Serikali: Visa vya COVID-19 vyafikia 53. Vyuo na Shule kuendelea kufungwa hadi Serikali itakapotoa tamko jingine


Ndalichako kapiga marufuku ‘twisheni’ zote, unaleta ukaidi.?
 
Tuache masihara tuige mfano wa Wachina, hii kusema eti utoaji wa taarifa za kutosha za gonjwa hili zinatutia hofu ndicho kitakachotumaliza, mimi nafikiri serikali ingeweka wazi zaidi taarifa za maambukizi ni maeneo gani hasa waathirika wamepatikana, itaje angalau mpaka kitongoji au mitaa na jinsi waathirika walivyopata maambukizi.

Hii itasaidia watu wengine kuchukua tahadhari zaidi maanake unaambiwa tu kuna watu kadhaa wameongezeka lakini hujui hata watu hao ni wa mtaa gani, inawezekana hata ni jirani yako wewe hujui. Sisemi wagojwa watajwe au picha zao zitolewe hapana bali taarifa zitolewe kwa mapana zaidi kama ilivyokuwa kwa yule mgojwa wa kwanza kabisa Isabela.
 
Kuna tatizo mahali,huyu pm atakuwa hayuko poa na mteuzi wake,ni kama magufuli anataka shule zifunguliwe ila vion GH ozi wengine hawataki,kuna jambo haliko sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 


What's wrong with PM's Office?

Inakuwaje Tangazo ambalo ni so official linatoka PM analisoma na linakuwa na makosa ya namna hii?

Makosa ni haya:

1. Tarehe 26, April kila mwaka ni kumbukumbu ya sherehe za Muungano wa Tanganyika & Zanzibar siyo Mapinduzi ya Zanzibar!!

2. Sherehe za kukumbuka Mapinduzi ya Zanzibar (Zanzibar Revolution) kila mwaka ni tarehe 12, January

3. Kikatiba ni nani mwenye mamlaka ya kuisemea SMZ kwenye mambo yasiyo ya Muungano? Hili la sherehe za Mapinduzi PM, Majaliwa ama Rais Magufuli hawezi kulisemea. Labda kwa kuwa mmekosea kuliandika hivyo!!

Sijui ni kwa nini hata Waziri Mkuu mwenyewe hakugundua makosa ya wazi kabisa ya namna hii...!!!??
 
Ni kweli hivi virusi vya corona vinapenda hali ya baridibaridi

Hizi siku 4 za hali ya mvua na mawingumawingu maambukizi yameongezeka kwa kasi sana

Jamani watu wa dar tumuombe Mungu atuletee jua kali sana ndio kinga bora kabisa ya corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ndo tunapofeli
Sijui kwanini hakuna hizi takwimu za wanaopimwa Ni wangapi

Tz tunachukulia Hilo Jambo kisiasa na sio kisayansi.... Ulisikia ushauri wa Mwiguru?.


Mpaka leo Uganda wamepima watu takribani 5600 na walio na maambukizi ni 54
Sisi tumepima wangapi mpaka leo?


Sent using Jamii Forums mobile app

Upo sahihi

Ikiwezekana watangaze taarifa za Corona kila siku... Watangaze majina ya waliokufa maana kifo sio Siri na hii itazuia kuenea huu ugonjwa.... Watangaze na waliopimwa, waliopo karantini na wanaopona kila siku...

Kuna mabilioni ulipwa mashulen kila mwezi sasa mashule yamefungwa hayo mabilion ya mwezi 1yanaweza kupambana na corona

Kwani Hadi Sasa serikali imeshakusanya shilingi ngapi?... Tuwe tunapewa mrejesho wa pesa zilizokusanywa Tz kwaajiri ya covd19.
 
opondo,
Hata kama mtu ana uhitaji wa mwalimu hawezi kukupa ww, una matatizo ya herufi H, angalia hapo ulipoandika Hila, pia hapo ulipoandika Hiki badala ya Ili. Nyie ndio wale mkipewa mwanafunzi wa kike unaishia kumpa account ya facebook.
Hili tatizo la kuchanganya herufi kwa kweli limekithiri na linaudhi kweli kweli unakuta mpaka taasisi za elimu nazo zinakosea kuandika jina la shule. Mfano kule Mwanza nilishuhudia kibao cha shule kimeandikwa shule ya msingi Kishili badala ya Kishiri unategemea wanafunzi wajifunze nini hapo.
 
Imekuwa kawaida walimu na wahazili huamka kwenda ofisini na kurudi nyumbani nothing to do, mbona wasijiongeze kuwawezesha wanafunzi wao kipondi hili cha lockdown ya corona

Hili wazo lako ni zuri, suala la wahadhiri kuwawezesha wanafunzi wao ( sijajua kuwawezesha kwa njia ipi) ni suala ambalo linatakiwa litolewe utaratibu na serikali na vyuo vitekeleze, wala sio suala la chuo husika kwa sababu zifuatazo:
1. Hakuna chuo kitakuwa na muhula wa masomo wa peke yake.
2. Hakuna chuo kitakuwa na utaratibu wa udahili wa peke yake isipokuwa tu ule ambao umetolewa na Regulatory authorities ( NACTE na TCU).
Na pia ikumbukwe kuwa mwanafunzi aliyedailiwa kusoma darasani kumbadilishia asome kwa njia ya mtandao anahitaji kuandalia, maana wengi wanatumia sana mtandao wanapokuwa chuoni maana vyuo vingi vina wi-fi, akiwa huko kwao kijijini mtandao atautoa wapi!

So, tusubiri mwongozo wa serikali, wala chuo kisijichukulie utaratibu wake ambao hata mamlaka zinazokisimamia hazijatoa utaratibu. Ila kujiandaa katika mfumo huo ni vizuri zaidi.
 
Nani kathibitisha wanaugua na kupona kimya kimya hebu prove au ni story za viniweni tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…