Serikali: Wanafunzi waliopata mimba kuendelea na Masomo katika mfumo rasmi

Serikali: Wanafunzi waliopata mimba kuendelea na Masomo katika mfumo rasmi

Serikali imeruhusu wanafunzi wa kike wanaopata mimba kurejea shuleni baada ya kujifungua na kuendelea na masomo.

Hii imo kwenye Ilani ya uchaguzi ya Chadema ya 2020 iliyoandaliwa chini ya Freeman Mbowe na kunadiwa nchi nzima na Tundu Lisu.

Hongereni sana Chadema kwa kuwapigania wanafunzi wa kike.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ipo pia kwenye ilani ya CCM,ni ulimbukeni tu wa mwendazake!
 
Mi nasikitika suala la kijana kufungwa miaka30 kwann wasifungwe wote
Pic%20Layer_2021111311215721.jpg
 
Kwa hivi vitoto vya farao sio siri serikali itajua haijui. ukimtia mimba mwanafunzi chap kwa wazazi wake mnayamaliza kifamilia na kwa kuwa mshua anajua mwanae mwaka kesho atarudi shule basi unampoza kidogo then anaweka mambo sawa life linasonga. Baada ya miaka miwili tutaona matokeo ya huu waraka umeopendwa na wengi (Mimi na Mwendazake excluded)
 
RUKSA: WANAFUNZI WAJAWAZITO WAENDELEE NA MASOMO.

Na: Baraka Odingo

Ujumbe: Natumpige mzungu bao la mkono, kabla ajatupiga bao la kichwa.

Kwanzia Novemba 24, 2021 wanafunzi wajawazito kwa mujibu wa serikali wataruhusiwa kurudi shuleni ndani ya kipindi cha miaka miwili baada ya kujifungua. Ili kumpa mtoto huyu ambae keshakuwa mzazi wa mtoto mwenzie haki yake ya msingi ya kupata elimu.

Lengo hili la Serikali lililoshinikizwa zaidi na wahisani kupitia misaada yao ya fedha na mikopo ni zuri na wahisani pia maono yao ni mema tuliopokee.

Binafsi sipingi maamuzi ya serikali, japo ningekuwa mwamuzi nisingekubali.

Hata hivyo ni vema kubaini tatizo ndani ya jambo na kulitafutia suhulu ili lisilete shida mbeleni.

Hivyo suluhu hapa ni:
Kwamza ni kulipokea na kulitekeleza bila ubishi kwani mambo ubadilika tusiishi kwa mazoea.

Pili, nakazia maarifa kuwa kuwaruhusu warudi shule ndani ya miaka miwili si sawa kabisa tutawapoteza mabinti wengi sana, ni bora waendelee na shule wakiwa wajawazito, muda wa kujifungua ukikaribia wajifungue, wanyonyeshe miezi mitatu mfululizo kisha warudi shuleni wakiwa na wanao. Yaani kama ilivyokwa wafanyakazi wa umma.

Tatu, tujiandae kuwapeleka mabinti zetu kuchoma sindano, kupandikiza vijiti, kufunga kitanzi au kutumia vidonge vya uzazi wa mpango japo awajazaa ili viwanda vya wahisani viendelee kuzalisha bidhaa tiba hizi kisha watoe tena misaada ya uzazi wa mpamgo ili wapate upendeleo wa kuchukua rasilimali: dhaabu, urenium, gesi, mafuta makaa zetu bila gharama kubwa.

Wakati huu lengo la pili la mhisani la kupunguza idadi/wingi wa mwafrika litimie pale mabinti hawa watakapo kufa wakati wakujifungua na pia kushindwa kulea mimba ukubwani baada ya kuvuruga mfumo wao wa uzazi tangu wakiwa wadogo.

Tulitumia Hofu (kuwapima mimba wanafunzi kila muhula) na adhabu (kuwafukuza shule) kuwalinda wasishiriki ngono na kupata mimba.

Lkn leo tumeondoa Hofu na Adhabu tumeamua kufungulia bomba la ngono na mimba za utotoni. Ngono za utotoni kwa wanafunzi ruksa, mimba ruksa.

Nne, nashauri shule ziwe na nursing Centre - binti akisha jifungua arudi shule akiwa darasani mtoto awe analelewa huko, break anaenda kunyinyesha. La! wengi awatarudi shule kwa kuelemewa na jukumu la malezi na uwezo wa kuajiri walezi nyumbani hawana.

Tano, nashauri kama wazazi na walezi tujikite kuwaelimisha wenetu juu ya hatari hii waliyonayo ili balaa liwaepuke.

Sita, kumpiga mzungu bao la mkono, tusiwaruhusu binti zetu kutumia uzazi wa mpango wasijewakakosa kuzaa katika ndoa zao ikawa shida, majuto na dhahama. Badala yake wazae tu waje na wanao shuleni wasome huku wanalea ili lengo la mhisani la kupunguza idadi ya watu lisifanikiwe zaidi waongezeke tena wakiwa wemesoma.

Saba, wakati mwingine badili hasi kuwa chanya. Jambo hili lina hasara lkn tunaweza badili hasara kuwa faida kinachotakiwa ni kuacha kuishi kwa mazoea.

#LindaTanzaniayaleoJengaTanzaniayaKesho.
 
Mbona Waziri wa Elimu anajichanganya. Wakati wa awamu ya tano walifyata mkia. Sasa hivi Magufuli hayupo kila mtu anatoa tamko. Kwa nini usiwe na msimamo hata ukipoteza uwaziri wako?. Namshangaa sana.
 
Uamuzi wa kuruhusu mwanafunzi-mtoto kupata mimba pia uruhusu ndoa za utotoni. Angalau mtoto-mke anakuwa na mme wa kumtunza na kumwendeleza. Huyo aliyepata mimba hakika atakuwa mzigo kwa wazazi/walezi wake.

MIMI SIAFIKI KABISA. Ni uamuzi wa kishetani. Uamuzi wa kishetani kwa kuwa anayemtia mimba huyo mwanafunzi-mtoto hupata kifungo cha miaka 30. Je, iwapo ni mwanafunzi mwenzake atakuwa amepoteza nafasi ya elimu.

UPUUZI mtupu
 
Mawazo ya kale kabisa na ya kishamba. Wewe binti akirudi kusoma atakuathiri nini? Kama kufukuza shule kungesolve tatizo la mimba shuleni basi zingekuwa zimetoweka. Mtu hata akimaliza form 4 na watoto watatu ni sawa tu.
 
Siamni kama tunaruhudu huu mpango huu, kwahiyo akipata mimba ya pili inakuwaje.
Ivi tunafikiri vizuri kweli?????.

R.I.P Late JPM.
 
Mawazo ya kale kabisa na ya kishamba. Wewe binti akirudi kusoma atakuathiri nini? Kama kufukuza shule kungesolve tatizo la mimba shuleni basi zingekuwa zimetoweka. Mtu hata akimaliza form 4 na watoto watatu ni sawa tu.
Alafu utamlelea wewe hao watoto?? Amaunaongea kama umekatwa kichwa.
Unajua atakae mpa mimba atakuwa wapi!!.
 
Mbona badoo mambo yako mbele huko mtachoka mwenyewe tuombe uzima tyu
20211125_115710.jpg
 
Alafu utamlelea wewe hao watoto?? Amaunaongea kama umekatwa kichwa.
Unajua atakae mpa mimba atakuwa wapi!!.
Aliempa mimba ni mbakaji, atakuwa jela. We unataka kumnyima elimu muhanga wa kubakwa? Ndiyo akili hiyo!!
 
Tunaelewa matokeo ya misaada ya mabeberu hayo!

Tunasubiria sharti la wanafunzi kuruhusiwa kulana viboga sasa.
We nakufahamu baba ako alimbebesha mamayo mimba akiwa nyumbani kwao,sasa unaachama nn,acha watoto wasome hutaki hamia burundi,,yani tutengeneze kizazi cha wajinga eti kisa walibeba mimba!!!!!!!?
 
Mawazo ya kale kabisa na ya kishamba. Wewe binti akirudi kusoma atakuathiri nini? Kama kufukuza shule kungesolve tatizo la mimba shuleni basi zingekuwa zimetoweka. Mtu hata akimaliza form 4 na watoto watatu ni sawa tu.
Kabisa mkuu. Hii itafacilitate hao wadada wa persue dreams zao na kutokua tegemezi hapo baadae. Heko kwa mama Ndalichako kwa kugundua hao wadada wasiposoma jamii ndio inaathirika zaidi kulea huo mzigo.
 
Hahaha

1.Na waotia mimba isiwe kesi wafikiriwe

2.Akipata mimba ya pili anakaa miwili nyumbani anarudi tena ahaaaa ya tatu je

Haya ndo mambo tunayotaka hahaha

Imenifanya nikumbuke kipindi nasoma kuna essay zilikuwa na point za pande mbili zote na zote ni strong point inategemeana na upande utakao amua kutetea mambo haya yana wachache jamani.

#Watia mimba wanafunzi nao wafikiriwe kuja kulea watoto wao wasije watoto kukosa malezi ya baba na kama ni mwanafunzi asije kukosa elimu hitaji la msingi.

Ivi kwanini huwa wanafunga jela mzazi wq kiume tuu aha inakuwa kabaka sasa kama ni mwanafunzi(mzazi wa kiume ) bado inakuwa kabaka
 
Back
Top Bottom