Serikali; mzazi anayetaka na kudai matunzo ya mtoto asikae na Mtoto. Full stop!

Serikali; mzazi anayetaka na kudai matunzo ya mtoto asikae na Mtoto. Full stop!

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
SERIKALI; MZAZI ANAYETAKA
NA KUDAI MATUNZO YA MTOTO ASIKAE NA MTOTO. FULL STOP!

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Hii iwe kwa Mzazi wa kike au wakiume. Yaani Baba au Mama.

Huruma sio malezi.
Mmeamua kuachana msisumbue watu hapa.

Mmeamua kuzalishana huko msisumbue watu. Watoto ni wenu. Msipowapenda ninyi huko serikali na watu wengine hawana muda nao. Haki za watoto wakwanza kuzijua ni ninyi mliozaa huyo mtoto.

Siku hizi wanaume wanalea na kujtunza watoto wao vizuri tuu tena kuliko hata wanawake wengi.

Ukitaka mtunze kwa pamoja mtoto wenu. Ishini pamoja. Hamtaki kuishi pamoja sasa hapo tunakuja kwenye maslahi ya mtoto. Mwenye uwezo wa kumtunza ndiye akae na mtoto basi.

Serikali iweke sheria kwamba, anayekaa na mtoto ndiye anatakiwa kuhusika kwenye matunzo ya mtoto kwa asilimia kubwa kama sio asilimia mia moja.

Anayebisha ni kwamba hana uwezo wa kukaa na mtoto. Hana vigezo na sifa za kuishi na mtoto ndio maana anakataa.
Hii itachochea watu kufanya kazi na kujitegemea. Itapunguza utegemezi.

Lakini pia itaondoa migogoro ya kipumbavu na kipuuzi inayoendelea. Kwenye jamii.

Wewe unakaa na mtoto. Unajifanya ni mzazi sijui Mama sijui Baba. Lakini uwezo wa kutunza huna,unategemea matunzo kutoka kwa mzazi mwingine. Nini kinakufanya usimpe huyo mzazi mwingine huyo mtoto kama sio uchizi, na ukichaa,na ukatili?

Nawajua watoto wengi waliolelewa na Mama zao bila Mama hao kusumbua Baba zao. Wamama wanafanya kazi,wanavipato wanatunza watoto wao bila kusumbua watu.
Sasa wewe mwanamke kwa nini uzae mtoto alafu unashindwa kutunza watoto uliowazaa mwenyewe? Unashindwa hata na wanyama? Kama huwezi kutunza mtoto kwa nini uzae sasa? Alafu mbaya zaidi unang'ang'ania kuishi na mtoto uwezo wa kutunza zero. Upuuzi tuu.

Anayekaa na mtoto ndiye anajua mtoto aishije. Anastandrd zake. Anasheria na malezi anayoyajua yeye. Anamtazamo wake kwamba mtoto kuishi vizuri ni nini kwa mtazamo wake. Sasa hayo yote gharama yake unampa ambaye hakai na mtoto hizi Akili za wapi?

Wanawake wa Tibeli wanalea watoto wao bila kusumbua wengine. Hawawezi kuzaa mtoto kwa kutegemea atatunzwa na mtu mwingine. Vipi huyo mtu mwingine asipokuwepo? Akifa? Mkiachana.
Ndio maana siku zote wanawake wa Tibeli ni wanawake bora na wapo juu ya wanawake wengine kimtazamo, kiuzuri, kiuchumi kwa sababu wanajitegemea.

Hatuwezi kuwa na visheria vinavyochochea na kuhamasisha watu kuwa wavivu.
Kuchochea wanawake kuwa wavivu na tegemezi.

Kwamba mimi mwanamke ninazaa zangu. Alafu matunzo atatoa mwanaume. Kama chizi vile. Ndio haya yanasumbua watu huko maofisini.

Mwanamke mchapakazi, mwenye akili, anayejitambua,mzalishaji suala la kutunza mtoto kwake ni lalazima. Hasa mtoto akiwa mikononi mwake. Sio kujidhalilisha.

Panya aweze kulea watoto wake. Kuku, mbuzi. Wewe unayejiita mtu mwenye akili unataka kukaa na mtoto alafu matunzo atoe asiyekaa naye. Ni lijinga tuu litakuwa ma mtazamo wa hivyo.

Halikadhalika na mwanaume.
Kuna wanaume nao wanapenda kulazimisha kukaa na watoto alafu uwezo halina.
Kazi yenyewe kuungaunga. Kula ya tabu. Hapana. Huo ni uhuni.

Kama mwanamke uliyezaa naye anauwezo wa kutunza mtoto. Muachie mtoto. Malezi na maadili hiyo ni ishu nyingine alafu ni rahisi sana kuliko mambo ya matunzo na mahitaji.

Sisi Watibeli hatuoni shida. Kama mwanamke anauwezo wa kutunza mtoto. Tunamuachia fresh tuu lakini hatutaki usumbufu.

Huwezi sema unaupendo na mtoto alafu huna uwezo wa kumtunza. Wamama wengi wanakuambia tunaupendo na watoto lakini hayana huo upendo zaidi ya blah blah blah.

Ukitaka kujua Mama yako anakupenda. Angalia anavyokuhudumia kama halalamiki kwa kumhusisha Baba yako ujue huyo anakupenda.
Lakini kama anakutunza na kukuhudumia alafu muda huohuo anaona anachokifanya angetakiwa kukifanya Baba yako ujue hapo hamna kitu. Hapo huna Mama. Ni vile alikuzaa tuu.
Kwa sababu huo sio upendo bali unyanyasaji.

Mwambie kabisa ni wajibu wako Mama kunitunza. Kama ulishindwa nipeleke Kwa Baba yangu mzazi. Yeye hatashindwa. Kama hunipeleki nitaenda mwenyewe.
Halikadhalika na Baba.

Hakuna udhuru kwenye kutunza mtoto. Anayekaa na mtoto ndiye anawajibika.

Serikali, kama mtu analeta kesi za kijinga kama hizi. Kwamba sijui Baba yake haleti matumizi. Imuite huyo Baba, kisha imwambie kwamba huyu Mama ameshindwa kumtunza mtoto, na wewe Baba umeshindwa kutoa pesa ukiwa mbali. Mchukue mwanao ukamlee kwako. Simple!

Sio kujifanya unauchungu na watoto alafu kutunza huna uwezo. Huo uchungu wa kijinga.

Nimemaliza!

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Subiri wanakuja hapa, kutolea ufafanuzi mujarabu.
😂😂😂
 
Subiri wanakuja hapa, kutolea ufafanuzi mujarabu.
😂😂😂

Sasa unataka matunzo ya mtoto kwa nini usimpe mwenye uwezo wa kutunza?

Utasema hana muda wa kulea kutokana na kazi.
Ni wanawake wangapi wanafanya kazi za kuajiriwa wanaondoka asubuhi na mapema na kurudi usiku. Watoto wanaacha kwa mayaya?

Familia zote kubwa duniani mpakq kza kifalme. Watoto wanalelewa na mayaya.
Mama na Baba kazi zao ni usimamizi na maelekezo.
 
Back
Top Bottom