Serikali yapiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vikiwemo Wimpy Kid ili kulinda mila, desturi na tamaduni za Kitanzania

Serikali yapiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vikiwemo Wimpy Kid ili kulinda mila, desturi na tamaduni za Kitanzania

Serikali ya Tanzania imeingia mkenge kukubali fake news ya "Diary of a Wimpy Kid" kilichobadilishwa na wahafidhina na kusambazwa Whatsapp?

Kama ni hivyo, Wizara ya Elimu itakuwa kichekesho kikubwa sana.

Kuna siku page moja ya moja ya hivi kitabu ilikuwa inasambazwa Wwhatsapp, ina maandishi ya kushawishi watoto kufanya ngono.

Sasa mwenzetu mmoja akashangaa sana, kwa sababu mtoto wake anavipenda sana hivi vitabu (yupo Uingereza).

Akakichukua kile kitabu, akatafuta ule ukurasa, akakuta ukurasa wa kwenye kitabu na ukurasa ulele unaosambazwa Wwhatsapp ni vitu viwili tofauti.

Tukajua hizi ni kampeni za fake news.

Sasa najiuliza sana, kama habari hizi ni kweli, je, wizara imefanya uhakiki kwenye vitabu?

Au imetumia maandishi yaliyoonekana Whatsapp na kukurupuka?
Msiwe na ujuaji sana Mazee.


Wizara haiwez kukulupuka kupiga marufuku kitu Kwa Hisia tu.

Hapo wamepitia vitabu vyote kupitia tume iloundwa na Wizara na wakajiridhisha
 
Wewe ni mpumbavu kabisa huwezi hata kutambua maudhui ya kitabu, wewe wataka wataje neno ushoga ndo ujue kwamba wanaeneza ushoga.
Ndio nieleze wewe sasa, A Diary of a Wimpy Kid ina maudhui gani yaliyofanya yaharibu maadili ya Mtanzania?
 
Acha ukoloni!! Kwahiyo mtoto kusikiliza bongo flavor ni ukosefu wa maadili?
Hapana maana yangu hiyo miziki mingi ina maudhui ya ngono na matusi, "inama nisafishe mtaro... una rambo mi nina mua nitakupwelepeta....kausikilize wimbo wa Lina na Dogo janja.... hizo singeli ndio usiseme"
 
Nimegundua watu hawasomi ila wanakurupuka mfano kuna mtu kaweka soft copy hapo juu hali ya kua na yeye anaamini hicho kitabu kinakiuka maadili lakini ukisoma huoni hicho kitu [emoji3] sasa tatizo ni lugha au ushabiki hadi watu wanajitia upofu
Mtanzania anajua ubishi na sio fact.... ndio maana tupo nyuma nyuma tu kwenye kila jambo kasoro Umbea
 
Ndio nieleze wewe sasa, A Diary of a Wimpy Kid ina maudhui gani yaliyofanya yaharibu maadili ya Mtanzania?
Kama unajua kiingereza translate haya maneno unieleza kama ni mazuri kwa watoto wako.
Screenshot_20230214-112606.jpg
 
Wewe ni mpumbavu kabisa huwezi hata kutambua maudhui ya kitabu, wewe wataka wataje neno ushoga ndo ujue kwamba wanaeneza ushoga.
Mbona umekasirika sana ushajua umeingizwa mkenge eeh 🤣
Bado hujamjibu huo Ushoga au Maudhui ya Ushoga yapo ukurasa wa ngapi kwenye hicho kitabu cha Wimpy Kid?? Kwanza hata umeshawahi kukisoma kweli au unajiaibisha tu hapa🤔
Lol
 
Kama unajua kiingereza translate haya maneno unieleza kama ni mazuri kwa watoto wako. View attachment 2517046
Hizo kurasa hazipo kwenye a Diary of a Wimpy Kid, kumbe hata hicho kitabu hukijui halafu unajitia ujuaji usokua na maana, ungetulia ueleweshwe dada makasiriko hayajengi,

Mtoto anaeleweshwa kuutambua mwili wake kulingana na mabadiliko ya mwili (its for teenagers)
 
Kama unajua kiingereza translate haya maneno unieleza kama ni mazuri kwa watoto wako. View attachment 2517046
Sasa hiyo ni Diary ya Wimpy Kid kweli? Hebu acha utani wako ndio maana nikakuuliza hicho kitabu umekisoma kweli au unakurupuka?.... haya nitajie jina la kitabu ulichoweka hiyo kurasa,

Btw, kuna mtu huko juu ameweka soft copy ya Wimpy Kid kipitie
 
Tunakumbushana sana mtasikia matetemeko ndio hayo ya Syria na Uturuki.

Vita ndio hizo Russia, Ukraine, Congo na sasa USA anatunishiana misuli na China.

Manabii wa uongo ndio hao wamejazana kila kona.

Upendo utapoa, ndio unaona kila mwanasiasa anaiba na wengine wanamuonea wivu Babu Tale na Udaktari wake.

Atakayevumilia hadi MWISHO ndiye atakayeokoka.

Prof. Mkenda kazana kuwalinda watoto ijapokuwa Dunia inakwenda kasi sana na muda hautusubiri.

Mungu wa mbinguni akutie nguvu ya ziada Adolf.
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda leo February 13, 2023 kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya Elimu Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada katika Shule za umma na binafsi nchini.

Vitabu vya 16 vilivyopigwa marufuku vimekutwa katika baadhi ya Shule si kama vitabu vya kiada wala ziada ambapo maudhui yake yanakizana na mila, desturi na utamaduni wa Mtanzania na yanahatarisha ukuaji wa Wanafunzi ikiwemo vinavyofundisha mapenzi ya jinsia moja.

Vitabu vilivyopingwa marufuku kutumika na kuwepo shuleni ni Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid - The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever.

Vingine ni Diary of a Wimpy Kid - The Third Wheel na Diary of a Wimpy Kid - Hard Luck, Diary of a Wimpy Kid - The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid -Old School, Diary of a Wimpy Kid -Double Down, Diary of a Wimpy Kid-The Gateway, Diary, Diary of a Wimpy Kid-Diper Overlode.

Vitabu vingine vilivyopigwa marufuku kutumika shuleni ni Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA ( find the words that make you you) na Sex Education a Guide to life.

View attachment 2516384

Prof.Mkenda amesema, uwepo wa vitabu hivyo pia unahatarisha malezi bora ya watoto na kwa shule ambayo itabainika kuendelea kutumia vitabu hivyo mara baada ya katazo la Serikali itachukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na kisheria ikiwemo kufutiwa usajili wake.

“Nahimiza wazazi mkague mabegi ya wanafunzi kuhakikisha vitabu hivi havitumiki nyumbani; ukaguzi na ufuatiliaji huu ni endelevu ili kubaini kama vitabu kama hivi hipo katika shule tuweze kichukua hatua,".Profesa Mkenda”

Prof. Mkenda ametoa rai kwa watanzania kupiga namba 0262160270 ya mezani na 0737 962965 ya mkononi ili kutoa taarifa ya uwepo wa vitabu hivyo shuleni na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa shule yoyote itakayokutwa na vitabu hivyo ikiwemo kufutiwa usajili
Ni Waziri yupi aliyewahi kuviruhusu kutumika? Hii Wizara mbona siku hizi pilika pilika ni nyingi sana kuna nini?
 
Mila, desturi na tamaduni za Tanzania sio sheria.

Marufuku ya Waziri pia sio sheria.

Nchi inapaswa kuongozwa na utawala wa sheria.

Tunataka sheria.
Ni kitu kidogo tu, tutaipelekea mswada Bunngeni ili iwe sheria; kama siyo sheria kwa sasa. Si unataka utawala wa sheria?
Kuna siku mtu atakuja kwako halafu atakata kichwa mtu kwa upanga halafu utaanza kumtetea kwa kusema kuwa haipo sheria inayomkataza mtu kukata kichwa mtu mwingine kwa upanga, isipokuwa kuna sherai inayokataza kuua
 
Hii vita viongozi njaa wa Tz hawaiwezi,hayo nimaigizo matupu,ushoga bongo hawawezi kuugusa,alishindwa jpm ataweza huyu mtembeza bakuli.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ngojaa wapate onyo kutoka nje, utawaona na warakaa mrefuuu. Utaskia ni msimamo wa waziri pekee sio msimamo wa serikali.

Huwa nachekaga sanaaaa.
 
Back
Top Bottom