DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Simu nyingi zina option ukifuta picha kuna sehemu zinakaa kwa muda au walikuwa wajanja wakafuta mpaka huko?
 
Noma sana, hii ya kuchezea odometer inafanywa sana, wanajua wabongo wengi wanaangalia uchache wa mileage na sio service history. Kwa hiyo wanarudisha odo nyuma ili kutupa tunachokipenda.

Hongera kwa kupata milioni 1 na bado umefichua uovu. Sasa hapo polisi nao wanakwenda kujipatia hela huko.
Kabisa, yaani ushawapa police Chaka
 
Mzee alinunua land cruiser ila mpaka Sasa ashakua fundi garage🤣🤣 jinsi Chuma inavomsumbua ni miaka kama SITA ila bado anaishi nayo
Mzee anafanya makosa makubwa ya kiufundi ndiyo maana linakuwa ni "spana mkononi".

Hilo akilipeleka gereji zenye kueleweka mbona atapumzika?

Ila kabla ya kulipeleka ajipange kwanza kiuchumi.

Kuna watu wananunua magari ya minada yaliyotumika hadi yakashindikana kwenye mataasisi huko na hayatembei.

wakishakuyanunua huyapeleka kwenye gereji mahsusi zenye kuaminika ili kuyafufua.

Yakishafika gereji hukaguliwa magonjwa pamoja na mapungufu kisha kununuliwa genuin spare parts na kufungwa na kurudi barabarani kama kawaida.

Sembuse gari amenunua yard limsumbue!
 
Wewe mtoa mada,hao wauza magari na Serikali yenu wote wezi.Wewe kwa kukubali rushwa na kuwaacha hao maana yake umeendele kuleo huo ujinga na watu wengi wataendelea kuumia.

Ningekyona wa maana kama ungesema yard XXX inafanya XXX watu waende kuchukua hatua,kwa kuficha nina la yard huna tofauti na uovu wanaufanya hao
 
Serikali itupie macho uhuni unaofanywa na hawa wafanyabiashara wa magari wenye asili ya Pakistan.

Jana mida ya saa sita mchana tulienda na rafiki yangu kwenye moja ya maduka (yard) ya kuuzia magari. Rafiki yangu alikuwa anataka Toyota Probox kwa ajili ya kubebea mizigo yake Kariakoo na kwenye godown yake.

Tukafika hiyo saa sita tukakuta magari ndiyo yanapangwa. Walivyomaliza tukaomba kukagua gari moja. Kijana akaitwa akaja mbio na funguo za gari zikiwa mkononi kwake.

Nikakaa kwenye usukani na rafiki yangu pembeni. Nilipoiweka gari switch on nikakuta odometer inasoma gari imetembea kilometa 219,551. Bei milioni 16

Tukashauriana tukasema hapana hili gari halifai. Tukaendelea duka jingine na jingine na jingine.

By saa tisa tukafudi tena kwenye ile Probox, tukakuta ishachezewa odometer, sasa inaonekana imetembea kilometa 46,755.

Nilikuwa nimeoiga picha chasis namba mlangoni na dashboard. Nikipowauliza mbona hii gari mmeichezea kilometa, nikawaonyesha na picha wakakasirika sana wakapora simu yangu. Nikawaambia kaeni nayo, leo mtalala polisi.

Nikawa naondoka kulekea kwenye gari tuliyokuja nayo hapo yard, ndipo mmoja ya wafanyabiashara wale akaja mbio huku akinibembeleza nifute zile picha watatupa million moja.

Hela tamu, tukakubali kufuta picha, tukabeba milioni yetu. Tukaondoka.

Lakini backyard ya hizo yard zote kuna mafundi wako busy wanayaweka sawa mamikweche hayo.

Kingine tulichogundua ni kwamba kwenye minada ya magari, magari ya nauzwa kwa classes. Hawa wanachagua class duni kabisa, yakifika hapa wanaongea vizuri na wakaguzi, wanatolewa bandarini.

Kwa somo hili tulilojifunza jana rafiki yangu amekata tamaa kabisa na magari haya. Sasa kaona bora aagize kutoka Japan [emoji557] asubiri siku 45 abebe mwana wake wa uhakika
Kuwa tajiri siyo mchezo .mpk mtu amemiliki Mali Tanzania ujue kafanya sarakasi nyingi Sana, period

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Tanzania yenye watu kama wewe itazidi kuwa na matatizo tu, kwa sababu watu wenyewe hamjawa na nia thabiti ya kuyamaliza hayo matatizo.

Mna kisebusebu na kiroho papo.

Huna haki ya kulalamika, ushakula rushwa.
Haya umemaliza hamu zako?
 
Miye na Japani damu damu,na hivi sina utaalamu aaanh Beforward mko wapi? Nachukua mkebe wangu nduki.
 
Usikute huo ujanja wa kuchezea odometer wamefundishwa na wabongo, maana ana ujanja wa uharibifu na sio wa ubunifu
Nakumbuka juzi TRA wakati wanatoa training ya UPGRADED E FILLING SYSTEM mkufunzi alisema "najua kuna watu wamekuja ili kuijua system na kuichezea kufanya uharibifu
Tafadhini acheni"
Sisi ndo wabongo bwana.
 
Mkuu hata uwapeleke mbinguni askari wa Tanzania hawawezi kuishi bila rushwa, hii ni kutokana na mishahara yao ni midogo mno. Askari polisi wa Tanzania ukikutana nao wamevaa gwanda, ndiyo wanaonekana wa maana. Kaangalie wanapoishi, hawana tofauti na wale ombaomba wanaolala viwanja vya mnazi mmoja.
Unaijuwa mishahara ya askari?
 
Mzee anafanya makosa makubwa ya kiufundi ndiyo maana linakuwa ni "spana mkononi".

Hilo akilipeleka gereji zenye kueleweka mbona atapumzika?

Ila kabla ya kulipeleka ajipange kwanza kiuchumi.

Kuna watu wananunua magari ya minada yaliyotumika hadi yakashindikana kwenye mataasisi huko na hayatembei.

wakishakuyanunua huyapeleka kwenye gereji mahsusi zenye kuaminika ili kuyafufua.

Yakishafika gereji hukaguliwa magonjwa pamoja na mapungufu kisha kununuliwa genuin spare parts na kufungwa na kurudi barabarani kama kawaida.

Sembuse gari amenunua yard limsumbue!
Ukinunuwa gari mbovu towa engine weka engine nyingine used shughuri imekwisha.

Siku hizi Kwa mafundi inatakiwa uende kufanya service tu siyo kutafuta ugonjwa wa gari.
 
Bado ninajiuliza kimaadili, hiyo millioni mliipokea ni ya kazi gani!

Tusipigie kelele mambo tunayoyahusudu na kuyatenda.
Mtu anakula rushwa kuficha ushahidi, akishirikiana na matapeli.

Halafu anailalamikia serikali imsaidie.

Serikali itakusaidia vipi wakati ushakula rushwa kuharibu ushahidi?

Hao ndiyo wabongo wengi walivyo.

Contradictions.
 
TBS wapo busy kukimbizana na akina mama walala hoi pale Kasumulu border, wanaohangaika na vibiscuits!,hii nchi ni shida kila kona!,pls my IGP chukua hawa police wako peleka Botswana,even for a 14days waone wenzao wanavyofanya kazi ,Tanzania bila RUSHWA INAWEZEKANA, why Gaborone wamefanikiwa kwa hili?,Zambia wanasogea nao kuwa wasafi sisi tumekwama wapi
tatizo ccm
 
Back
Top Bottom