Serikali ya Tanzania yaanza mchakato wa kuunda Satelaiti yake

Serikali ya Tanzania yaanza mchakato wa kuunda Satelaiti yake

Satellite inaweza punguza gharama za mawasiliano.

Tunaponda serikali kuanza mchakato.

Na tunalia gharama za bando.

Satellite inaweza saidia Hali ya hewa.

Tunaponda serikali kutojiandaa na ukame na tunaponda tukisikia imeanza mchakato wa satellite.

Mradi kazi yetu kuponda kila kitu...

Hakuna ukweli hapo. Tushughulike na mambo ya msingi kwanza tukimaliza ndio tuje kwenye advanced technology. Unaanzaje kuwa na satellite wakati umeme wa shida.
 
Kuwa na satelaiti siyo kukimbizana na dunia ya kwanza,ni muhimu kwa kufuatilia Hali ya hewa,majanga na mawasiliano

Tushughulike kwanza vitu vya muhimu kuliko kujionesha. Nchi umeme wa shida halafu unawaza kutengeneza satellite ambayo ikianguka itavutwa nanmitumbi ziwani.
 
Satellite inaweza punguza gharama za mawasiliano.

Tunaponda serikali kuanza mchakato.

Na tunalia gharama za bando.

Satellite inaweza saidia Hali ya hewa.

Tunaponda serikali kutojiandaa na ukame na tunaponda tukisikia imeanza mchakato wa satellite.

Mradi kazi yetu kuponda kila kitu...
Tangu nilivyoanza ziara nchi za wenzetu ,mfano Dubai Wana majengo hadi mengine hayakaliwi Ili tu kuvutia mji.

Nilichogundua wengi wetu hawana elimu ya mazingira mapya ya kujifunza (exposure),unakuta wanapinga Kila hatua , SGR watasema hamna mizigo,

Bandari bagamoyo sijui mwekezaji kawapiga,

Kualika wawekezaji, watakuhoji wanatokea nchi Gani

Hapo satellite ndo kabisaa!!
 
Tushughulike kwanza vitu vya muhimu kuliko kujionesha. Nchi umeme wa shida halafu unawaza kutengeneza satellite ambayo ikianguka itavutwa nanmitumbi ziwani.
Hali ya hewa,majanga na mawasiliani siyo vya maana!?
 
yataka moyo kuendelea kuwaamini CCM.
 
Kama satellite itapunguza gharama za bando kwa zaidi ya asilimia 50 sawa. Ila kama sivyo siungi mkono hoja.
 
Serikali imesema katika mwaka huu wa fedha imeanza kuandaa utaratibu wa kuunda na kurusha satelaiti yake angani.

Akizungumza bungeni leo, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Mathew Kundo amesema Serikali imeunda andiko dhana na timu ya watalaamu watakaoshauri aina ya satelaiti itakayorushwa angani.

Naibu Waziri Mathew Kundo amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Bahi, Kenneth Nollo aliyetaka kujua ni lini Serikali itaanza programu ya kuunda na kurusha setelaiti angani.

“Ni matarajio kuwa timu hiyo itakamilisha kazi ya uchambuzi na kuwasilisha mapendekezo yake Serikalini kwa hatua za kimaamuzi ndani ya mwaka huu wa fedha,” amesema Kundo.

Naibu waziri amezungumzia satelaiti zilizopo Afrika ambapo amesema hadi sasa Afrika ina jumla ya satelaiti 41, na kuanzia mwaka 2016 ni satelaiti 20 tu ambazo zimekuwa angani.
 
Satellite ya kumnyoosha Kagame maana tumesikia anarusha yake time hii.
 
Au waziri anamaanisha NASA au SpaceX watapewa eneo fulani Tanzania (possibly Serengeti 🙂 ili kurushia setilaiti zao? I mean, kampuni ya US Tanzania, bado ni Bongo itakuwa imerusha, right?

By the way, ile maabara ya kisasa ya Artificial Intelligence (AI), aliyotuahidi Mh. Mollel mwaka 2020 imeishia wapi? Was it just ^hot air,^ ama?
 
Miniature Satellites (Cubesats) zinarushwa na nchi nyingi za Afrika.

Nadhani ni uwekezaji mzuri hasa kwa wale wanaosomea masomo ya sayansi.

Tunapeleka wataalamu wetu wanajifunza kuziunda, halafu zinarushwa na shirika kama NASA au TSC.

Rwanda, Kenya, Ethiopia na Algeria wamesharusha satellite zao tayari, wakishirikiana na mataifa makubwa kama Japan, Israel na Urusi.

Kuna taarifa inasema vyuo vikuu vingi duniani ndiyo vinaongoza kwa kurusha hizi Satellite ndogo (Miniature Sats/Cubesats) huko anga la nje. Nelson Mandela, MUST, UDSM na COSTECH wawezeshwe tu.
Economic benefits? Nadhani tunatakiwa kuwa financial and political independent kwanza. Otherwise, zitakuwa kama historia zisizokuwa na tija.
 
Sisi ni Taifa bandia lisilojielewa, ambalo likisikia tu Taifa fulani wanafanya, basi na sisi ili tuonekane ni Taifa, tunasema tutafanya bila hata kujua ni nini hicho ambacho hilo Taifa linalofanya linatarajia kupata kutoka kwenye jambo hilo.

Kufanya tu uchaguzi wa viongozi tumeshindwa, kuitoa tu ndege kutoka ufukweni mwa ziwa ili kuwaokoa wenzetu waliokwama ndani ya ndege tumeshindwa. Hata kuitoboa tu ndege ili waliomo wapate hewa tumeshindwa, halafu tunaongelea satellite kwa vile tu tumesikia kuna kitu kinaitwa satellite. Hawa watawala wetu hata ukiwauliza satellite nui nini, nina hakika hakuna hata anayeelewa.

Could it be true Trump aliposema kwamba tungepaswa kuendelea kutawalia for the next a hundred years?
 
Kuwa na satellite ni jambo moja, kutumia kwa ufanisi ni jingine.
Kama maandalizi ya matumizi sahihi na ufanisi yataainishwa na kuzingatiwa, ni jambo bora sana.
Miradi mingine huanzishwa kwa mihemko kama vile SGR, ambapo inaweza kuja kuendeshwa kwa ruzuku kutoka serikalini.
Itaanzishwa na serikali, then ikishindwa, utasikia imebinafsishwa like many other government projects.
 
Issue siyo kuunda

Issue Ilikuwa ni kununua

Wajanja wakaleta likampuni lao FEKI

Bei kubwa na mashart kibao

Likapigwa chini
 
Economic benefits? Nadhani tunatakiwa kuwa financial and political independent kwanza. Otherwise, zitakuwa kama historia zisizokuwa na tija.
Economic benefits of Satellites:
A: Enhancement of accuracy, monitoring and forecasting of;
1. Weather
2. Environmental Mapping
3. Human Settlements Patterns
4. Geological Dynamics
5. Ecological and Biological Interactions

NB: Finally, we are able to communicate here, because of a satellite that is placed somewhere in a lower-orbit.
 
Back
Top Bottom