Serikali ya Tanzania yaanza mchakato wa kuunda Satelaiti yake

Serikali ya Tanzania yaanza mchakato wa kuunda Satelaiti yake

Satellite inaweza punguza gharama za mawasiliano ..
Tunaponda serikali kuanza mchakato
Na tunalia gharama za bando...
Satellite inaweza saidia Hali ya hewa..
Tunaponda serikali kutojiandaa na ukame na tunaponda tukisikia imeanza mchakato wa satellite....

Mradi kazi yetu kuponda kila kitu...
Niliwahi kukuheshimu humu jamvini, najuta !

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mmh!!

Kuna habari ukizisoma ama zisikia, inakubidi ugune tu
 
Miniature Satellites (Cubesats) zinarushwa na nchi nyingi za Afrika.

Nadhani ni uwekezaji mzuri hasa kwa wale wanaosomea masomo ya sayansi.

Tunapeleka wataalamu wetu wanajifunza kuziunda, halafu zinarushwa na shirika kama NASA au TSC.

Rwanda, Kenya, Ethiopia na Algeria wamesharusha satellite zao tayari, wakishirikiana na mataifa makubwa kama Japan, Israel na Urusi.

Kuna taarifa inasema vyuo vikuu vingi duniani ndiyo vinaongoza kwa kurusha hizi Satellite ndogo (Miniature Sats/Cubesats) huko anga la nje. Nelson Mandela, MUST, UDSM na COSTECH wawezeshwe tu.
 
Serikali imesema inatambua umuhimu wa nchi kuwa na satelaiti na kwamba katika mwaka huu wa fedha imeanza kuandaa utaratibu wa awali utakaowezesha kuunda na kurusha satelaiti yake angani.

Aidha, imesema ili kuwezesha kufikia azma hiyo tayari imeunda andiko dhana na kuunda timu ya watalaamu watakaoshauri aina ya satelaiti itakayorushwa angani itakayoendana na mahitaji halisi ya nchi.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Mathew Kundo amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Bahi, Kenneth Nollo aliyetaka kujua ni lini Serikali itaanza programu ya kuunda na kurusha setelaiti angani.

“Ni matarajio kuwa timu hiyo itakamilisha kazi ya uchambuzi na kuwasilisha mapendekezo yake Serikalini kwa hatua za kimaamuzi ndani ya mwaka huu wa fedha,” amesema Kundo

Akizungumzia kwa upande wa Afrika, Kundo amesema kuwa hadi sasa Afrika ina jumla ya satelaiti 41, na kuanzia mwaka 2016 ni satelaiti 20 tu ambazo zimekuwa angani, na kati ya hizio 41 ni tisa tu ambazo zimetengenezwa na zina taswira ya Kiafrika.
Eti taswira ya kiafrija[emoji1787][emoji1787]
 
Satellite inaweza punguza gharama za mawasiliano.

Tunaponda serikali kuanza mchakato.

Na tunalia gharama za bando.

Satellite inaweza saidia Hali ya hewa.

Tunaponda serikali kutojiandaa na ukame na tunaponda tukisikia imeanza mchakato wa satellite.

Mradi kazi yetu kuponda kila kitu...
Kuwa na satellite ni jambo moja, kutumia kwa ufanisi ni jingine.
Kama maandalizi ya matumizi sahihi na ufanisi yataainishwa na kuzingatiwa, ni jambo bora sana.
Miradi mingine huanzishwa kwa mihemko kama vile SGR, ambapo inaweza kuja kuendeshwa kwa ruzuku kutoka serikalini.
 
yani priority za nchi hii zinachekesha.. yani tunataka kukimbizana na mambo ya dunia ya kwanza wakati ya dunia ya tatu hatujaya-master

wakati hii ndo ingetakiwa kua priority namba 1, ama umuhimu wa satelite hujui
 
Back
Top Bottom