Serikali yaongeza mara mbili zaidi mzunguko wa fedha (M3) kutoka 6.5% hadi 12.7%

Hizo hela ni za wapiga dili.hivi unajua kuwa mtaani vijana walikuwa hawasafiri sasa wamerejea safari zao za kufuata mizigo?
Hivi unajua sasa hivi malori ni mizigo mkubwa?
 
Bora hata mchambuzu, kwanza mkongwe humu ndani. Wewe sijui hata umetokea wapi. Unaleta vitu ambavyo havina ukweli. Mtaani kugumu, vitu vimepanda bei, vipato ni vilevile, halafu unaleta utopolo wako?
Hata aluzeti haishikiki.
 
===
Katika kipindi cha miezi tisa sasa Uchumi wa Tanzania umeendelea kuwa imara siku hata siku ambapo ulikuwa kwa wastani wa 5.2% toka 2.1% katika kipindi kama hicho FY2020.

Ukuaji huu unachagizwa zaidi na kuimarishwa kwa Sekta ya Utalii iliyochangia 18.1%,Kilimo kilichochangia 15.1% lakini pia kuimarishwa kwa miundombinu ya Usafirishaji,Mawasiliano na kuimarisha sekta ya fedha nchini,

Mfumuko wa bei umeendelea kusalia katika urari wa tarakimu moja ya kati ya 3-5% hali iliyosababishwa naupatikanaji wa Chakula cha kutosha cha zaidi ya tani laki mbili kwa mujibu wa ripoti za BOT huku ukiyumbishwa kidogo na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kulikosababishwa na janga la COVID 19.

Katika mwaka 2019|2020 Ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi ( M3 ) kwa mujibu wa BOT ulikuwa na kufikia 6.5%,

Majaabu ni ripoti za robo ya tatu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha ujazi huo huo wa fedha zinazomiminika ( liquid money-M3 ) umefikia 12.7% kutoka 6.5% sawa na ongezeko la karibu 100% yaani marambili zaidi kwa kipindi hiki kifupi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan,

Kwa maana nyepesi sasa hivi unaweza kuiandika noti ya Shilingi elfu 10 jina lako na baada ya muda mfupi ikakupata tena ikiwa na jina lako ( Natoa mfano tu sisemi tuchafue noti zetu) tufanyeni kazi vipimo vya kitaalamu vinaonesha pesa tayari iko mtaani inamiminika ila lazima tufanye kazi kwa bidii hakuna pesa ya bure,

Wakati huohuo Ujazi wa fedha kwa tafsiri finyu ( M2 ) nayo imeongezeka kutoka 9.1% FY2019|2020 hadi 14.9% hivi sasa huku akiba yaani ( M0 ) nayo ikikua kutoka 5.7% hadi 6.3% yaani kila sekta mambo ni bambam na Rais Samia Suluhu Hassan,

Ukuaji huu wa pesa yaani M3,M2 na M0 unachagizwa na sera rafiki za Kiuchumi zinazosimamiwa na Rais wa awamu ya sita Mhe Samia Suluhu Hassan anayesimamia kwa Vitendo Uchumi wa Maendeleo ya Watu na Vitu,

View attachment 2070665

View attachment 2070666
Miezi sita tu ya kuwa jf, una post 2000? Insonesha ulivyokuja ki mkakati. Mpe heshima yake mchambuzi
Screenshot_20220106-163023.jpg
 
Stupid, stupid stupid.
Tunahitaji sisi ni kudhibiti mfumuko wa bei, si ujinga ujinga mnaotuletea huu.
Sasa Tanzania bei za vitu zimepanda kwa zaidi ya 100%.
Mbona huko nyuma hatukuwahi kufikia hapa tulipofikia.
 
Huo mzunguko unapita wapi? Huo mzunguko umeasidia nini na umemsaidia nani? huo uchumi na mzunguko ulioongezeka uko mtaa gani?
Hebu twambie kuna faida gani kuongezeka mzunguko ikiwa
Mabati bei juu
Mafuta bei juu
CEMENT,NONDO.GAS bei juu....
Unajua hizo data za kuandika wenyewe ni rahisi kukataliwa maana hali mtaani ni tete labda mtwambie huo mzunguko upo zanzibar...

Waliosema namba azidanganyi walimaanisha mtu akiongelea takwimu ni rahisi kutafsiri kwenye maisha halisi kama ni kweli au lah...
Umejaza vitu vya kufikirika lakini kila anayesoma anaona wazi kuwa hali ni mbaya mtaani kila leo bidhaa zinapanda bei......
Labda unaongelea mzunguko wa wajinga ndio umeongezeka.........
 
Wewe mchambuzi mpumbafu tu, Huna hoja kabisa,

Mimi nafanya vitu serious wewe unaleta UCHADEMA kwenye vitu serious,
Unadhihirisha kweli una I'd nyingine, maana umemjuaje Kama Ni mchadema? Ina maana mnajuana. Haya jijibu na ile I'd yako Sasa
Unaleta takwimu ambazo wakati wa mwendazake mlikuwa mnataja za juu lini zimeshuka mpaka zianze kupanda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHADEMA wanateseka sana na performance za Mama
Performance gani ww,, uchumi ulele aliouacha ndugu Magu,, zaidi ya pembejeo na vifaa vya ujenzi kupanda isivyo kawaida ongeza tozo juu,,
Labda ndiyo performance
 
===
Katika kipindi cha miezi tisa sasa Uchumi wa Tanzania umeendelea kuwa imara siku hata siku ambapo ulikuwa kwa wastani wa 5.2% toka 2.1% katika kipindi kama hicho FY2020.

Ukuaji huu unachagizwa zaidi na kuimarishwa kwa Sekta ya Utalii iliyochangia 18.1%,Kilimo kilichochangia 15.1% lakini pia kuimarishwa kwa miundombinu ya Usafirishaji,Mawasiliano na kuimarisha sekta ya fedha nchini,

Mfumuko wa bei umeendelea kusalia katika urari wa tarakimu moja ya kati ya 3-5% hali iliyosababishwa naupatikanaji wa Chakula cha kutosha cha zaidi ya tani laki mbili kwa mujibu wa ripoti za BOT huku ukiyumbishwa kidogo na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kulikosababishwa na janga la COVID 19.

Katika mwaka 2019|2020 Ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi ( M3 ) kwa mujibu wa BOT ulikuwa na kufikia 6.5%,

Majaabu ni ripoti za robo ya tatu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha ujazi huo huo wa fedha zinazomiminika ( liquid money-M3 ) umefikia 12.7% kutoka 6.5% sawa na ongezeko la karibu 100% yaani marambili zaidi kwa kipindi hiki kifupi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan,

Kwa maana nyepesi sasa hivi unaweza kuiandika noti ya Shilingi elfu 10 jina lako na baada ya muda mfupi ikakupata tena ikiwa na jina lako ( Natoa mfano tu sisemi tuchafue noti zetu) tufanyeni kazi vipimo vya kitaalamu vinaonesha pesa tayari iko mtaani inamiminika ila lazima tufanye kazi kwa bidii hakuna pesa ya bure,

Wakati huohuo Ujazi wa fedha kwa tafsiri finyu ( M2 ) nayo imeongezeka kutoka 9.1% FY2019|2020 hadi 14.9% hivi sasa huku akiba yaani ( M0 ) nayo ikikua kutoka 5.7% hadi 6.3% yaani kila sekta mambo ni bambam na Rais Samia Suluhu Hassan,

Ukuaji huu wa pesa yaani M3,M2 na M0 unachagizwa na sera rafiki za Kiuchumi zinazosimamiwa na Rais wa awamu ya sita Mhe Samia Suluhu Hassan anayesimamia kwa Vitendo Uchumi wa Maendeleo ya Watu na Vitu,

View attachment 2070665

View attachment 2070666
Haya peleka jina wakuchague kwenye list ya mawaziri....

Tunachokiangalia je, ukuaji wa uchumi au mzunguko wa fedha unaenda sawia na ukuaji wa kipato cha wananchi? Au tunakazana kufurahisha genge la walio nacho?
 
Back
Top Bottom