N
Ndugu yangu ni angalau wao wana demokrasia inayoonekana hata wanawezajivunia mbele ya macho ya dunia sio sisi! Tangu zoezi la kutafta wadhamini lilipoanza matendo na hatua zilizochuliwa na serikali na vikundi vya wahuni ni kielelezo tosha kuwa demokrasia yetu ina shida! Mifano ni kama vile:
1.Kuviba vyombo vya habari midomo visitangaze habari za wapinzani, haya mabo ya kutakiwa kuomba vibali kwanini yaanze leo wakati Tundu Lissu kaanza kufanya mahojiano?? Hivi ni leo ndio tumeanza kusikiliza redio za nje kama BBC, Aljazeera , VoA na nyinginezo?
2.Kuchomwa moto ofisi za CHADEMA mkoani Arusha katika mkesha wa kumpokea Mgombea urais wa CHADEMA, Je kwanini tukio lile lifanywe leo wakati akielekea huko na si siku nyingine zote za nyuma? Je lina lengo la kumpa picha gani yeye na wanachama na wananchi wengine?
3.Kushambuliwa vibaya kwa msafara wa mgombea uraisi wa CHADEMA wilayani Hai na kuharibu hovyo magari yanayotumiwa na chama kwenye shuguli hiyo, Je haya yote yanapangwa na kutekelezwa ili iweje?
4.Hivi leo baada ya kupeleka taarifa mkoani Mbeya kuhusu ujio wa Mgombea urais wa CHADEMA, tayari kumetolewa ruling kwamba kila gari linalojishugulisha na matangazo lazkima lisajiliwe! Je kwanini haya yote yanafanyika baada ya kusikia ujio wa Tundu Lissu je lengo ni lipi?
CCM ilishasema uchaguzi huu ni mwepesi kuliko chaguzi zote zilizopita, sasa mahangaiko yote haya ni ya kazi gani?