Serikali yaondoa ukomo wa Matumizi ya Vitambulisho vya Taifa
Naomba nipewe namba ya huyo mrembo anastazia, pia nipewe email yake, na twitter yake, nataka nimuoe haraka inavyowezekana, nawasilisha
 
Nchi haina hela inataka kuhuisha huisha vitu , uliona wapi ?
 
Nadhani sio sahihi.
Watu hubadilika sura, dini, kazi, mahali
Elimu

Lengo la Renew ni ili kuona mabadiliko ndani ya miaka 10, hii itawasaidia serikali kujua kina nani wamekufa na nani wako hai.

Serikali imekosea
 
wamefanya makosa sana.
ili litakuja kugarimu pale unashida kurudisha kitambulisho au wanaotaka kutumia kitambulisho kwa ajili ya kulizisha kuwa ni wewe.

dini unaweza kubadilisha au ubini. Makazi mpaka leo kuna watu wanapanga na wamesajili sio sehemu kwa sasa wanpoishi mwisho wa siku kurudisha taarifa zako utaulizo zile taarifa.
 
Ni umasikini wa nchi tu kukwepa gharama ya kutengeneza card mpya lakini duniani kote vitambulisho hivi vina expire lengo ni muhusika kuhuwisha, (update) taarifa zake. Picha uliyoweka Leo kwenye kitambulisho ukiwa na miaka 20 haitakuwa sawa wakati ukiwa na miaka 40.hivyo huwezi kusema utumie kitambulisho hicho milele wakati details zako zinabadilika

Huu nuongo at its best, ID ukomo wake unapokufa, acha kuongopa humu
 
Mi huwa sielewe hata umuhimu wake.

Wangetujaza passport tu basi. Tangu watu waamepewa vile vya kwanza hadi leo hawajawahi kuvitumia .
 
Bora kitambulisho cha taifa kiwe cha milele
Lakini uhai hapa duniani sio milele!

Ningeombwa ushauri, ningependekeza kuwa Vitambulisho viendelee kuna na ukomo, lakini kanzi data iunganishwe na ya vizazi na vifo.

Vitambulisho vinavyoisha muda viwe "renewed automatically" baada ya kuhakiki kuwa mwenye kitambulisho yuko hai. Mwenye Kitambulisho atumiwe ujumbe kuwa kiko tayari kwa kuchukuliwa. Kama shida ni malipo, basi kusiwe na ada.
 
Hapa ndio utaona watu wa serikali hawatumii akili au wanaweka mazingira ya kupiga. Waliweka muda wa nini kama sio kueleta gharama zisizo za msingi
 
Serikali imesikia kilio cha Wananchi na imetangaza rasmi kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA), vilivyomalizika muda wake baada ya kufanya mabadiliko ya kanuni za usajili na utambuzi wa watu.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne tarehe 21 Februari 2023 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na hali ya utolewaji wa vitambulisho hivyo.​
View attachment 2525037

--

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema wamefanya mabadiliko ya kanuni ya utambuzi na usajili ili kuruhusu kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa.

Masauni ametoa kauli hiyo leo Jumanne Februari 21, 2023 wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na hali ya utolewaji wa vitambulisho.

Waziri huyo, amesema marekebisho ya kanuni yamekamilika na zimeshaanza kutumika baada ya kutangazwa rasmi katika gazeti la Serikali la Februari 17, 2023.

"Nitoe rai kwa watoa huduma kwa wananchi hasa taasisi za kifedha, benki na kampuni za simu kuendelea kuvitambua na kuvitumia vitambulisho vya Taifa vyenye tarehe ya ukomo uliopita kwa sababu havitakuwa na ukomo tena wa matumizi.

"Marekebisho hayo hayahusiani na vitambulisho vya wageni wakazi na wakimbizi na kwamba muda wa vitambulisho hivyo uzingatiwe," amesema Masauni.

Kwa uamuzi huo wa Serikali, wananchi sasa wataondokana na wasiwasi pamoja na hofu pale vitambulisho vyao vya taifa vitakapokwisha muda wake.

Lakini sasa hakutakuwa na ukomo tena na hawatalazimika kuvihuisha kwa kulipa Sh 20,000.

MWANANCHI

Pia, soma; Kwanini kitambulisho cha taifa kina muda wa kuisha matumizi
Watoe pi na ukomo wa wa leseni za udereva
 
kuna mwanadada alikua akitumia mkorogo alipiga picha ya Nida akiwa mweupe pe kama mzungu,punde akaacha mkorogo akarudi kua cheusi mangarama.

je'nida wanaweza kumkubalia kurudia picha ili aweke ya sasa akiwa cheusi mangala,maana anadai akitoa kitambulisho kwenye michongo yake ya kazi uko wanamkataa katakata wanasema sio yeye awaonyeshe nida yake.
 
Serikali imesikia kilio cha Wananchi na imetangaza rasmi kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA), vilivyomalizika muda wake baada ya kufanya mabadiliko ya kanuni za usajili na utambuzi wa watu.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne tarehe 21 Februari 2023 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na hali ya utolewaji wa vitambulisho hivyo.​
View attachment 2525037

--

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema wamefanya mabadiliko ya kanuni ya utambuzi na usajili ili kuruhusu kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa.

Masauni ametoa kauli hiyo leo Jumanne Februari 21, 2023 wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na hali ya utolewaji wa vitambulisho.

Waziri huyo, amesema marekebisho ya kanuni yamekamilika na zimeshaanza kutumika baada ya kutangazwa rasmi katika gazeti la Serikali la Februari 17, 2023.

"Nitoe rai kwa watoa huduma kwa wananchi hasa taasisi za kifedha, benki na kampuni za simu kuendelea kuvitambua na kuvitumia vitambulisho vya Taifa vyenye tarehe ya ukomo uliopita kwa sababu havitakuwa na ukomo tena wa matumizi.

"Marekebisho hayo hayahusiani na vitambulisho vya wageni wakazi na wakimbizi na kwamba muda wa vitambulisho hivyo uzingatiwe," amesema Masauni.

Kwa uamuzi huo wa Serikali, wananchi sasa wataondokana na wasiwasi pamoja na hofu pale vitambulisho vyao vya taifa vitakapokwisha muda wake.

Lakini sasa hakutakuwa na ukomo tena na hawatalazimika kuvihuisha kwa kulipa Sh 20,000.

MWANANCHI

Pia, soma; Kwanini kitambulisho cha taifa kina muda wa kuisha matumizi

Utaratibu wa ukomo ni kwasabu hizi Picha inatakiwa kupigwa mpya. Lakini na vitu kama anwani za makazi lakini namba ya NIDA haitakiwi kubadilika.
 
Pambana na namba ya NIDA tu hakuna msaada mwingine. Si mlituonaga mabwege sisi wa mwanzoni tulipokuwa tunavifuatilia nyie mkauchuna
Hapana sikuzembea. Niliandikisha kipindi cha mwanzo kabisa. Namba ninayo..
 
Wananchi wanapitia hali ngumu Sana ya maisha halafu mkuja na short stories kuwa serikali imefuta sijui ujinga gani!. Wakati mnaweka ukomo mlifikiria nn na Sana mmefikiria nn kuondoa ukomo?.
Wamebadili gia angani.
 
Back
Top Bottom