Serikali: Wanaoanza Biashara kutolipa Kodi ya Mapato kwa muda hadi wa mwaka mmoja

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Hello Wadau,

Naioongeza Serikali kwa kuchukua uamuzi huu utakaosaidia sana kutatua shida ya ajira na pia kuchochea vijana kujiajiri.

Tulikuwa wapi kumpata Rais kama Samia? Mungu ambariki.

====

Screenshot 2023-03-09 112755.png

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kibali cha kuruhusu wafanyabiashara wanaoanza biashara kutokulipa kodi kwa kipindi cha miezi sita hadi mwaka moja.

“Rais ametoa kibali, wale wanaoanza biashara kufanya biashara miezi sita hadi mwaka moja ndipo waanze kulipa kodi,” alisema. Alisema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Kondoa.

Alisema hilo linaonesha ni jinsi gani Rais Samia anawajali wananchi wake. “Ni vyema kila mmoja akauunga mkono juhudi za Rais katika kuwaletea wananchi maendeleo,” alisisitiza. Pia aliwataka wananchi kuachana na mikopo umiza na ile ya kausha damu kwani imekuwa ikiumiza wananchi kutokana na kuwa na riba kubwa.

“Halmashauri zimekuwa zikitoa mikopo ya asilimia nne, wananchi mwende mkope huko. Pia Rais Samia ametoa fedha kwenye Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) ambapo mikopo hutolewa kwa riba ya asilimia tisa,” alisema. Alisema kuwa mikopo yenye riba kubwa imekuwa ikiumiza wananchi huku wakiwa hawapati faida yoyote.

Chanzo: Habari Leo
 
“Rais ametoa kibali, wale wanaoanza biashara kufanya biashara miezi sita hadi mwaka moja ndipo waanze kulipa kodi,” alisema. Alisema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Kondoa.
Waswahili walivyo watakuwa wanaanza biashara kwa majina mapya kila mwaka
 
Hili lisiishie kuwa tamko bali itungwe sheria kabisa ili akiondoka madarakani,,,, basi sheria iendelee kufanya kazi.

Ila na nyinyi TRA,,, baada ya mtu kufanya hyo biashara kwa mwaka mzima, siku mnayokuja kumkadiria mtu kodi msimkomoe. Mana mnaweza kadiria kodi kubwa ili kufidia ule mwaka alofanya biashara bila kulipa kodi
 
👍👍
 
Kabisa mzee wanaweza sema uyu kapata income all year makadirio wanakupa makubwa.
 
Hili lisiishie kuwa tamko bali itungwe sheria kabisa ili akiondoka madarakani,,,, basi sheria iendelee kufanya kazi.

Ila na nyinyi TRA,,, baada ya mtu kufanya hyo biashara kwa mwaka mzima, siku mnayokuja kumkadiria mtu kodi msimkomoe. Mana mnaweza kadiria kodi kubwa ili kufidia ule mwaka alofanya biashara bila kulipa kodi
kumbe unawajua, jamaa lazima wafidie huo mwaka wa bure
 
Hili lisiishie kuwa tamko bali itungwe sheria kabisa ili akiondoka madarakani,,,, basi sheria iendelee kufanya kazi.

Ila na nyinyi TRA,,, baada ya mtu kufanya hyo biashara kwa mwaka mzima, siku mnayokuja kumkadiria mtu kodi msimkomoe. Mana mnaweza kadiria kodi kubwa ili kufidia ule mwaka alofanya biashara bila kulipa kodi
Unakadiriwaje kodi?
Kodi unajikadiria mwenyewe.
Na una uwezo wa kufanya marekebisho ya makadirio
 
Hii ndio serikali ya mama mchapa kazi na kazi ndio Hii.
 
Back
Top Bottom