who said it?
Kwani hata hicho Kiswahili anakijua? Si unamsikia kila mara na stories zake za utani wa 'kuoa', kuolewa, kuzaa kila apatapo fursa ya kuongea kwenye mikutano ya hadhara?
Pengine hujui kwa nini wenzake tulikuwa tukimuita borer wakati tukiwa UDSM. Mtu asiyejua hata ABC za uchumi, ability to communicate, technological turn around, ataongozaje nchi ikawa na full dynamics kwenye maendeleo?
Mtu asiyejua kuwa katika uchumi wa dunia pesa huzunguka duniani kutoka nchi kwenda nchi nyingine kama tuonavyo hewa na mawingu ya mvua, baridi na joto yakizunguka, atasimamiaje maamuzi sahihi ya kitaalam ya kuongoza uchumi wa nchi?
Mtu asiyekuwa na uwezo wa kutambua kuwa competencies za wananchi ku-mobilise (kuvuta) rasilimali zailizo duniani kuingia nchini mwao ndio chanzo kikuu cha maendeleo katka nchi husika ataongoza nchi iapate maendeleo ya kijamii na kiuchumi?
Sera za Magufuli zinazuia vipaji binafsi vya wananchi ku-acquire competitiness halafu anajidanganya kuwa maendeleo yataletwa na juhudi za serikali peke yake? Nyoo!
Kama Tanzania inataka kupata maendeleo ya haraka, Magufuli hatufai baada ya miaka yake mitano ya majaribio. Ni mwoga kupindukia. Kwa kuwa yeye ni incompetent kwenye broader global engagment hataki kuwa out-smartted. Anaishia kuzui kila fursa za wananchi ambao ni smart na inakuwa hasara kwa nchi. Muulize kwa nini ameagiza BoT wasijihusishe na Cryptocurrency? Kwa nini amedhibiti biashara ya foreign exchange? Kwa nini serikali inaingilia account za wafanyabiashara na NGOs ndani ya benki, tena bila kufuata sheria, maadamu wamechungulia na kuona una pesa nyingi huko? Yeye akili yake ni kutaifisha pesa za watu tu, basi! Unafungulliwa kesi ya kubambika ya utakatishaji pesa, halafu unaletewa mkataba usaini na DPP achukue pesa yako ili wakuanchie. Nonsense Government kabisa!
Kwa nini amekataa Tanzania isipatiwe dola Bilioni moja ili kuamusha uchumi wakati huu wa uchumi wa dunia unaharibiwa na janga la corona? Unajua ameabulia nini?.....dola milioni 14 (tzs. 33B/-!) upo? Ni ujinga mkuu kudhani nchi itafanya biashara ya dunia peke yake au itanufaika na kutajirika kibiashara wakati nchi nyingine dunina kote uchumi wao umelala kutokana na janga la corona. Unajua madhara ya Serikali ya Magufuli imefanya hivyo? Kwa sasa hawana pesa! Na tutarajie serikali kufiliska mara baada ya uchaguzi iwapo utawala wa Magufuli utafanikiwa kuiba kura na kubakia madarakani.
Pengine unaweza kushangaa kuona kuwa wakati Serikali ya Tanzania inahaha kupitia kwa waajiri, kutoza wafanyakzi wa serikali na sekta binafsi kodi ya zuio (5%) kutoka kwenye posho za kujikimu (malazi, chakula na usafiri wa ndani wakati mfanyakazi akiwa nje ya kituo cha kazi) kwa kuwa Serikali haina pesa, katka kipndi hicho hicho, nchi za Kenya, Uganda, Nigeria, Ghana, Ethiopia, Egypt, Morocco, Rwanda, Afrika Kusini na kwingineko zimeingiza nchini mwao zaidi ya dola bilioni moja kwa kila nchi (isipokuwa Rwanda, Uganda na Ethiopia walioingiza dola millioni 750 kila nchi).
Huyu Ndugu anachoweza ni ku-memorize tu, basi. Na hizo (kukariri) ni tabia za walimu wa zamani.