Serikali yakiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudi tena

Serikali yakiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudi tena

Kuna watu mnaleta siasa kila sehemu.

Yaani ni kama mmeamua kwenda kinyume tu na wale wanaoabudu na kusifu.

Hivi kwa akili za kawaida kabisa unakuja kupanda kilimanjaro 2021,utarudi tena kupanda mlima lini?

Mwingine analalamikia gharama,sijui anadhani mzungu ni sawa na mchaga wa uru anayerudi kuhesabiwa dec kwao moshi!!!wale wanajiandaa miaka hata 7 au 19 kabisa kwa ajiri ya kutengeneza kumbu kumbu maishani mwake.

kama kandaa sehemu 5 atembee duniania baada ya kujipanga,anarudije tz!!!
 
Mkuu, swala siyo gharama tu, swala ni thamani ya gharama anazolipa. Ukiacha vivutio kama hifadhi za Serengeti, Ngorongoro, Gombe na Mlima Kilimanjaro, au visiwa vya Zanzibar, Mafia, nk...vivutio vingine huduma zake ni za chini sana...
yes na lengo lisiwe kurudisha watalii waliokwishakuja.

bali kuongeza wengine zaidi.
 
Kwani kuna vitu gani ambavyo vitasababisha arudi,, inawezekana huduma zenu ni mbovu
 
Asante kwa mrejeshonyuma....
Hakuna kitu kama kutoa SARVICE nzuri kwa mteja wako ,ukae shimoni mteja atakufuata huko huko ukiwa na sarvice nzuri ,lkn ikiwa mambo yenyewe ya kiswahili swahili hakuna mtalii wa ndani wala nje atakae kuja mara ya pili ktk matangazo yaho unaandika mambo mingi ya kumvutia lkn akifika haoni hata moja .Kwa kweli kuna mambo mengi ya kuzingatia .
 
Hakuna kitu kama kutoa SARVICE nzuri kwa mteja wako ,ukae shimoni mteja atakufuata huko huko ukiwa na sarvice nzuri ,lkn ikiwa mambo yenyewe ya kiswahili swahili hakuna mtalii wa ndani wala nje atakae kuja mara ya pili ktk matangazo yaho unaandika mambo mingi ya kumvutia lkn akifika haoni hata moja .Kwa kweli kuna mambo mengi ya kuzingatia .
Hilo ni tatizo.

Au wanakopwa mshahara hivyo hawana motisha?

Au hawana mafunzo ya kutosha ya ukarimu kwa wateja-watalii?

Au hawana "exposure" juu ya taaluma yao?

Maswali ni mengi, bado ninashangaa...
 
Huyu katibu mkuu anajitaka kweli?Utawala huu ukisema ukweli wewe ni kibaraka wa mabeberu,Wanapenda mambo mengi ya hovyo yawe siri.

Juzi nilikua na dr mfawidhi wa hospitali fulani akaniambia budget ya dawa kwa hospital hailetwi wanaambiwa watumie zile tozo ndogondogo wanazowatoza wagonjwa kujiendesha pesa ambazo hazitoshi.Lakini wakipata ugeni wakisiasa kama waziri kwenye kuhutubia wananchi unatakiwa usifie kwamba hakuna tatizo la dawa,ukijichanganya imekula kwako.Tunaambiwa budget ya wizara imeongezwa wakati ni figure tu hakuna kitu.

Wakati watu wanalalamika kodi tz imekuwa ni kaa la moto tayari kuna kodi mpya kwa watilili inaitwa kodi yakitanda.

Yani utawala wa awamu ya tano umekuwa kero sana kila siku mambo mapya kiasi ambacho huwezi jua kesho watakuja na lipi.

Punguzeni hizi kodi ili mshawishi wageni waje wengi
 
Culture tulishaua sasa hivi tunajifanya ni waarabu kwa mavazi, tabia lugha na hata vyakula. Tunajifanya wazungu kwa mavazi,chakula, tabia na hata lugha ni kitu gani mtalii atapenda kujifunza kwetu?
 
hivi hawa watu wanafikiriaje? wakifanya dola 100 hapa kupanda mlima tutapata malaki na malaki ya watalii kwa mwaka hivyo bei kubwa sio kupata sana tuangalie na wingi wa watu pia
Kuna kitu kwenye service provission "queing models" /"Queing Management Sysytems" ... Sijui watendaji wetu hawajavisomea 'na naamini hiyo wizara husika wachumi, mipango, wathamini 'na wote wesoma hicho ...tunafeli wapi sijui
 
Punguza Kodi Ili ukusanye kidogo lakini kingi. Sio unakamua damu yote
 
Kuna siku mtalii kalipa dola 250 eti nauli ya tax toka airport hadi hotelini mjini huu ni wizi hata Kama ana hela kuzidi bilgate huwezi ukamchaji mtu teksi kwa laki 570000
 
Tuendelee kutangaza vivutio vya utalii na kuboresha huduma. Shout out to Bongozozo na Ndumbaro kwa kumleta Drew Binsky
 
Labda tuangalie mtalii kabla yakuamua kuitembelea Nchi fulani hua ana angalia mambo gani hasa? je katika hayo mambo ambayo mtalii hujiridhisha kabla ya kuamua kufunga safari sisi tupo sawa katika mambo hayo?
 

mfano huu unaweza kutusaidia kujua tatizo la utalii wetu liko wapi na namana ya kulitatua​

Friendly vs. Hospitable​

KES
80s hospitality
A lot of people claim to have friendly churches. But we have to ask, “Friendly…compared to what?”
Most would avoid saying, “our church is unfriendly.”
Yet, friendliness is distinctly different from hospitality.
• A friendly church might–by policy or administration–greet newcomers
• A friendly church may staff a church information center
• A friendly church might include a greeting time within the order of the worship.
But, this is surface-level hospitality.
Friendliness involves a, “Hello, how are you?” But, hospitality waits for the real answer, and offers an invitation to break bread together… Really, to do life together.
• After church, are folks staying afterwards to visit, or do they rush off to their kids’ soccer matches, NFL games, or other obligations?
• Are spiritual siblings, sort of, shooed out so the Sexton can lock up the building?
• Can congregants make and share a meal at church, a snack, or put on a pot of coffee, without the deacons getting nervous about clean up and carpet stains?
• Does the building, and the programs and schedules therein eclipse the human beings for whom the church exists?
Shouldn’t church feel (be) comfortable–like an inviting hearth and home? Should it not have the kitchen and the living room vibe, where people feel a bit saddened to leave, at the end, because they have enjoyed a time with people who love them. A place where people don’t look at their watch, but instead comment on the pity it is that time went so quickly. A. hospitable. place.
What is the culture of your church?
If you could change something, what would it be?
What does hospitality
look and behave like, [to you]?
Thanks for your ideas.
 
Urudi Tanzania kufanya Nini? Kwingine duniani nchi zinapunguza Kodi kubusti utalii, hapa kwetu tunaongeza Kodi kwa watalii kila uchao. Tayari Kuna jini jipya linaitwa bed levy linasubiri wageni wamiminike kwa wingi
Kuna hatari ya kuanzishwa na Oxygen levy maana watafiti wazalendo wamegundua oxygen ya Tanzania ni nzuri kuliko duniani kote hivyo ipo haja ya kuwekewa kodi kwa watalii maana ni chanzo cha mapato. Jamani sijatimiza vigezo vya uteuzi kwa awamu hii kweli?
 
Sijui ndo uzalendo ama Ni Nini lakini kiukweli sisi tunaona Tanzania Kama nchi ya kipekee Sana duniani kitu ambacho sio kweli, Wala si kweli kuwa Tanzania ni nchi pekee ya kuvutia watalii duniani. Kuna nchi nyingi duniani Zina vivutio vya kutosha hasa wanyama wa mwitu. Hapa Afrika tu Kuna nchi Kama Botswana, Namibia na south Afrika Zina wanyama wengi na vivutio vingi hata nje ya wanyama...
Utamaduni na usafi ni jambo muhimu, mindset zetu kuhusu mazingira ya usafi kwa kweli. Nikitolea mfano Zanzaibar sidhani kama wangewekeza katika vitu muhimu kama public toilets nzuri za uhakika, mji uwe safi ukarabati wa majumba ya kale, kujengwe hostels za bei nafuu kusudi wale watalii wa kundi lanaitwa backpackers huwa wanapenda kufikia.

Yaani tufanye utafiti tulenge kila kundi la watalii. Kundi la back packers wale ambao huwa wanatembea na mabegi yao ni aina ya watalii ambao huwa ndio wengi kweli, huwa wanatembea ma nchi tofauti na kulala katika maeneo design mfano hostels za bei nafuu special kwa wageni na huwa wana design safari zao katika affordable budget mfano yule drew binzky aliyekuja hapa Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo land cruiser ili ziingie zitengenezwe kwa ajili ya kubeba watalii Kodi yake ipo juu tunabaki kuwa na gari chakavu kwa wageni wanaolipa Kodi kubwa...punguzeni Kodi kwa vifaa vinavyohusiana na utalii ili kuweka mazingira mazuri ya kupata wageni wengi mimi ninapata wageni wanaoenda table mountain nikiwashawishi baadhi wanakuja Tanzania mwaka unaofatia wanarudi Cape hawataki kusikia kuhusu Tanzania tena maana Cape gharama za kawaida mno au hapo Botswana gharama zao zinaeleweka sio kama sisi na tunasahau kuwa wanyama wapo na wataendelea kuwepo tuu ni sisi kuweka mazingira rafiki kwa wageni...
Mimi nafikiri tungetoa unafuu kwa vifaa hivi ili kusudi wajasiriamali wengi wajitokeze wanunue yale macamping equipment. Magari ili utalii wa ndani ukue

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa hakuna kupepesa macho customercare ni sifuri kwa viongozi wa serikali na watumishi wa serikali walio wengi wametanguliza usanii katika utekelezaji wa majukumu yao.

Fikiria kiongozi anampokea mtalii aliye kiongozi-star ana kimbilia kupiga nae mipicha tuu hamuulizi angependelea nini akione ili baadae abaki na kumbukumbu.

Haya mtalii anaondoka hadi anafikabkwake hata haulizwi kama amefurahishwa na nini na hajafurahishwa na nini ili waboreshe hata kumpigia simu tu kumkumbuka na kumuomba aje tena na watalii wengine au kwa sasa wameboresha hiki na kile ,hawawezi.

Fikiria hapa hapahapa nchini kiongozi anatoa namba yake ya simu kwa wananchi na kuwaambia wampe malalamiko yao,wananchi wanampa na inaonesha kwenye simu amepokea lakini kiongozi huyo hawezi hata kujibu kama amepata malalamiko hayo na atayashughulikia ila unaona kabisaa anachati tu hana mpango na wewe.

Bado kuna kazi kubwa sana katika hili.
 
Back
Top Bottom