, hivyo hata ukilipwa milioni Saba bado utalalamika.

Kwa kilichoweka kinatosha, tusubiri mwaka kesho Mungu akipenda.
 
Alitakiwa atoe ufafanuzi Kipindi kile watu wanapotoshana kuhusu 23%!
 
Swali rahisi la kujiuliza ni moja, kwanini walipokua wanatangaza hili ongezeko hawakutoa ufafanuzi af leo ndo wanajidai kutoa ufafanuzi? Hii ni damage control tu hakuna lolote
Tangazo lilikuwa linajifafanua lenyewe, tuliolielewa hatukutarajia mabadiliko makubwa.
 
[emoji2] Abeg.

Acheni kazi
Hakuna muajiriwa mwenye ujanja wa kuishi nje ya mshahara,we uoni wakistaafu upewa teuzi Ili wasife mapema,usione mabiashara makubwa wanafanya wakiwa makazini yote yanategemea ofisi kupitia kodi zetu, ukitaka kuthibitisha hilo iangalie biashara hio baada ya kustaafu, nyingi nazo huwa zinastaafu kwa maana ofisi imekata.
 
Back
Top Bottom