Serikali yapiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vikiwemo Wimpy Kid ili kulinda mila, desturi na tamaduni za Kitanzania

Serikali yapiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vikiwemo Wimpy Kid ili kulinda mila, desturi na tamaduni za Kitanzania

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda leo February 13, 2023 kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya Elimu Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada katika Shule za umma na binafsi nchini.

Vitabu vya 16 vilivyopigwa marufuku vimekutwa katika baadhi ya Shule si kama vitabu vya kiada wala ziada ambapo maudhui yake yanakizana na mila, desturi na utamaduni wa Mtanzania na yanahatarisha ukuaji wa Wanafunzi ikiwemo vinavyofundisha mapenzi ya jinsia moja.

Vitabu vilivyopingwa marufuku kutumika na kuwepo shuleni ni Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid - The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever.

Vingine ni Diary of a Wimpy Kid - The Third Wheel na Diary of a Wimpy Kid - Hard Luck, Diary of a Wimpy Kid - The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid -Old School, Diary of a Wimpy Kid -Double Down, Diary of a Wimpy Kid-The Gateway, Diary, Diary of a Wimpy Kid-Diper Overlode.

Vitabu vingine vilivyopigwa marufuku kutumika shuleni ni Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA ( find the words that make you you) na Sex Education a Guide to life.

View attachment 2516384

Prof.Mkenda amesema, uwepo wa vitabu hivyo pia unahatarisha malezi bora ya watoto na kwa shule ambayo itabainika kuendelea kutumia vitabu hivyo mara baada ya katazo la Serikali itachukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na kisheria ikiwemo kufutiwa usajili wake.

“Nahimiza wazazi mkague mabegi ya wanafunzi kuhakikisha vitabu hivi havitumiki nyumbani; ukaguzi na ufuatiliaji huu ni endelevu ili kubaini kama vitabu kama hivi hipo katika shule tuweze kichukua hatua,".Profesa Mkenda”

Prof. Mkenda ametoa rai kwa watanzania kupiga namba 0262160270 ya mezani na 0737 962965 ya mkononi ili kutoa taarifa ya uwepo wa vitabu hivyo shuleni na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa shule yoyote itakayokutwa na vitabu hivyo ikiwemo kufutiwa usajili
Namhakikishia prof kuwa sasa ndio amevitangaza viatsomwa sana
 
Serikali ya Tanzania imeingia mkenge kukubali fake news ya "Diary of a Wimpy Kid" kilichobadilishwa na wahafidhina na kusambazwa Whatsapp?

Kama ni hivyo, Wizara ya Elimu itakuwa kichekesho kikubwa sana.

Kuna siku page moja ya moja ya hivi kitabu ilikuwa inasambazwa Wwhatsapp, ina maandishi ya kushawishi watoto kufanya ngono.

Sasa mwenzetu mmoja akashangaa sana, kwa sababu mtoto wake anavipenda sana hivi vitabu (yupo Uingereza).

Akakichukua kile kitabu, akatafuta ule ukurasa, akakuta ukurasa wa kwenye kitabu na ukurasa ulele unaosambazwa Wwhatsapp ni vitu viwili tofauti.

Tukajua hizi ni kampeni za fake news.

Sasa najiuliza sana, kama habari hizi ni kweli, je, wizara imefanya uhakiki kwenye vitabu?

Au imetumia maandishi yaliyoonekana Whatsapp na kukurupuka?
Hatunaga ueredi sie hata kidogo
 
Vitabu Gani vipo kwenye syllabus hapo? Nachosema kama mmeamua kuzuia content za magharibi basi muache vyote sio kuchagua Moja na kuacha njia zingine 10.

Mfano ukiskiliza bongo fleva 90% zinaimba kuchuma mchicha, kusafisha mtaro, Kwa mpalange n.k watoto wanaziimba bila kukosea verse unadhani ukiondoa vitabu pekee inasaidia?

Ushauri wangu ni kwamba watoto wafundishwe ubaya wa mambo hayo maana watayasikia tu at some point in life. Ila kuzuia haiwezekani maana mmeachia bongo fleva waimbe matusi hayo hayo mnayopinga kwa vitabu. And bongo fleva inasikilizwa zaidi kuliko vitabu kusomwa!!
Sasa unalalamika nini!? Serikali ndo umeanza kuchukua hatua, suburi na hizo nyanja nyingine huenda zikaguswa. Tuache kulalamika ovyo
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda leo February 13, 2023 kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya Elimu Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada katika Shule za umma na binafsi nchini...
Wazungu watu washenzi sana. Yani wanalazimisha na kutumia kila mbinu ilimradi waone watu wanakua mashoga.
 
Ondoa matopic magumu magumu au futa vitabu vyenye topic ngumu ngumu kama equlibrium, atoms, probability katika hesabu, cos, sin n.k

Vimepitwa na wakat havimsaidii mtu wala kijana wa sasa kumudu mazingira

Badala yake hizo topic lete vitabu vifuatavyo

1. Kilimo theory ichukue 10%

2. Kilimo practical 90%

3. Ufugaji theory 10%

4. Ufugaji practical 90%

5. Home decors

6. Welding, plumbing and irrigation system

7. Farm machineries Mechanics

8. Business practical (Biashara jwa vitendo)

9. Money ethics (Kanuni za fedha)

10. Self reliance (Elimu ya kujitegemea)

11. Nchi yako ni tajiri ulipo pana rasirimali nyingi sana Kuishi bila kutegemea Mikopo ya nje

Hicho cha 11 iwe core course kuanzia chekechea hadi PhD, Maana Ili tuendelee lazima mawazo ya utegemezi na utumwa yafutwe kwenye mind ya vizazi vyetu.
Dunia haieendeshwi na topics nyoronyoro kama ulizotaja hapo. Hizo ni fantacy
 
Puhleeezz!!!

Sini mbwembwe tu na kufuata mkumbo baada ya kuona hiyo fake news inatrend online.

Na walivyo hawana akili hata hawajafanya research yoyote kuthibitisha hizo tuhuma ni za kweli, (maana kama wangefanya hivyo wangegundua ni uongo mtupu) wamelibeba tu kama lilivyo.
Kwani si kuna mtu kaweka ushahidi wa kurasa juu hapo.
 
Watanzania wakurupukaji na hawataki fanya tafiti.
Hivyo vitabu vyote ukisoma havina malengo hayo...
Hata uki google search wimpy kid, gayism hutapata matokeo yoyote yale
 
Wazungu watu washenzi sana. Yani wanalazimisha na kutumia kila mbinu ilimradi waone watu wanakua mashoga.
Mbaya zaidi mengi yanayofanyika yanaonekana kama fashion. Mfano uvaaji wa hereni kwa watoto wa kiume, kujichubua ngozi, kuimba imba kwa sauti za kike zenye kulalamika (nazungumzia bongo flavour)

Utamsikia mtoto wa kiume anaimba analalamika hadi unajiuliza huyu ni wa kiume kweli? Na vile walivyo ndio mashaka yanaongezeka!
 
SIvijui hivyo wimp kid ila 14,15 na 16 kweli walimu wanawafundishia wanafunzi? Like seriously??
Kuna vitabu vya kufundishia madarasani.
Hivi vingine unavikuta kwenye library za shule na wanafunzi huazima kwenda kusoma majumbani kwao na kuvirejesha.
 
Au mimi macho yangu hayaoni vizuri?
Shida iko wapi kwenye hicho kitabu?
Mashoga (wanaume) mmoja akijifanya Mama na mwingine baba wakishindiliana mboo mkunduni huku wakilea mtoto kamą baba na Mama japo wote wanaume. Hii ni sawa kwako?
 
Sasa unalalamika nini!? Serikali ndo umeanza kuchukua hatua, suburi na hizo nyanja nyingine huenda zikaguswa. Tuache kulalamika ovyo
Nyie ndio hamjitambui, Dunia ya Sasa content 80% ipo Mitandaoni badala mbane huko na media za bongofleva mko busy na mavitabu ambayo yanasomwa IST pekee sio kayumba. Hivi mnajitambua kweli?
 
Tanzania ndio nchi pekee inasubiri vitu kuingia vishalipa kodi na takataka kisha ndio vinakatazwa.

Ulaya mzigo wako unaishia bandarini
Sio kweli bwashee, Huawei iliingia USA miaka shazi na baadae ikala ban, Tiktok vivyo hivyo na mengine mengi tu…
 
Back
Top Bottom