Serikali ya Tanzania Yalifungia Gazeti La The East African

Una chuki na mzalendo wetu watanzania.... Jichambe kimavi hicho kwanza

Mengi ni mzalendo kweli? Wanajikusanya na kuibia wa TZ wenzao kwa kujidai wanaunda kampuni ya NICOL? Siibiwi mimi hata kama ni mchaga mwenzangu? No way!
 
Afadhali wamelifungia,hili gazeti nilikua silielewi kabisa.lilikua linaila kisogo Tanzania kwa kuzitumikia nchi za EAC zinazopingana na sera za TZ halafu bila ya woga kabisa.hapa TZ kwanza,wengine baadae.hatuwezi kuishi na nyoka ndani.
 

Asante kwa taarifa
 

Hiki kituko kimenifikirisha sana na kurejea jinsi gani Mwl. Nyerere alitumia Wizara ya Habari.Maelezo na Taasisi kama Shihata,RTD kujibu mapigo pale Serikali ya wakati huo ikiona imeshambuliwa.

Leo hii utadhani Tanzania haina Information minister,wala Msemaji wa Serikali!! Jibuni mapigo kwa busara badala ya jazba za kijinga kama hizi. Nimekuwa naandika kwa kusema kwamba Rais ajaye sifa kubwa itakuwa kupambana na rushwa,uzembe serikalini,kujenga uchumi,kuliunganisha taifa tena na kujenga upya mahusiano na majirani zetu!
 
At last, Mungu amejibu maombi. Gazeti la The East Africa limekuwa mstari wa mbele kuichafua Tanzania kwa kipindi kirefu sana na hata columnist/Opinions column imekuwa biased sana na almost kuikandia Tanzania. Personally, nimewahi kukwaruzana na waandishi wa gazeti hili kwa kuandika Tanzania kwa mabaya tu. Kuna watu humu, wana-comment wasichojua, hili gazeti limekuwa na chuki kubwa kwa Tanzania kwa muda mrefu, na serikali ilikuwa inawavumilia tu. I wish lisirudi kabisa kwenye circulation in TZ, Once again, Thanx govt. Mungu ibariki Tanzania
 
=Kikwete hataki kukosolewa. Anataka sifa tu, basi. Salva Rweyemamu, Muhingo Rweyemamu, Premi Kibanga nk wengine waliifanya kazi hiyo ya kumpamba leo wanaula. Wameuza utu wao kabisa. Sasa hivi si waandishi tena, ni mbwa wa Kikwete. The East African na ----------- mafichua siri, yamefungiwa. Udikteta wa Kikwete. Rais ajaye ayafungulie magazeti hayo. Kikwete hafai uongozi, ni mhuni tu mmoja kama alivyo mwita Prof. Lipumba...!
 
Mkunali mkatae, sio kila kitu kushabikia tu bila kufanya tafiti. Naungana na Serikali kwa kulifungia hili gazeti. Kwa muda mrefu sama halina positive informatoon kwa Tanzania. Wameendelea kuichafua nchi kwa ajili ya manufaa ya Kenya na Rwanda. Hatulitaki kwa sasa lipumzike tu huko huko.
 
Mungu wetu ni mwema sana hili gazeti limefanya kazi ya uchochezi na kuzalilisha mda mrefu sana taifa letu sasa wamepata walichokuwa wanakitafuta safi kabisa manina zao.
 



tatizo ni kuwa na viongozi vilaza na wananchi vilaza. leo wanashangilia kufungiwa hilo gazeti pasipokujua linaweza kupatikana kama mmiliki akiamua. kwani anaweza kuomba kibali kwenye nchi zingine na akahamisha mitambo yake na magazeti yakawa yanaletwa kama bidhaa zingine. lazima tuwe na ufikiri nje ya box miaka 20 gazeti halijasajiliwa, rita wako wapi?tra wako wapi? wizara ya habari iko wapi? kabla ya kulifungia taasisi zote hizo zilitakiwa kushughulikiwa
 
lazima tuwe na ufikiri nje ya box miaka 20 gazeti halijasajiliwa, rita wako wapi?tra wako wapi? wizara ya habari iko wapi? kabla ya kulifungia taasisi zote hizo zilitakiwa kushughulikiwa

Siyo zinatakiwa kushughulikiwa bali zote pamoja zinatakiwa zilishughulikie hilo gazeti kwa kufanya biashara bila kusajiliwa kwa miaka 20 ili liwe fundisho kwa magazeti mengine yanayoendesha biashara bila kusajiliwa.
 
Siyo zinatakiwa kushughulikiwa bali zote pamoja zinatakiwa zilishughulikie hilo gazeti kwa kufanya biashara bila kusajiliwa kwa miaka 20 ili liwe fundisho kwa magazeti mengine yanayoendesha biashara bila kusajiliwa.

Miaka 20 serikali haijui NMG inafanya biashara bila kusajiliwa? Si huu ndio uzembe katuni unagusia. Incompetence uliopitiliza.
 
Reactions: 999
Ukifungia gazeti miaka hii hakikisha unafungia na website. Ama sivyo unatwanga maji.
 

Nani ameviondoa vyote hivyo!? Bila kupepesa macho na bila kuogopa kupelekwa mabwepande inabidi Chama Cha Mapinduzi wafungashe virago waondoke tujaribu na wengine! CCM walituaminisha kuwa mkichagua wapinzani wataleta vita, ushoga n.k, kumbe ilikuwa ni hila! Nyuma ya pazia ni wao ndio wanaleta vita tena kwa speed! Wameteka Media karibu zote na ma-presenters wao maslahi kwa fedha haramu za Escrow,Ivory ili kuwapromote waendelee kuitafuna nchi bila bugudha!!!
 
Miaka 20 serikali haijui NMG inafanya biashara bila kusajiliwa? Si huu ndio uzembe katuni unagusia. Incompetence uliopitiliza.

Hakuna marefu yasiyo na ncha.Na hakuna incompetence isiyo na mwisho.Cha msingi tunafurahi kuwa incompetence imefikia mwisho wake na hatimaye waliokuwa incompetent wameweza kulidaka the EAST AFRICAN newspaper.Hata kichaa huwa hawi kichaa milele kuna siku hubahatisha akapata mganga mzuri akapona.

Tunashukuru wamegundua halijasajiliwa na wamewafungia.
 
Miaka 20 serikali haijui NMG inafanya biashara bila kusajiliwa? Si huu ndio uzembe katuni unagusia. Incompetence uliopitiliza.

Mimi kama Mtanzania na Mwananchi wa kawaida kabisa, naumia ninapoletewa taarifa na picha kuwa Rais wetu kaenda Brazil kukutana na kocha wa timu ya mpira wa miguu aje kuifundisha club anayoishabikia yeye! Ninaumia ninapoletewa habari na picha kuwa Rais wangu anakokotwa kwenye gari la kifahari na farasi alipoenda Jamaica Rais wangu kaenda Botswana kujifunza kilimo cha mananasi!?!?!? Waziri wa kilimo na maafisa kilimo wako wapi!? Kwanini wasipelekwe wao!?, ni kwanini bac asiwatume wawakilishi wake badala ya kwenda yeye anaonekana ni kama vile anakwenda kutalii na kuzurura mwaka mzima anashinda angani kwa kwenda nchi mbalimbali! Tumekuwa kama yatima nchi inaendeshwa na wenye viburi, ubinafsi na ufedhuli! Ni lini bac tutachoka kusikia mambo haya!?
 
Ukifungia gazeti miaka hii hakikisha unafungia na website. Ama sivyo unatwanga maji.

Unachosema si kweli
Gazeti liko kibiashara, website ni ya bure.Ukifungia gazeti maana yake pesa za mauzo haziingii tena.Mishahara na marupurupu ya wafanyakazi yanakuwa mgogoro.Faida kwa wanahisa zinaingia matatani.Hisa zinashuka bei.Na yaweza sababisha gazeti kufilisika.

Hatua ya kulifungia gazeti ni hasara kubwa kwa gazeti kuliko kufunga website.
 
Nilishangazwa na kufungiwa kwa gazeti la the East African nchini Tanzania..huu ni ufisadi na kutowajibika kwa serikali ya CCM. Sababu ni kuchapisha vibonzo vinavyoelezea JK katika hali ya kuikuza na kusherehekea ufisadi, uzembe n.k Katika serikali yake huku nchi ikiangamia kwa umaskini, miundombinu na hospitali kukosa madawa.

Gazeti hili lilifungiwa maramoja kwa kielelezo kuwa linamshusha hadi rais JK lakini ukweli ni kuwa JK ameliona kuchochea wananchi na kuwafumbua macho juu ya uongozi wake mbovu. Mambo haya ya viongozi kutisha na kufunga vyombo vya habari si geni E.A ikiwemo siku Museveni kuwahi kulifunga gazeti la the Monitor na kujeruhi wafanyakazi wake kutumia askari wake kwa kuwa walifichua siri ya uongozi wake wa kiimla.

Uongozi wa CCM si wakushabikiwa kamwe lakini wapo watanzania wanaoipa pongezi CCM kwa kulifungia gazeti bila kujua mwenzako akinyolewa chako kitie maji.

The citizen pia gazeti la Kenya linapaniwa kufungwa na CCM. Mtizamo wangu ni magazeti haya yaisifu serikali ya CCM kwa mabaya na mazuri wanayofanya.wajue kuwa nchi si ya mtanzania ni ya CCM na lolote watakalofanya ni wamsifu mfalme Jakaya Kikwete ili biashara yao ipate kudumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…