Serikali yaondoa ukomo wa Matumizi ya Vitambulisho vya Taifa
Sawa sasa ulishindwaje kupata kitambulisho na wewe? Maan hakuna wa mwanzoni mwa hili zoezi alikosa kitambulisho
Wa mwanzoni kabisa labda kwenye mashirika huko. Ilipokuja zamu ya kuandikisha huku kwetu nikaenda sikupoteza muda.
 
Serikali imesikia kilio cha Wananchi na imetangaza rasmi kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA), vilivyomalizika muda wake baada ya kufanya mabadiliko ya kanuni za usajili na utambuzi wa watu.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne tarehe 21 Februari 2023 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na hali ya utolewaji wa vitambulisho hivyo.​
View attachment 2525037

--

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema wamefanya mabadiliko ya kanuni ya utambuzi na usajili ili kuruhusu kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa.

Masauni ametoa kauli hiyo leo Jumanne Februari 21, 2023 wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na hali ya utolewaji wa vitambulisho.

Waziri huyo, amesema marekebisho ya kanuni yamekamilika na zimeshaanza kutumika baada ya kutangazwa rasmi katika gazeti la Serikali la Februari 17, 2023.

"Nitoe rai kwa watoa huduma kwa wananchi hasa taasisi za kifedha, benki na kampuni za simu kuendelea kuvitambua na kuvitumia vitambulisho vya Taifa vyenye tarehe ya ukomo uliopita kwa sababu havitakuwa na ukomo tena wa matumizi.

"Marekebisho hayo hayahusiani na vitambulisho vya wageni wakazi na wakimbizi na kwamba muda wa vitambulisho hivyo uzingatiwe," amesema Masauni.

Kwa uamuzi huo wa Serikali, wananchi sasa wataondokana na wasiwasi pamoja na hofu pale vitambulisho vyao vya taifa vitakapokwisha muda wake.

Lakini sasa hakutakuwa na ukomo tena na hawatalazimika kuvihuisha kwa kulipa Sh 20,000.

MWANANCHI

Pia, soma; Kwanini kitambulisho cha taifa kina muda wa kuisha matumizi
Gazeti la serikali ni lipi?
 
Vitambulisho kuwa na ukomo ilikuwa ni sheria,au kanuni?..
Tunaishi kwa matamko
 
Gazeti la serikali ni lipi?
Ndiyo nyaraka rasmi ya kutangaza taarifa rasmi za serikali kama sheria, kanuni, ajira, majina ya waajiriwa, kupandisha vyeo serikalini, mabadiliko yo yote katika serikali nk. Gazeti la serikali (Government Gazette) linachapishwa kwa lugha ya kiingereza na kiswahili. Gazeti hili linachapwa na mpiga chapa wa serikali na linapatikana katika ofisi za umma.

Gazeti la serikali ni kwa ajili ya matumizi ya serikali tofauti na Habari Leo au Daily News ambayo ni kwa matumizi ya wananchi.
 
Jina lake hlo gazeti la serikali ni lipi? Au ndo hvyo jina lake ni Gazeti la serikali ? Leo nilikuwa ofsi ya mkuu wa wilaya ubungo pale mapokezi sijaliona hlo gazeti, ofsi za Uma hzo huwa ni zipi mana hata TRA tuu pale Kimara huwa silioni ..... Taarifa mhimu kama hzo waende broadcast waachane na analog kichaka cha upigaji
 
Serikali imesikia kilio cha Wananchi na imetangaza rasmi kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA), vilivyomalizika muda wake baada ya kufanya mabadiliko ya kanuni za usajili na utambuzi wa watu.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne tarehe 21 Februari 2023 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na hali ya utolewaji wa vitambulisho hivyo.​
View attachment 2525037

--

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema wamefanya mabadiliko ya kanuni ya utambuzi na usajili ili kuruhusu kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa.

Masauni ametoa kauli hiyo leo Jumanne Februari 21, 2023 wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na hali ya utolewaji wa vitambulisho.

Waziri huyo, amesema marekebisho ya kanuni yamekamilika na zimeshaanza kutumika baada ya kutangazwa rasmi katika gazeti la Serikali la Februari 17, 2023.

"Nitoe rai kwa watoa huduma kwa wananchi hasa taasisi za kifedha, benki na kampuni za simu kuendelea kuvitambua na kuvitumia vitambulisho vya Taifa vyenye tarehe ya ukomo uliopita kwa sababu havitakuwa na ukomo tena wa matumizi.

"Marekebisho hayo hayahusiani na vitambulisho vya wageni wakazi na wakimbizi na kwamba muda wa vitambulisho hivyo uzingatiwe," amesema Masauni.

Kwa uamuzi huo wa Serikali, wananchi sasa wataondokana na wasiwasi pamoja na hofu pale vitambulisho vyao vya taifa vitakapokwisha muda wake.

Lakini sasa hakutakuwa na ukomo tena na hawatalazimika kuvihuisha kwa kulipa Sh 20,000.

MWANANCHI

Pia, soma; Kwanini kitambulisho cha taifa kina muda wa kuisha matumizi
Imesikia kikio cha wananchi au wameona ngoma ngumu watachemka kabisa..
 
Bado ni upigaji vitambulisho kupata ninda mpaka uonge ndo upate namba. Afu usitaje shida dooh bongo
 
Jina lake hlo gazeti la serikali ni lipi? Au ndo hvyo jina lake ni Gazeti la serikali ? Leo nilikuwa ofsi ya mkuu wa wilaya ubungo pale mapokezi sijaliona hlo gazeti, ofsi za Uma hzo huwa ni zipi mana hata TRA tuu pale Kimara huwa silioni ..... Taarifa mhimu kama hzo waende broadcast waachane na analog kichaka cha upigaji
Linaitwa Gazeti la Serikali kwa kiingereza Government Gazette.

Ni kweli usingeweza kuliona kwa sababu mara nyingine haliwekwi wazi kwa matumizi ya kila raia. Lakini ungeliomba wangekupatia ila inakuwa vizuri unapoliomba ujue namba ya gazeti unalohitaji, tarehe na mwezi.
 
Serikali imesikia kilio cha Wananchi na imetangaza rasmi kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA), vilivyomalizika muda wake baada ya kufanya mabadiliko ya kanuni za usajili na utambuzi wa watu.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne tarehe 21 Februari 2023 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na hali ya utolewaji wa vitambulisho hivyo.​
View attachment 2525037

--

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema wamefanya mabadiliko ya kanuni ya utambuzi na usajili ili kuruhusu kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa.

Masauni ametoa kauli hiyo leo Jumanne Februari 21, 2023 wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na hali ya utolewaji wa vitambulisho.

Waziri huyo, amesema marekebisho ya kanuni yamekamilika na zimeshaanza kutumika baada ya kutangazwa rasmi katika gazeti la Serikali la Februari 17, 2023.

"Nitoe rai kwa watoa huduma kwa wananchi hasa taasisi za kifedha, benki na kampuni za simu kuendelea kuvitambua na kuvitumia vitambulisho vya Taifa vyenye tarehe ya ukomo uliopita kwa sababu havitakuwa na ukomo tena wa matumizi.

"Marekebisho hayo hayahusiani na vitambulisho vya wageni wakazi na wakimbizi na kwamba muda wa vitambulisho hivyo uzingatiwe," amesema Masauni.

Kwa uamuzi huo wa Serikali, wananchi sasa wataondokana na wasiwasi pamoja na hofu pale vitambulisho vyao vya taifa vitakapokwisha muda wake.

Lakini sasa hakutakuwa na ukomo tena na hawatalazimika kuvihuisha kwa kulipa Sh 20,000.

MWANANCHI

Pia, soma; Kwanini kitambulisho cha taifa kina muda wa kuisha matumizi
bora wangesema namba za nida wengi hatuna vitambulisho mbona
 
ni maamuzi ambayo hajazingatia vigezo.
kuna watu kuhama kubadili ubini na zaidi kufariki. sasa wao watajuaje hayo yoye kama hakuna ku renewl? au mtu akibadili ubini aende Nida je akifariki watajuaje?
 
Kungekuwa na ufanisi serikalini ku-renew ingekuwa muhimu lakini kwa hali ilivyo sasa itakuwa mzigo mzito sana kwa serikali.
 
Hapo ndo majanga na ile mashine ya chuga haijawai semekana ilipo hapo wasomali tuwategemee kuwa tz kwa wingi
 
Serikali imefuta Ukomo wa Muda wa Matumizi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kwa Watanzania wote, na kuzitaka taasisi na Mashirika yote yanayotumia utambulisho huo kuendelea kuvitumia bila kuangalia muda wake wa kuisha.

20230221_212005.jpg
 
Back
Top Bottom