Serikali yakiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudi tena

Mimi huwa nawashangaa wanaoenda kisiwa cha saa nane,maana kuna pimbi tu na vi swala vya kuhesabu.bora hata zamani kulikuwa kuna cage wanafuga wanyama mfano simba, sokwe, chui, fisi hii iliwavutia watu wengi kulipia na kwenda kuwaona mi naomba warudishe huo utaratibu.

lakini vile vile wanaweza kuongeza na mabwawa ya kufuga mamba itakuwa ni kivutio tosha maana kuna wakazi wengi wa mwanza japo wamezungukwa na ziwa ila hawajui mamba anafanana vipi.
 
Kwa maoni ya wadau hapa, inaonyesha kodi kubwa ndio changamoto kubwa.

Ninachojiuliza ni kuwa mbona suala la kodi bongo ni kaa la moto?

Kwenye biashara kodi kubwa, viwandani kodi kubwa, kwenye kilimo tozo kibao, kuagiza bidhaa nje e.g. magari ndio balaa kabisa. Kumbe kwenye utalii nako hali nin gumu pia?

Ilitakiwa tuwe mbali sana kiuchumi kwa kodi hizi.
 
Sekta ya utalii nikama imekuf inajiendea tu bora liende.Changamoto zake ni nyingi sana na hakuna mwenye ujasiri wakuziweka wazi nakuzifanyia kazi.ndo maana kuanzia wazir hadi watendaji ndani ya wizara ni porojo tu siku ziende.

Sasa kama kuna waziri kateuliwa juzi yeye badala yakukaa na wadau wahiyo sekta kujadiki changamoto zilizopo ili apush kuleta tija na ufanisi yeye anaongelea watumishi kukariri ilani ya chama wakati wizara ina mambo chungu mzima yakuyajadili.

Kwahiyo sidhani kama tuko serious na hii sekta.Kwahiyo hao watalii kutokurudi sio kosa lao ni letu.Sasa hivi watendaji wamejificha kwenye kichaka cha corona.
 
Labda waongeze vivutio vingine vya mapumziko; kwa sasa asilimia kubwa ya tourism destination zetu ni ‘special interest tourism’ usually it has a niche market. Udhani kila mwaka familia itakuja kutembelea simba at the minimum cost of $5000 per head au kupanda mlima Kilimanajaro kila baada ya miaka mitatu.

Ni aina ya utalii ambao ukishamuona fisi anavyowinda mara moja inatosha ukizingatia bei zenyewe. Wajiongeze ili watu warudi inabidi wapewe sababu zingine. Mtu kabla ajaondoka labda anapitishwa Arusha au Kilimanajaro anapata sababu zingine za kurudi.

Sitoshangaa kusikia asilimia kubwa ya watalii wanaorudi ni wale waliotembelea Zanzibar kufuata beach resorts ambazo kwa sasa wanajaribu kutengeneza mazingira to rival anywhere in the world.
 
Napendekeza

1. Sisi Watanzania Tujifunze na Tuwe Vivutio.
2. Sisi Tukivutia kwanza na Vivutio vingine vitavutia zaidi wavutiwaji.
3. Taifa Zima kila mtu avutie kwa upekee wa eneo husika.

Mfano Ukija Arusha watu Wote tuvae na Tuwe na muonekano wa Kimasai, Kibarghaidu, Kihadzabe n.k. Tusivae Kama wavutiwaji maana sasa hakutakuwa na tofauti.

Nyumba Tujenge za Kisasa katika muonekano wa Kiasili.

Ni kutengenezwa upya kwa Utaifa na Utalii Policy Mpya.
 
ili kuvutia watalii wa kigeni zaidi, nadhani tozo za kuingia hifadhi ingepunguzwa ili wengi wao waweze kumudu na kuongeza mapato ya nchi.
Hili limekuwa tatizo kubwa. Kuna hifadhi moja kubwa. Wageni wanakuja pesa kiasi fulan ila wanaishia getini na malalamiko kibao.

Embu tujaribu kushusha tozo ziko juu sana sana sana
 
Inasikitisha kiwango cha inefficiency katika nchi hii. Halafu wahusika wala hawajali.

Mimi kuna biashara hata hapa Dar tu niliamua sirudi tena kwao. Pesa yangu nataka niitumie sehemu nitakayoheshimiwa kama mteja, bila kutapeliwa au kuchukuliwa poa. Na hili ndiyo ninaloliona kwenye suala hili.

Hakuna anayejali.
 
Hapo sijaongelea mminyo wa online content creators wa Kitanzania.

Wahusika hata hawakujiuliza utaathiri vipi idadi ya content nzuri zilizokuwa zinatengenezwa na Watanzania za kuitangaza vyema Tanzania.

Kiufupi tatizo ni gharama kuwa juu sana, customer care mbovu, hatujaongeza thamani na creativity ya kutosha katika vivutio vyetu na pia marketing effort bado iko chini sana.
 
Napendekeza

1. Sisi Watanzania Tujifunze na Tuwe Vivutio.
2. Sisi Tukivutia kwanza na Vivutio vingine vitavutia zaidi wavutiwaji....
That thing haita work 100%. Eti wote wavae rubega? Nani kasema inavutia watalii?

Mgeni anapotaka kuja tz asianze kulalamika bei.. apate hile customer care top notch.
Bei iwe rafiki. Mfano wageni wanaopanda mt.klm wanalalamika tozo ni kubwa sana. Halaf service wanazopata ndani si zenye value hizo.

Ndio kusema kwamba wachaga hawakai kitalii.. nope? Service.. na gharama ziangaliwe upya.

Kipindi hiki cha corona..wenzetu uchumi wao ume shake. Tungepunguza tozo tuweze kuwa accomodate. Kama wanavyofanya maiafa mengine.
 
Hii topic ingefundishwa darasani ,tunaita repetitive purchase ina maana kuna shida kwenye service quality au overall customer satisfaction

Walimu wa marketing Udbs wamejaa wangeenda wakafundisha how to bridge 4 gaps za service quality ambazo ni Tatizo ku retain customers -defensive marketing ,otherwise ku attract a new customer (tourists) costs 5 times than keeping existing customer.

So topic italenga ku attract new customers (acquisition strategies e.g marketing communication tools e.g advertising and other promo mix) then ku defend existing customers' retention strategies kama relationship marketing ,service failure recoveries ,marketing research etc
 

1. most places ukishaenda mara moja ukirudi mara mbili inakua sio adventure tena, hata kama ni dubai ukishaenda mara moja ukienda the second time it doesnt add up

2.ebu fanya comparison na sehem zingine za utalii utajua tanzania bei ni che sana, mfano kupanda tu mlima everest andaa mil 300 tanzania ni $1000 sasa nan ana nafuu apo
 
Hii topic ingefundishwa darasani ,tunaita repetitive purchase ina maana kuna shida kwenye service quality au overall customer satisfaction...
Nimeipenda idea yako. Wakatoa seminar. Au hov iwape access waje na model itakayo changia kuongezeka kwa watalii
 
ili kuvutia watalii wa kigeni zaidi, nadhani tozo za kuingia hifadhi ingepunguzwa ili wengi wao waweze kumudu na kuongeza mapato ya nchi.
Alitarajia kukuta kipusa akakuta kipussy......hahahahaha
 
Huyo katibu mkuu siyo mzalendo kwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…