Serikali: Wanaoanza Biashara kutolipa Kodi ya Mapato kwa muda hadi wa mwaka mmoja

Mikopo ya Halmashauri ina umangimeza mwingi. Wahusika wafanyie kazi jambo hilo. Urasimu na kujuana ndiyo mpango mzima.
 
Hii ndiyo inaitwa startup package.

Ingawa nashauri kuwepo na small fees ya 20,000 kwa kila biashara inayosajiliwa TRA
 
Huyu Mama ametumia akili kubwa sana katika hili!
 
Rais Samia Suluhu Hassan ameruhusu wafanyabiashara wanaoanza biashara kutolipa kodi kwa kipindi cha miezi sita hadi mwaka mmoja.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 08,2023 yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Kondoa.

“Rais ametoa kibali, wale wanaoanza biashara kufanya biashara miezi sita hadi mwaka mmoja ndipo waanze kulipa kodi,” amesema.

Amesema hatua hiyo inaonesha jinsi gani Rais Samia Suluhu anavyowajali wananchi na kutoa wito kwa wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa katika kuleta maendeleo.

Aidha, amewataka wananchi kuachana na mikopo umiza kwa kuwa imekuwa ikiwaumiza kutokana na kuwa na riba kubwa.
 
Hiyo nayo ni ahueni kidogo kwenye biashara, Suluhisho la mikopo umiza ni Serikali kubuni namna ya kuwawezesha wananchi wake wa chini na wafanyabiashara mdogondogo kwa mikopo isiyoumiza. Ila kwa kusema tu kila siku Microfinance mpya zitazidi kufunguliwa na kuendelea ku-operate kwenye Long Run.
 
Tusibiri yule kichaa toka canada atapinga tu
 
Tunamsubiri Lema aje na ngonjera zake hapa ;
 
Ni vyema
 
Mashine za EFD nazo zipatikane kwa bei ya chini ya shilingi laki 2. Hiyo itasaidia kila mfanyabiashara kufanya biashara na kutoa receipt.
Kwanza hii biashara ya kuuza mashine za EFD Ina ukakasi. Kwa Nini zisiwe ni Mali za TRA na wafanya biashara wanazichukua kutoka kwako na wanaingiziwa gharama yake katika makadirio Yako ya mwaka na utalipa kidogo kidogo mara nne kama ulipavyo Quarterly Provisions?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…