Serikali msijisahau katika hili la daktari kumtibia mtu wa jinsia tofauti na yeye

Serikali msijisahau katika hili la daktari kumtibia mtu wa jinsia tofauti na yeye

Hao wanawake wwnyewe asilimia kubwa hasa wajawazito wanapenda kuhudumiwa na ma Dr wa kiume, chunguzeni mtaligundua hilo
 
Hilo ni tatizo,haiwezekani kwenye kazi zingine jinsia ziangaliwe alafu katika udaktari jinsia isiangaliwe it's totally wrong.
kwani mzee katiba ya tz kisheria inasemaje raia akifanya kosa ? si inasema ashtakiwe au?

lakini katiba hiyo hiyo imempa immunity raisi kwamba hatakiwi kushtakiwa kivyovyote vile na hata akitoka madarakani hupaswi kumshtaki kwa makosa aliyoyafanya akiwa raisi

swala la afya ni swala nyeti lenye kushughulika kuhakikisha uhai wetu unaimarika ipasavyo, huku gender it does not matter usitumie itifaki za "ujinsia" kwenye mambo ya afya.
Iamagine katika upolisi jinsia hutazamwa ndio maana polisi wa kike atamfanyia upekuzi mtuhumiwa wa kike pekee,mbona hapa haisemwi kuwa kinachoangaliwa ni ujuzi wa kupekua tu hivyo hata mwanaume apekue tu pale na jinsia inaangaliwa ?
sasa upolisi unafikiri unahitaji taaluma yeyote ya kibailojia?

kwani kuna polisi maalumu kutoka kitengo cha kupekua ambaye amekua trained special kwa kazi hiyo au ni gender tu ndiyo kigezo?

hivi unafikiri huyo mpekuzi akiwa huko mafunzoni anafundishwa namna ya kuwapekua watu wenye jinsia kama yake?

hospitali kuna mtu anaitwa "Obstetrician" huyu kakaa shuleni miaka zaidi ya miaka zaidi ya minne akis mfumo mzima wa uzazi wa mwanamke kuanzia mimba, mpaka kuzalisha. huyu amegraduate kwenye medical school kashapata ujuzi na anaenda hosipali kulipwa mshahara kwa kazi hiyo hiyo tofauti na mwela mshika kirungu ambaye mostly ni form four failures

Ujuzi lazima uendane na jinsia huu ndo ustaarabu,linapofika suala la kutibu jinsia lazima iangaliwe nayo.
hapa ndio unatumia hisia kuliko uhalisia.

ikiwa wanafunzi wa jinsia hiyo ambao wanapaswa kushugulika na wagonjwa wa kike hawaja-qualify kupata huo ujuzi utawalazimisha waingie kwenye majukumu ambayo hawana uwezo wa kuyamudu?
Solution ya kudumu ni kuzalisha madaktari wengi wa kike ambao nao watakuwa na ujuzi.
wengi wanakua ni nurse assistant, yani kama fundi msaidizi wa ujenzi ambaye hufanya kile anachoagizwa na fundi mkuu wake kutokana na kutokua na taaluma ya ujenzi.
Akini hasa hasa uzi wangu ulilenga hospitali ambazo madaktari wa kike wapo lakini wanaume ndo huwa wanatibu hata wale wagonjwa wa kike.\
ishu sio kuwepo, ishu ni ujuzi wa taaluma husika. kwa mfano imetokea kaja mgonjwa anatakiwa afanyiwe operation ya na titi ukicheki around kuna ma-nurse ambao kimsingi hawana taaluma halafu kukawa na daktari wa kiume mwenye ujuzi wa hilo tatizo je utalazimika kurudi na mgonjwa nyumbani ?
Ikiwa ugonjwa huo anaeweza kutibu ni dokta wa jinsia tofauti na mgonjwa basi uzi wangu wala haukukataa kutibiwa.
na hiyo ita conclude kua gender doesn't matter on health services, kwahiyo utajikuta point nzima ya kulalamikia madaktari kuhudumia wagonjwa wenye jinsia tofauti na yao ni invalid
Labda niseme kuwa hukuelewa uzi,na hili ni tatizo la sisi wana jf.
nimeuelewa from the top to the bottom
Kumbuka niliposema 👇👇
Yani utakuta hospitali kuna madaktari wa jinsia nyingi lskini mwanamke anatibiwa na mwanaume au kinyume chake.

Serikali isomeshe watoto wengi wa kike ili kuja kuepusha hii aibu,ipunguze vigezo vya kusomea udaktari kwa mwanamke hasa kwa mambo ya kawaida haya ambayo hayahitaji kujitoa sana wanawake wasomeshwe waje kuzalisha wanawake wenzao.
kwani serikali haisomeshi watoto wa kike? mbona ndio wanaotuongoza kwenye matokeo kitaifa kila mwaka?

ishu ya udaktari ni persona interest, unaweza kuwapata maelfu ya wanawake wasomi na wenye ufaulu mzuri lakini katika hao ni wachache tu ndio wakawa attractive na udaktari. na katika hao watao chagua udaktari ukapata kundi lenye kujigawa tena wengine wakawa madaktari wa mifugo

Hapo ukisoma utagundua nimemaanisha kuwa hospitali ama sehemu ambazo hazina daktari jinsia sawa na mgonjwa basi sijasema kuwa asitibiwe.
najua hukumaanisha hivyo ila kutumia protocols za police kuhusu gender kwenye swala nyeti la afya hapo ndio wasiwasi wangu ulipokua
Na kusomesha watoto wa kike wengi ni solution ambayo nimeitoa ili hata mama yangu au ndugu yangu akitaka kufanyiwa operation basi amkutedaktari wa kike ambaye yuko na utaalamu huo.
na ndio maana nimekuambia haya mambo yana base sana kwenye interest binafsi, kwa mfano hata katika shule uliyosoma kulikua na wanafunzi wangapi darasani mwenu ambao walikua science taker?

wanawake wengi ni wasomi tena sana (mpaka wanaume) ila usomi wao asilimia kubwa ni katika masomo sanaa. na hawa pia kumbuka ni wasomi hatuwezi kuwaita sio wasomi eti kwakua hawaja chagua masomo ya sayansi wakati mfumo wa kielimu umetoa uhuru kila mwanafunzi kuchagua mchepuo autakaye.

na kumbuka hauwezi kuwashurutisha wasome masomo ambayo wao wameona yanawazidi uwezo eti kwakua sector fulani inahitaji watu wengi zaidi
Kuna hospitali moja iko ilala pale kuna mama mmoja ni mtaalamu mzuuri tu anazalisha na kufanya operation kubwa tu,huyu kaweza kuwa mtaalamu na wengine pia wanaweza ni jambo la kuwekeza juhudi tu
wengi wa hivyo wapo ila ku-balance kwamba kila hospitali hususani hizi za hospitali kwamba iwe na madokta bingwa wa jinsia tofauti zaidi mmoja ndio kasheshe

huyo mama haishii kwa wanawake tu mpaka tohara kwa watu wazima anawafanyia
 
Kuna dhana moja kwamba mafundi nguo wa kiume ni wajuvi sana wa mishono ya kina mama.

Lakini ni aghalabu fundi nguo wa kike kushona mavazi ya kiume.


Sasa mkuu, vipi kwa fundi nguo wa kiume kumpima mwanamke mwilini?
Nayo pia haiko sawa.

Anakushika shika fundi wa kiume wakati wewe ni mwanamke hii nayo pia ikemewe.

Akupime fundi wa kike ama skupime mwanamke then vipimo apewe fundi wa kiume anashona vizuri tu,simple tu
 
hii sio rahisi ,hakuna ubaya kuvua boxer yako kwa Dr wa kike.Cha muhimu ni matibabu.Hata kule labour ward madaktari wa kiume ndio wanaongoza kwa kufanya operation za kuzalisha na wala hakuna malalamishi.Huwezi kufika hospital na kuanza kuchagua mtu wa kukutibu .
Kwa sababu hawatoshi hasa wanawake madaktari,wangetosha basi ingewezekana.

Sasa ni kazi ya serikali kuchukua juhudi kuhakikisha kuwa wanapunguza wimbi la hili suala.
 
unachotakiwa kujua ni kwamba, sehemu za siri za mwanaume au mwanamke hazina thamani yeyote. MIMI ni mwanaume, ningekuwa naumwa ugonjwa wa aibu singependelea nitibiwe na mwanaume mwenzangu. imagine mwanaume mwenzio anakushikashika makalio, penis, korodani, etc, bora mwanamke nitakuwa confortable. uchi hauna uzee au ukijana, ni uleule tu. ukitaka kujua kuwa ucho wako huo na wa mkeo hauna thamani, waulize wanawake ambao walishaenda leba kujifungua.

acha wivu, hakuna mwenye shida na mkeo, hata yeye anakushangaa pamoja na kwamba hawezi kukuambia hilo.
Kama uchi hauna thamani kwa nini katika suala la kupekua polisi wa kiume haruhusiwi kumpekua raia wa kike ?
 
Wakuu naomba niipongeze serikali kwa jitihada zake inazofanya katika kuhakikisha ile heshima ya jinsia zote inalindwa.

Tukiangalia katika majeshi hasa jeshi la polisi utakuta kuna askari wa kike ambao kama itatokea muhalifu ni mwanamke basi askari yule hakuajiriwa kwa bahati mbaya bali hiyo itakuwa ni kazi yake kumpekua sehemu za mwili wake.

Hali kadhaalika mwanaume atapekuliwa na askari wa kiume katika kulinda heshima.

Hata mashuleni kuna waalimu wa kike kibao ambao wao watashughulikia masuala mbali mbali ya wanafunzi wa kike.

Mbona sioni suala hili la kuheshimu jinsia na kulinda heshima ya mtu likifanyika na kusisitizwa katika kada ya afya ?

Kwa nini isiwe kosa daktari wa kumtibia mgonjwa wa jinsia tofauti na yeye ikiwa katika hospitali hiyo ama maeneo hayo kuna daktari mwenye jinsia sawa na mgonjwa ?

Kama ambavyo polisi haruhusiwi kumfanyia upekuzi wa mwili mtu wa jinsia isiyekuwa yake wakati wa jinsia yake wakiwa pale hii ni kosa,vipi isiwe kosa katika hii kada ya afya ?

Yani utakuta hospitali kuna madaktari wa jinsia nyingi lskini mwanamke anatibiwa na mwanaume au kinyume chake.

Serikali isomeshe watoto wengi wa kike ili kuja kuepusha hii aibu,ipunguze vigezo vya kusomea udaktari kwa mwanamke hasa kwa mambo ya kawaida haya ambayo hayahitaji kujitoa sana wanawake wasomeshwe waje kuzalisha wanawake wenzao.

Chumba cha kuzalisha kuna madaktari wa kike watano na wa kiume mmoja,huyu wa kiume anatafuta nini,kwa nini isiwe kosa kisheria?
Issue ya msingi sana hii.
 
Naunga mkono hoja yaaan niende korodani znauma nmwoneshe mwanamke ww uliskia waaaaaap ..hiii si sawaa kabsaa na ndo mana kuna kesi madokta wa kiume kubaka wagonjwaaa
Halafu wenyewe wanachukulia powa tu eti kwa vile ni hospitali.
Kuna siku nilienda kufanyiwa utrasound sasa nimeingia maabara kuna kaka mmoja akawa ananipima huku nikiwa uchi kitandani basi nikashangaa kuna mdada mmoja nesi anaingia tu mle ndani halaf anaona mimi niko uchi wala hashtuki akawa anatafuta sijui vikorokoro gani,aisee nilikasirika nikasema nitadeal naye nje ya hospitali tumalize mchezo kabisa
 
Ward ya wazazi kuna Madaktari mchanganyiko, lkn Mzazi mwenyewe atamwita au kumsubiri Dr wa kiume, kuliko wanawake, na wanaamini Dr mwanamke ni Nurse tu. wanume wako makini na huruma kwa wanawake kuliko wanawake wenzao!!!

Hili swali uwachie wanawake wenyewe wachague? wanavotaka kumbuka unaweza kwenda Hosptali ukakataa kufunuliwa au kuchunguzwa na yeyote au km una Dr wako unaye mwamini unamfuata huyo huyo.

Hospita zetu zote za Serikali kuna milango nane ya Madaktari na humo wamo mchanganyiko uchaguzi ni wako! Temeke Hosp. OPD milango 10. lkn katika kuchunguzwa na Dr anakuomba akufanyie uchunguzi kwa jinsi anavofikiria tatizo lako hapo unaweza kukubali au kukataa, halazimishi au kukufanyia kimyakimya! BIG NO. na yote wanaandika kwenye cheti chako isije ikaonekana kuwa Dr ni mzembe!!! Ukikataa ataandika, ukikubali ataandika. atakushauri unavotaka wewe!!!

kulazwa, Kupima Malaria, kutumia dawa, kufungwa kidonda nk, siyo lazima unaweza kukataa vilevile. Bila shaka mmeona Mabinti wengi walio toa Mimba kwa njia za kienyeji wakifa kwa kukosa Damu au kuoza nk, kwa sababu ya kukataa kutibiwa na kuficha tatizo lao! kwa kumjali alompa mimba asigundulike!!

hawatakagi kufunuliwa kabisaa! sana atasema ana Malaria tu Basi. Dr yeye atamwambia ukweli kuwa wewe nahisi umetoa mimba unatakiwa upimwe hivi na hivi, ila hutaki unasema una Malaria Ok! ataandika hivohivo alivo kuona kitaalamu kwenye cheti chako na kitabu chake cha Mahudhurio ya siku hiyo muda na Saa! ila wewe hutajua labda uwe mtaalamu wa Afya. Lengo asionekane mzembe huko mbele ya Safari.

Ulizaga kabla
 
Mi napenda nihudumiwe na daktari wa kiume. Kama huo mswada wenu utapita iwe option na sio lazima
 
Angalizo Kama atahitajika kupimwa vipimo Kama ECHO, MRI, CT SCAN, na vingine vya kuvua nguo imekula kwako maana wataalamu wa kike bado Ni wachache.
Jingine Ni pale shemeji atakapohitaji huduma za daktari mbobezi wa magonjwa ya kina mama,
Hii ndio shida ya wana jf inakuwa ngumu sana kuelewa mada.

Sasa wapi nimesema kuwa watu waache kuhudumiwa na madaktari wanaume?

Nilichosisitiza kuwa swrikali iweke juhudi za kusomesha wanawakw zaidi ili huko baadae(sio jambo la mara moja) hili suala lipungue ama aliondoke kabisa.

Au huo utaalamu wanawake hawana uwezo wa ku master ?
 
Sheria inaruhusu kupata huduma kwa mtoa huduma unayemtaka, kwa hiyo ukiona anayekupa huduma ni jinsia usiyeitaka kataa ili uende kwa hiyo jinsia unayotaka ikupe huduma,..na kama utakuwa kwenye hali ya dharura,kuokoa maisha na umekataa itabidi uandike ili ukifa mtoa huduma awe safe.
Tuletee hiyo sheria tupate kufaidika mkuu.

Kusema peke ake haitoshi
 
Halafu wenyewe wanachukulia powa tu eti kwa vile ni hospitali.
Kuna siku nilienda kufanyiwa utrasound sasa nimeingia maabara kuna kaka mmoja akawa ananipima huku nikiwa uchi kitandani basi nikashangaa kuna mdada mmoja nesi anaingia tu mle ndani halaf anaona mimi niko uchi wala hashtuki akawa anatafuta sijui vikorokoro gani,aisee nilikasirika nikasema nitadeal naye nje ya hospitali tumalize mchezo kabisa
Hahahahaah
 
Mimi nishawahi kukatisha dose ya sindano nilikuwa nachomwa sindano na nesi wa kike sindano ya mwisho nikamkuta mwamba ndio yuko zamu nikajisemea moyoni hii tunu nitaitunza kwa gharama yoyote hugusi ta.ko langu nikajichenga na malaria yangu tatu
 
Back
Top Bottom