Mafian cartel
JF-Expert Member
- Nov 19, 2021
- 3,876
- 7,118
Wana backupMsomali na Mpakistani wengi wao wanapiga issues haramu na wanajiamini kishenzi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wana backupMsomali na Mpakistani wengi wao wanapiga issues haramu na wanajiamini kishenzi.
Walikukosaje eleza kidogo mkuuHawa waliwahi kunikosakosa maeneo ya Aghakan,nilipowastukia wakaniambia watanipigia simu,baada ya kuona kimya nikawapigia simu ikawa inaita bila majibu,nikaona baadaye kama walini blacklist maana ilikuwa haipatikani tena...
Kabisa, yaani ushawapa police ChakaNoma sana, hii ya kuchezea odometer inafanywa sana, wanajua wabongo wengi wanaangalia uchache wa mileage na sio service history. Kwa hiyo wanarudisha odo nyuma ili kutupa tunachokipenda.
Hongera kwa kupata milioni 1 na bado umefichua uovu. Sasa hapo polisi nao wanakwenda kujipatia hela huko.
Mzee anafanya makosa makubwa ya kiufundi ndiyo maana linakuwa ni "spana mkononi".Mzee alinunua land cruiser ila mpaka Sasa ashakua fundi garage🤣🤣 jinsi Chuma inavomsumbua ni miaka kama SITA ila bado anaishi nayo
Kuwa tajiri siyo mchezo .mpk mtu amemiliki Mali Tanzania ujue kafanya sarakasi nyingi Sana, periodSerikali itupie macho uhuni unaofanywa na hawa wafanyabiashara wa magari wenye asili ya Pakistan.
Jana mida ya saa sita mchana tulienda na rafiki yangu kwenye moja ya maduka (yard) ya kuuzia magari. Rafiki yangu alikuwa anataka Toyota Probox kwa ajili ya kubebea mizigo yake Kariakoo na kwenye godown yake.
Tukafika hiyo saa sita tukakuta magari ndiyo yanapangwa. Walivyomaliza tukaomba kukagua gari moja. Kijana akaitwa akaja mbio na funguo za gari zikiwa mkononi kwake.
Nikakaa kwenye usukani na rafiki yangu pembeni. Nilipoiweka gari switch on nikakuta odometer inasoma gari imetembea kilometa 219,551. Bei milioni 16
Tukashauriana tukasema hapana hili gari halifai. Tukaendelea duka jingine na jingine na jingine.
By saa tisa tukafudi tena kwenye ile Probox, tukakuta ishachezewa odometer, sasa inaonekana imetembea kilometa 46,755.
Nilikuwa nimeoiga picha chasis namba mlangoni na dashboard. Nikipowauliza mbona hii gari mmeichezea kilometa, nikawaonyesha na picha wakakasirika sana wakapora simu yangu. Nikawaambia kaeni nayo, leo mtalala polisi.
Nikawa naondoka kulekea kwenye gari tuliyokuja nayo hapo yard, ndipo mmoja ya wafanyabiashara wale akaja mbio huku akinibembeleza nifute zile picha watatupa million moja.
Hela tamu, tukakubali kufuta picha, tukabeba milioni yetu. Tukaondoka.
Lakini backyard ya hizo yard zote kuna mafundi wako busy wanayaweka sawa mamikweche hayo.
Kingine tulichogundua ni kwamba kwenye minada ya magari, magari ya nauzwa kwa classes. Hawa wanachagua class duni kabisa, yakifika hapa wanaongea vizuri na wakaguzi, wanatolewa bandarini.
Kwa somo hili tulilojifunza jana rafiki yangu amekata tamaa kabisa na magari haya. Sasa kaona bora aagize kutoka Japan [emoji557] asubiri siku 45 abebe mwana wake wa uhakika
TrueKuwa tajiri siyo mchezo .mpk mtu amemiliki Mali Tanzania ujue kafanya sarakasi nyingi Sana, period
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Very long time agoJABA....😂😂
Wivu unakusumbua. Fidia kwa harassment niliyopataBado ninajiuliza kimaadili, hiyo millioni mliipokea ni ya kazi gani!
Tusipigie kelele mambo tunayoyahusudu na kuyatenda.
Je una experience na car importation ya muda gani?Siku 45 hilo gari linakuja kwa mtumbwi au wajapani wanajitwisha wanakuletea kama mkungu wa ndizi.
Haya umemaliza hamu zako?Tanzania yenye watu kama wewe itazidi kuwa na matatizo tu, kwa sababu watu wenyewe hamjawa na nia thabiti ya kuyamaliza hayo matatizo.
Mna kisebusebu na kiroho papo.
Huna haki ya kulalamika, ushakula rushwa.
Nakumbuka juzi TRA wakati wanatoa training ya UPGRADED E FILLING SYSTEM mkufunzi alisema "najua kuna watu wamekuja ili kuijua system na kuichezea kufanya uharibifuUsikute huo ujanja wa kuchezea odometer wamefundishwa na wabongo, maana ana ujanja wa uharibifu na sio wa ubunifu
Unaijuwa mishahara ya askari?Mkuu hata uwapeleke mbinguni askari wa Tanzania hawawezi kuishi bila rushwa, hii ni kutokana na mishahara yao ni midogo mno. Askari polisi wa Tanzania ukikutana nao wamevaa gwanda, ndiyo wanaonekana wa maana. Kaangalie wanapoishi, hawana tofauti na wale ombaomba wanaolala viwanja vya mnazi mmoja.
Ukinunuwa gari mbovu towa engine weka engine nyingine used shughuri imekwisha.Mzee anafanya makosa makubwa ya kiufundi ndiyo maana linakuwa ni "spana mkononi".
Hilo akilipeleka gereji zenye kueleweka mbona atapumzika?
Ila kabla ya kulipeleka ajipange kwanza kiuchumi.
Kuna watu wananunua magari ya minada yaliyotumika hadi yakashindikana kwenye mataasisi huko na hayatembei.
wakishakuyanunua huyapeleka kwenye gereji mahsusi zenye kuaminika ili kuyafufua.
Yakishafika gereji hukaguliwa magonjwa pamoja na mapungufu kisha kununuliwa genuin spare parts na kufungwa na kurudi barabarani kama kawaida.
Sembuse gari amenunua yard limsumbue!
Mtu anakula rushwa kuficha ushahidi, akishirikiana na matapeli.Bado ninajiuliza kimaadili, hiyo millioni mliipokea ni ya kazi gani!
Tusipigie kelele mambo tunayoyahusudu na kuyatenda.
tatizo ccmTBS wapo busy kukimbizana na akina mama walala hoi pale Kasumulu border, wanaohangaika na vibiscuits!,hii nchi ni shida kila kona!,pls my IGP chukua hawa police wako peleka Botswana,even for a 14days waone wenzao wanavyofanya kazi ,Tanzania bila RUSHWA INAWEZEKANA, why Gaborone wamefanikiwa kwa hili?,Zambia wanasogea nao kuwa wasafi sisi tumekwama wapi