RUKSA: WANAFUNZI WAJAWAZITO WAENDELEE NA MASOMO.
Na: Baraka Odingo
Ujumbe: Natumpige mzungu bao la mkono, kabla ajatupiga bao la kichwa.
Kwanzia Novemba 24, 2021 wanafunzi wajawazito kwa mujibu wa serikali wataruhusiwa kurudi shuleni ndani ya kipindi cha miaka miwili baada ya kujifungua. Ili kumpa mtoto huyu ambae keshakuwa mzazi wa mtoto mwenzie haki yake ya msingi ya kupata elimu.
Lengo hili la Serikali lililoshinikizwa zaidi na wahisani kupitia misaada yao ya fedha na mikopo ni zuri na wahisani pia maono yao ni mema tuliopokee.
Binafsi sipingi maamuzi ya serikali, japo ningekuwa mwamuzi nisingekubali.
Hata hivyo ni vema kubaini tatizo ndani ya jambo na kulitafutia suhulu ili lisilete shida mbeleni.
Hivyo suluhu hapa ni:
Kwamza ni kulipokea na kulitekeleza bila ubishi kwani mambo ubadilika tusiishi kwa mazoea.
Pili, nakazia maarifa kuwa kuwaruhusu warudi shule ndani ya miaka miwili si sawa kabisa tutawapoteza mabinti wengi sana, ni bora waendelee na shule wakiwa wajawazito, muda wa kujifungua ukikaribia wajifungue, wanyonyeshe miezi mitatu mfululizo kisha warudi shuleni wakiwa na wanao. Yaani kama ilivyokwa wafanyakazi wa umma.
Tatu, tujiandae kuwapeleka mabinti zetu kuchoma sindano, kupandikiza vijiti, kufunga kitanzi au kutumia vidonge vya uzazi wa mpango japo awajazaa ili viwanda vya wahisani viendelee kuzalisha bidhaa tiba hizi kisha watoe tena misaada ya uzazi wa mpamgo ili wapate upendeleo wa kuchukua rasilimali: dhaabu, urenium, gesi, mafuta makaa zetu bila gharama kubwa.
Wakati huu lengo la pili la mhisani la kupunguza idadi/wingi wa mwafrika litimie pale mabinti hawa watakapo kufa wakati wakujifungua na pia kushindwa kulea mimba ukubwani baada ya kuvuruga mfumo wao wa uzazi tangu wakiwa wadogo.
Tulitumia Hofu (kuwapima mimba wanafunzi kila muhula) na adhabu (kuwafukuza shule) kuwalinda wasishiriki ngono na kupata mimba.
Lkn leo tumeondoa Hofu na Adhabu tumeamua kufungulia bomba la ngono na mimba za utotoni. Ngono za utotoni kwa wanafunzi ruksa, mimba ruksa.
Nne, nashauri shule ziwe na nursing Centre - binti akisha jifungua arudi shule akiwa darasani mtoto awe analelewa huko, break anaenda kunyinyesha. La! wengi awatarudi shule kwa kuelemewa na jukumu la malezi na uwezo wa kuajiri walezi nyumbani hawana.
Tano, nashauri kama wazazi na walezi tujikite kuwaelimisha wenetu juu ya hatari hii waliyonayo ili balaa liwaepuke.
Sita, kumpiga mzungu bao la mkono, tusiwaruhusu binti zetu kutumia uzazi wa mpango wasijewakakosa kuzaa katika ndoa zao ikawa shida, majuto na dhahama. Badala yake wazae tu waje na wanao shuleni wasome huku wanalea ili lengo la mhisani la kupunguza idadi ya watu lisifanikiwe zaidi waongezeke tena wakiwa wemesoma.
Saba, wakati mwingine badili hasi kuwa chanya. Jambo hili lina hasara lkn tunaweza badili hasara kuwa faida kinachotakiwa ni kuacha kuishi kwa mazoea.
#LindaTanzaniayaleoJengaTanzaniayaKesho.