Serikali yaeleza kusikitishwa na uamuzi wa Denmark kufunga ubalozi wake

Serikali yaeleza kusikitishwa na uamuzi wa Denmark kufunga ubalozi wake

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imeeleza kusikitishwa na hatua ya Serikali ya Denmark kuamua kufunga shughuli za Ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo mwaka 2024.

Denmark jana ilitangaza uamuzi huo ambao ulihusishwa na mkakati wao mpya wa masuala ya mambo ya nje. Mbali na Tanzania pia nchi hiyo itafunga ubalozi wake nchini Argentina, Ubalozi mdogo wa Chongqing nchini China na ujumbe wa biashara huko Barcelona (Uhispania).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula leo Jumamosi Agosti 28, 2021 amesema hatua hiyo ya Denmark inasikitisha ikizingatiwa kuwa hivi karibuni Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa ikifanya jitihada za kufufua na kuimarisha diplomasia na uhusiano wa nchi rafiki ikiwemo Denmark.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo imeeleza kulikuwa na jitihada za kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini pamoja na kuimarisha demokrasia na utawala wa sheria.

Aidha taarifa hiyo inaeleza Balozi Mulamula jana alifanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark, Flemming Mortensen ambapo walikubaliana kuendelea kushirikiana na Mortensen anatarajia kuzulu nchini siku zijazo.
 
Sijajua uamuzi wa Hawa wadenmark unaiathiri vipi Tanzania maana ni uamzi wao binafsi na vipaombele vyao kama walivyoeleza.
Mzunguko wa foreign currency utapungua,Baadhi ya watu watakuwa unemployed automatically,Baadhi ya miradi waliyokuwa wanafadhili inaweza kukwama na kufa,Connection ya wawekezaji kutoka Nordic itapungua and etc.Denmark's development assistance kwa Tanzania si chini ya 5 Trillions.
 
Serikali nafikiri imeweka pamba masikioni, haisikii la muadhini wala muumini.
Wananchi wanalia na sakata la Mbowe, kitu ambaco hata wana CCM tunaona ni filamu ya kuigiza.
Kama kuna ugaidi wa Mbowe serikali ingechukua hatua muafaka zaidi kuliko kuji expose negatively ili kuwafurahisha watu wa Mwendazake.

Serikali ilibidi kuona the writting on the wall baada ya mabalozi kuhudhuria kesi ya Mbowe pale Kisutu.
Badala ya kuchukua hatua mahsusi, Waziri wa Mambo ya nje anawaonya!!
Public rebuke kwa mtu anaye kufadhili kistaarabu kwa miaka mingi!

Hicho tunaita kiburi cha kijinga!

Sasa wanaanza kuondoka na kuhamisha balozi zao toka nchini!
Balozi Liberata Mulamula is this a POSITIVE OR NEGATIVE achievement under your tenure?
Frankly, what did we expect?
Wananchi gani hao? Kama wazungu Wana maslahi na akina Mbowe waweza endelea nao
 
Mzunguko wa foreign currency utapungua,Baadhi ya watu watakuwa unemployed automatically,Baadhi ya miradi waliyokuwa wanafadhili inaweza kukwama na kufa,Connection ya wawekezaji kutoka Nordic itapungua and etc.Denmark's development assistance kwa Tanzania si chini ya 5 Trillions.
Acha utoto,effects yake ni insignificance.Pesa za kigeni na kufungwa ubalozi wapi na wapi? Rwanda alifukuza balozi wa Us na France hadi kufungasha huo ujinga unaoongea ulitokea?

Vikwazo vya uchumi na biashara tuu ndio vinaweza leta shida tofauti na hapo wanajifurahisha.
 
Mulamula [emoji1787][emoji1787]mama wa kufungua nchi
 
Mh Rais Samia Suluhu Hassan, huyu Mama kaona mbali sana kila hotuba anawaasa vyombo vya ulinzi na usalama kutenda haki kwa raia wake. Demokrasia hakuna, ubambikizaji kesi ndiyo umeshamiri na hili linakera Sana mataifa ya nje. Tusibaki kusikitika tu chukua hatua acha uonevu kwa raia wako.
Haki gani zinazokandamizwa? Magu alikandamiza watu na mambo yalienda sembuse awamu ya Mama? Acheni utoto nyie.
 
Acha utoto,effects yake ni insignificance.Pesa za kigeni na kufungwa ubalozi wapi na wapi? Rwanda alifukuza balozi wa Us na France hadi kufungasha huo ujinga unaoongea ulitokea?

Vikwazo vya uchumi na biashara tuu ndio vinaweza leta shida tofauti na hapo wanajifurahisha.
Wewe jamaa ni hopeless sana-Full ujuaji na ubinafsi.Meko ndo maana alikuwa anawakomesha hopeless na wabinafsi kama nyie.Kisa MEKO kuibana construction sector na kuzuia upigaji mliokuwa unafanya ndo kulikufanya umchukie??? Sasa hv unabwabwaja tu kwa sababu fursa za upigaji wa kijinga kwenye construction zimerudi-Huu ubinafsi wa kishamba utaisha lini Tanzania 😕😕 Elli M denooJ Jidu La Mabambasi
 
Haki gani zinazokandamizwa? Magu alikandamiza watu na mambo yalienda sembuse awamu ya Mama? Acheni utoto nyie.
Wewe si ndo ulikuwa unapiga kelele kila kukicha huku mitandaoni kumhusu meko,Huna hiyo moral authority ya kuwapangia watu nini cha kuwaza
 
Niambie nchi top ten duniani ambazo hazijawahi kuwa na uvunjwaji wa haki za binadamu
Wewe ni sawa na anayesema niambie mtu ambaye hajawahi kutenda dhambi, sasa sijui kama unataka kuniambia kwamba hawa mapolisi wanaokamata wahalifu au mahakimu/majaji wanaohukumu watu wenyewe hawana dhambi au hawatendi makosa....!!!
 
Wewe jamaa ni hopeless sana-Full ujuaji na ubinafsi.Meko ndo maana alikuwa anawakomesha hopeless na wabinafsi kama nyie.Kisa MEKO kuibana construction sector na kuzuia upigaji mliokuwa unafanya ndo kulikufanya umchukie??? Sasa hv unabwabwaja tu kwa sababu fursa za upigaji wa kijinga kwenye construction zimerudi-Huu ubinafsi wa kishamba utaisha lini Tanzania 😕😕
Haya unayoandika ni stress au? Yanahusikaje na mada ya ubalozi? Utakufa kwa stress nakwambia.

Huyo meko wako alikuwa kiazi Sana na nilianza kumdis kitambo hata hajawa Rais,enzi hizo wewe unafutwa makamasi na mama yako kima wewe.

Unaropoka hata hujielewi unachoongea,kama kuna upigaji na wewe kapige kwani hutaki pesa?
 
Wewe si ndo ulikuwa unapiga kelele kila kukicha huku mitandaoni kumhusu meko,Huna hiyo moral authority ya kuwapangia watu nini cha kuwaza
Sijawahi muacha salama meko,hapo natolea mfano kama meko na ukatili wake wote mambo yalienda sembuse mama? Ndio nawauliza haki gani hizo ambazo Maza anakandamiza kumzidi Meko?
 
Tumfungulie Mbowe, madai ya katiba yaendelee
Huwezi kua karibu na watu wanafinyanga democrasia kumbukeni Denmark nao wanamfumo wavyama vingi

Toka 1963 Ccm bado hamuelewi maswala
Jamani
 
Haya unayoandika ni stress au? Yanahusikaje na mada ya ubalozi? Utakufa kwa stress nakwambia.

Huyo meko wako alikuwa kiazi Sana na nilianza kumdis kitambo hata hajawa Rais,enzi hizo wewe unafutwa makamasi na mama yako kima wewe.

Unaropoka hata hujielewi unachoongea,kama kuna upigaji na wewe kapige kwani hutaki pesa?
Kwa asiyekuelewa wewe ni msaka tonge tu anayeongozwa na maslahi binafsi na ubinafsi-Mirija imerudi unaanza kupangia wengine nini cha kuwaza humu mitandaoni? 😳 😳 😳
 
#PICHA:Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Liberata Mulamula akiongea kwa njia ya mtandao na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Flemming Moller Mortensen kuhusu uamuzi wa nchi hiyo kufunga shughuli za Ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo mwaka 2024. https://t.co/t7WNhUMxlZ
 
Sijawahi muacha salama meko,hapo natolea mfano kama meko na ukatili wake wote mambo yalienda sembuse mama? Ndio nawauliza haki gani hizo ambazo Maza anakandamiza kumzidi Meko?
MEKO alikuwa anavamia watu makanisani ? Sheria inaruhusu serikali kupitia polisi kuingilia uhuru wa kuabudu? Matendo ya MEKO ya kuweka watu mahabusu kinyume cha sheria yamebadilika? Kujibu wananchi kwa dharau kumebadilika? manake watu wakihoji tozo wanaambiwa waende burundi,Mambo ya kuitwa siyo Raia yameisha?manake watu wanafungua kesi kupinga tozo wanaambiwa siyo Raia halali wa Tanzania
 
Back
Top Bottom