Serikali yapiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vikiwemo Wimpy Kid ili kulinda mila, desturi na tamaduni za Kitanzania

Wamekurupuka.

Hivyo vitabu tumenunua kwa watoto wetu na tumevisoma.

Havina hizo content.
Prof alidanganywa na kuna uwezekano yeye na kamati yake hawajavisoma hivyo vitabu
 
gays mmechefukwa na kupanic
Adhominem attack, mimi si gay, nakueleza hoja unaleta viroja.

Wizara imepiga marufuku vitabu kwa fake news za Whatsapp.

You are the laughingstock of the world!
 
Achaga ujuaji wa kisengerema kwenye mambo mazito. Kama una asili ya kubinuliwa, usitake kuambukiza vizazi vijacho.
Hujatoa hoja ya kukanusha hoja yangu, unakuja na matusi tu.

Hiyo ni alama ya mtu asiye na hoja na asiyeweza kujadiliana kwa mantiki.

Ni hivi, serikali yako imepiga marufuku vitabu kwa kuangalia fake news za Whatsapp.

Haiko makini.

Ni hilo tu. Fact.

Hayo mengine ni matatizo yako ya kisaikolojia na ya kukosa uwezo tu.
 
Msiwe na ujuaji sana Mazee.


Wizara haiwez kukulupuka kupiga marufuku kitu Kwa Hisia tu.

Hapo wamepitia vitabu vyote kupitia tume iloundwa na Wizara na wakajiridhisha
Hapa umeweka mahaba tu bila fact.

Wizara yako hata haijaeleza specifics kwa nini imepiga marufuku vitabu zaidi ya the awkwardly banal mila na utamaduni clause ambayo it is so overused and vague that it could mean anything.

Yani hata JF inaweza kufungwa kwa sababu uzi wa kula tunda kimasihara unakiuka mila na utamaduni za Mtanzania.

Hogwash!
 
Waziri gani aliviruhusu kuingizwa na kusambazwa kwenye mashule hayo kinyume na maadili na utamaduni wa Kitanzania?

Huku ndio kufungua nchi kuruhusu watu wenye tamaa ya kujamiiana jinsia moja?

Huu utawala ukiondoka kuna mtu ni lazima aondolewe kinga na kushitakiwa period!
 
Nimejikuta nakumbuka kitabu changu cha kiswahili na chapter zake
Siku ya gulio katerero
Simba mla watu
Kibanga ampiga mkoloni
Manenge na Mandawa

Hapo ndo tuanzie kama nchi wapi tulikwama tukaja na tamaduni za western?

kwa hasira siku moja nilisafiri mpaka kuona kijiji cha nanjilinji karibu na msola ili kujionea simba alipoandikwa na mwandishi akila watu
na siku moja akauwawa.
 
Mila, desturi na tamaduni za Tanzania sio sheria.

Marufuku ya Waziri pia sio sheria.

Nchi inapaswa kuongozwa na utawala wa sheria.

Tunataka sheria.
Sheria inatoa muongozo wa kipi na vipi kifanyike, na sheria ndio imempa mamlaka na kuongoza kuwa avifute. Hadi hapo sheria imefuatwa.

Kuna hapo umesema, mila, desturi na tamaduni za Tz sio sheria, Mkuu umejidanganya sana. Tambua kuna sheria ya kimila nchi hii na inafanya kazi huko kuna mila, desturi na tamaduni za jamii/makabila ya Tz hadi mambo ya kuchinja yapo huko.

Ukiacha hiyo kuna Kanuni ya adhabu, sura ya 16 inataja makosa ya kimaadili, ambayo yanatokana na hizomila, desturi na tamaduni. Pia zipo kesi za Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa.

Kubwa kuliko zote ipo katiba ya Jamhuri, ambayo ndiyo sheria mama na imetamka bayana hayo mambo ya mila, desturi na tamaduni zetu Tanzania.

Umesemamarufuku ya waziri sio sheria, ni kweli marufuku ya waziri hata raisi mwenyewe sio sheria bali huwa ni amri halali paletu itakapokuwa marufuku hiyo imetolewa kwa mujibu wa sheria fulani. Kwa kuwa sheria ya elimu imempa waziri mamlaka ya kupiga marufuku aina fulani ya vitabu kwenye mtaala wa elimu basi marufuku hiyo ni amri halali.

Mkuu, sheria imefuatwa na hiyo ndiyo sheria unayoitaka.

Ukiwana swali niulize tujifunze pamoja
(NB: Usilete ubishi usio na tija)

Karibu.
 
Moderator sijafurahishwa na kilichofanyika. Headings na kilichoandikwa humu ni vitu viwili tofauti. Why mme merge huu uzi? Ni nia yenu kuififisha ama?
 
Bora hata wangefuta topic ya circle kwenye maths, the earth as a sphere. Nilikuwa sizielewi. Tena bora hiyo sphere, circle sijawahi ielewa
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Sasa wewe ndugu hizo nazo ni hesabu? Just petty mathematics,kuna vyuma, abstract Mathematics science [emoji137][emoji137]
 
Mtoto anaelia ,hii imetosha kuvikimbia
 
Kulikuwa kuna education material approval committee (EMAC), hiyo kamati ipo au waliishaifuta? Maana hiyo kamati ilikuwa na jukumu la kupitisha zana na vifaa vya kufundishia. Ina maana siku hizi watu wanaingiza vifaa hivyo bila kupitishwa na mamlaka za elimu? Sasa kama serikali imepiga marufuku vitabu hivyo mbona haijasema ubaya wake zaidi ya kusema vinaenda kinyume na utamaduni wetu? Au vina ushoga ndani yake? Au usagaji? Kama ni novel tu ingeacha watoto wakuze msamiati wa lugha iliyotumika kuandika. Halafu serikali ingehamasisha waandishi wazawa waandike vyenye utamaduni wetu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Sasa wewe ndugu hizo nazo ni hesabu? Just petty mathematics,kuna vyuma, abstract Mathematics science [emoji137][emoji137]
Nilimaanisha kwa level ya secondary mkuu. Mimi zilinichemsha hasa circle
 
Watoto wadogo wa miaka minne hadi nane walikuwa wanafundishwa kut*mbana huko international schools😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…