Serikali ya Tanzania ifanye mazungumzo na Marekani ili tuwe jimbo lao. Hiyo ndio dawa

Kama mnawataka wamarekani kwanini mnaipinga DPW?
 
Usichoelewa jimbo la Tanzania ndio litakuwa na maendeleo kuliko jimbo la Texas na hakutakuwa na watu wengi wa jimbo la Tanzania watakaotamani kwenda kuishi majimbo mengine kama New York na DC.
🤣Wewe... mwenyewe umesema utahamia new york
 
Hili ni wazo la ijumaa, kabla sijala biriani wala kwenda kwenye senene za mabibo wine.

Ni hivi suluhisho la kweli la Tanzania kama tunataka kweli maisha bora kwa wote uanze mchakato wa Tanzania kujiunga na United states of America yani total sisi tuwe Wamarekani, na hii proposal Wamarekani hawawezi kukataa ingawa itawagharimu Waafrica wenzetu maana utakuwa ukitaka kuja Tanzania basi uombe viza ya Marekani hukohuko kwenu kwenye US Embassy.

Nitaongelea faida chache tu, kwa wale wanaongaika na viza za Marekani tatizo litakuwa limekwisha maana utakwenda New York kama unakwenda Mbeya tu.

Kwakuwa raslimali alizotupa Mungu tumeshindwa kuzisimamia basi federal government Washington Dc itafanya mabadiriko makubwa na kwakuwa USA ni serikali ya majimbo basi jimbo la Tanzania tutawazidi hata jimbo la Texas.

Kikwazo kikubwa nakiona kwa CCM tu, maana vyama vyote itabidi vifutwe vije Democratic, Republican na vyama vidogo vilivyopo Marekani.

Kwa sababu sioni sababu ya kuwa sovereignty country wakati kila kitu tumeshindwa.

Karibu wadau mwenye wazo la kujazia ajazie hapo kuelekea Tanzania kuwa jimbo la USA.
 
Jimbo la Alaska lilikuwa ni sehemu ya Urusi.

Kisiwa cha Mayote Commoro ni wilaya ya Ufaransa.

Zanzibar ilikuwa ni sehemu ya Oman na ndio yalikuwa makao makuu ya Sultan.

Zanzibar ingebaki chini ya Oman wangekuwa na maendeleo makubwa, wilivyotekwa na Ccm tu ndio imekuwa laana kama sisi tu.
CCM ni zaidi ya laana asee
 
kuna nchi imewahi kufanya hivi tuone kama case study ilikuwaje??
Kisiwa cha Mayotte, watu wake kiasili ni Waafrika, hata lugha yao ni ya kibantu, kipo karibu na Comoro, mara tatu wananchi wake wamepiga kura kuamua kama wanataka wawe nchi huru au sehemu ya Ufaransa, wananchi kwa kuangalia hali za mataifa ya Afrika ilivyo, wakati wote wamepiga kura kuendelea kuwa sehemu ya Ufaransa. Hawataki kabusa kuwa sehemu ya bara au nchi za Afrika.
 
Aaha unataka ya Comoro na Mayotte yajitokeze bongo.
Comoro na Mayotte zilikuwa nchi moja Kama Zanzibar na Pemba ikapigwa kura Mayotte wakaamua kuwa Jimbo la Ufaransa Leo Mayotte wanaenda Parii bila viza Kama raia wa ufaransa na angalau Wana maendeleo.
Labda wauziwe kabisa mkoa mmoja kama case study maana tawala zetu hazitabiriki Huwa ni mbele nyuma.Atakuja jiwe mwingine ataufuta huo mkataba watalamba hasara.
Kwani kigamboni ya Bush iliishia wapii baada ya JK.
 
Hata sisi tupige kura tunatakaje
 
Hili ni wazo la ijumaa, kabla sijala biriani wala kwenda kwenye senene za mabibo wine.

Ni hivi suluhisho la kweli la Tanzania kama tunataka kweli maisha bora kwa wote uanze mchakato wa Tanzania kujiunga na United states of America yani total sisi tuwe Wamarekani, na hii proposal Wamarekani hawawezi kukataa ingawa itawagharimu Waafrica wenzetu maana utakuwa ukitaka kuja Tanzania basi uombe viza ya Marekani hukohuko kwenu kwenye US Embassy.

Nitaongelea faida chache tu, kwa wale wanaongaika na viza za Marekani tatizo litakuwa limekwisha maana utakwenda New York kama unakwenda Mbeya tu.

Kwakuwa raslimali alizotupa Mungu tumeshindwa kuzisimamia basi federal government Washington Dc itafanya mabadiriko makubwa na kwakuwa USA ni serikali ya majimbo basi jimbo la Tanzania tutawazidi hata jimbo la Texas.

Kikwazo kikubwa nakiona kwa CCM tu, maana vyama vyote itabidi vifutwe vije Democratic, Republican na vyama vidogo vilivyopo Marekani.

Kwa sababu sioni sababu ya kuwa sovereignty country wakati kila kitu tumeshindwa.

Karibu wadau mwenye wazo la kujazia ajazie hapo kuelekea Tanzania kuwa jimbo la USA.
Dr mwenzangu umenena, umenena.
 
Zanzibar warudishiwe waarabu wa Oman irudi kwa sultan maana Hawa Wana udugu wa damu hadi kesho hata ukifika Oman kiswahili unaongea tu kama ujui kiarabu
 
Back
Top Bottom