===
Katika kipindi cha miezi tisa sasa Uchumi wa Tanzania umeendelea kuwa imara siku hata siku ambapo ulikuwa kwa wastani wa 5.2% toka 2.1% katika kipindi kama hicho FY2020.
Ukuaji huu unachagizwa zaidi na kuimarishwa kwa Sekta ya Utalii iliyochangia 18.1%,Kilimo kilichochangia 15.1% lakini pia kuimarishwa kwa miundombinu ya Usafirishaji,Mawasiliano na kuimarisha sekta ya fedha nchini,
Mfumuko wa bei umeendelea kusalia katika urari wa tarakimu moja ya kati ya 3-5% hali iliyosababishwa naupatikanaji wa Chakula cha kutosha cha zaidi ya tani laki mbili kwa mujibu wa ripoti za BOT huku ukiyumbishwa kidogo na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kulikosababishwa na janga la COVID 19.
Katika mwaka 2019|2020 Ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi ( M3 ) kwa mujibu wa BOT ulikuwa na kufikia 6.5%,
Majaabu ni ripoti za robo ya tatu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha ujazi huo huo wa fedha zinazomiminika ( liquid money-M3 ) umefikia 12.7% kutoka 6.5% sawa na ongezeko la karibu 100% yaani marambili zaidi kwa kipindi hiki kifupi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan,
Kwa maana nyepesi sasa hivi unaweza kuiandika noti ya Shilingi elfu 10 jina lako na baada ya muda mfupi ikakupata tena ikiwa na jina
lako ( Natoa mfano tu sisemi tuchafue noti zetu) tufanyeni kazi vipimo vya kitaalamu vinaonesha pesa tayari iko mtaani inamiminika ila lazima tufanye kazi kwa bidii hakuna pesa ya bure,
Wakati huohuo Ujazi wa fedha kwa tafsiri finyu ( M2 ) nayo imeongezeka kutoka 9.1% FY2019|2020 hadi 14.9% hivi sasa huku akiba yaani ( M0 ) nayo ikikua kutoka 5.7% hadi 6.3% yaani kila sekta mambo ni bambam na Rais Samia Suluhu Hassan,
Ukuaji huu wa pesa yaani M3,M2 na M0 unachagizwa na sera rafiki za Kiuchumi zinazosimamiwa na Rais wa awamu ya sita Mhe Samia Suluhu Hassan anayesimamia kwa Vitendo Uchumi wa Maendeleo ya Watu na Vitu,
View attachment 2070665
View attachment 2070666