Kigezo kinachoangaliwa pale ni ujuzi na sio jinsia
Hilo ni tatizo,haiwezekani kwenye kazi zingine jinsia ziangaliwe alafu katika udaktari jinsia isiangaliwe it's totally wrong.
Iamagine katika upolisi jinsia hutazamwa ndio maana polisi wa kike atamfanyia upekuzi mtuhumiwa wa kike pekee,mbona hapa haisemwi kuwa kinachoangaliwa ni ujuzi wa kupekua tu hivyo hata mwanaume apekue tu pale na jinsia inaangaliwa ?
Ujuzi lazima uendane na jinsia huu ndo ustaarabu,linapofika suala la kutibu jinsia lazima iangaliwe nayo.
Anaweza akawa daktari jinsia ya kiume ndio ana weledi na hiyo kazi kuliko hawa assistant nurse ambao kazi yao ni kufuata maelekezo nini wafanye kutoka kwa huyo daktari bingwa.
Solution ya kudumu ni kuzalisha madaktari wengi wa kike ambao nao watakuwa na ujuzi.
Akini hasa hasa uzi wangu ulilenga hospitali ambazo madaktari wa kike wapo lakini wanaume ndo huwa wanatibu hata wale wagonjwa wa kike.
Ikiwa ugonjwa huo anaeweza kutibu ni dokta wa jinsia tofauti na mgonjwa basi uzi wangu wala haukukataa kutibiwa.
Sasa We utakubali kumuacha dada yako au mama yako asifanyiwe operation azae eti kwasababu ya daktari kua ni mwanaume?
Labda niseme kuwa hukuelewa uzi,na hili ni tatizo la sisi wana jf.
Kumbuka niliposema 👇👇
Yani utakuta hospitali kuna madaktari wa jinsia nyingi lskini mwanamke anatibiwa na mwanaume au kinyume chake.
Serikali isomeshe watoto wengi wa kike ili kuja kuepusha hii aibu,ipunguze vigezo vya kusomea udaktari kwa mwanamke hasa kwa mambo ya kawaida haya ambayo hayahitaji kujitoa sana wanawake wasomeshwe waje kuzalisha wanawake wenzao.
Hapo ukisoma utagundua nimemaanisha kuwa hospitali ama sehemu ambazo hazina daktari jinsia sawa na mgonjwa basi sijasema kuwa asitibiwe.
Na kusomesha watoto wa kike wengi ni solution ambayo nimeitoa ili hata mama yangu au ndugu yangu akitaka kufanyiwa operation basi amkutedaktari wa kike ambaye yuko na utaalamu huo.
Kuna hospitali moja iko ilala pale kuna mama mmoja ni mtaalamu mzuuri tu anazalisha na kufanya operation kubwa tu,huyu kaweza kuwa mtaalamu na wengine pia wanaweza ni jambo la kuwekeza juhudi tu