Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Waswahili walivyo watakuwa wanaanza biashara kwa majina mapya kila mwaka
Ni upuuzi mwingine huuKwanza hii biashara ya kuuza mashine za EFD Ina ukakasi. Kwa Nini zisiwe ni Mali za TRA na wafanya biashara wanazichukua kutoka kwako na wanaingiziwa gharama yake katika makadirio Yako ya mwaka na utalipa kidogo kidogo mara nne kama ulipavyo Quarterly Provisions?
Kwani aliyeongea ni kanjanja au Waziri wa Biashara? Kwenye Bajeti ijayo litatungiwa Sheria na Wizara itaweka utaratibuMambo kama hayo inabidi umsikilize waziri mwenyewe sio waandishi wa habari makanjanja.
Mabadiliko yoyote makubwa ya kikodi kama hayo lazima yapite bungeni, yawasilishwe na waziri wa fedha na yawe sehemu ya finance act.
Raisi hana mamlaka hayo na kodi ni sheria sio swala la mtu kujiamulia tu.
Anafunga biasharaNIN, TIN?
[emoji2][emoji2] Aseee!! Kumbe ulishatangulia toka lini upo huko?Wanagawa na mitaji?
Ili ikiwezekana nitoke huku burundi nilikoambiwa nihamie na bwana mmoja hivi
Kwa ivyo unakubali sio sahihi kusema raisi ametoa kibali kwa jambo ambalo aliwezekani kutekelezeka bila ya bunge. Sasa ukisoma hiyo habari uoni huo ukanjanja kwa kusema raisi ametoa kibali?Kwani aliyeongea ni kanjanja au Waziri wa Biashara? Kwenye Bajeti ijayo litatungiwa Sheria na Wizara itaweka utaratibu
Kuna ule mchezo wa kusema biashara imefilisika kisha inaanza kwa jina jipya, nadhani waliutumia Sheraton, Moven pick Serena etcUtaratibu ni kwamba unasajiliwa, na unakua kwenye rekodi baada ya miezi sita au mwaka ndio makadirio huanza sasa
Anaanza baba, mwisho wa mwaka anasema amefilisika, anafungua mama, anafilisika wanapokea watoto etcUtabadili jina la NIDA kila mwaka?
Si kama makampuni yanavyofanya wanapopewa kipindi cha matazamioKwa mfumo wa sasa wa efilling utateseka sana.
Tecknolojia inakua. Tofauti na zamani Kuna link kati ya Brella na TRA na kila siku inaboreshwa. Ni risk sana kuwa na makampuni mengi yasiyofanya kazi. Na kufunga kampuni kuna gharama. Kwa mfumo wa sasa biashara ya kufungua na kufunga kampuni ni biashara kichaa. Itakugharimu tu, bora kama unaona hukui uachane na biashara.Si kama makampuni yanavyofanya wanapopewa kipindi cha matazamio
Mods unganisha huu uziRAIS SAMIA: WANAOANZA BIASHARA HAKUNA KULIPA KODI MWAKA MZIMA.
Na Bwanku M Bwanku.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa kibali cha kuwawezesha Watanzania wote wanaoanza biashara kutolipa kodi kwa kipindi cha mwaka mzima mpaka biashara zao zitakapoanza kukua.
Uamuzi huo wa Rais Samia umetangazwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika wilayani Kondoa.
Dkt. Kijaji amesema adhima ya Serikali ya Rais Samia ni kuwainua Wananchi kiuchumi na kukua kibiashara na ndio maana ameendelea kutoa mikopo isiyo na riba kwenye Halmashauri zote nchini pamoja na kutoa fedha kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) huku akiwataka Watanzania kumuunga mkono Rais Samia kwenye dhima yake ya kumkomboa Mtanzania.