Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Ni kosa ambalo linaweza kuja kusababisha ajali nyingi sana. Attention span ya ubongo wa mwanadamu ina ukomo wake. Kwa tunaofundisha tunajua kuwa huwezi kumfundisha mwanafunzi mfululizo kwa saa mbili ukaamini kuwa kweli umefundisha, kila baada ya dakika hamsini umpe mapumziko hata ya dakika nne tu ili kujenga upya attention span yake.

Dereva wa basi akikaa kwenye usukani kwa zaidi ya masaa mawili mfululizo usiku kuna chance kubwa sana ya kuangusha basi hilo na kuua watu. Wakitaka kuhalalisha safari za masaa 24 basi waweke utaratibu wa kuwa na madereva wawili kwenye basi pamoja na kitanda cha dereva kupumzikia kama ambavyo marubani wa safari ndefu wanavyokuwa watatu kwa ajili ya kuepeana zamu za kuendesha chombo.
 
Safi sana, habari njema mno.
Sikuwahi kuona sababu ya msingi kusimamisha usafiri wa abiria usiku.
 
Wangeanza kwa baadhi ya route fupi kama Moro - Dar, Arusha - Moshi, Tanga - Dar, Mbeya - Iringa, Lindi - Mtwara, Mwanza - Musoma n.k...

Bado kuna maeneo barabara zake sio rafiki kusafiri usiku, haswa zile ambazo hutumiwa sana na malori...

Serikali kama inatamani kuwe na uchukuzi wa watu kwa masaa 24, ilipaswa iimarishe usafiri wa njia ya reli...

Kipindi cha msimu wa mvua hasa masika, utaratibu huu wa kusafiri masaa 24 usitishwe kwa kuwa kuna baadhi ya njia si salama na hata uono wakati huu huwa hafifu...

Kwa wale wanaopenda kusafiri usiku kwa kutumia magari binafsi, huenda ukawa mwisho wa mimbio sababu kuna uwezekano trafiki wakawa wanakaa barabarani hadi mida ya popo...
 
Wale madereva wa malori wenye bifu na madereva wa mabus ambao wakiona bus inamuovertake alaf mbele kuna gari inakuja na yeye anaongeza mwendo waache hizo mambo ili ajali za uso kwa uso zisiwe nyingi maana usiku ndo hatari zaidi
 
Madereva wa Tz mchana kweupe wanashindwa kufuata mwongozo wa taa za barabarani mpaka awepo askari wa usalama barabarani (trafiki), kweli watafuata sheria za barabarani usiku wa giza, hapa tunajipangia kuongeza takwimu za ajali mbaya za barabarani.
Usiku hakuna traffic watafata tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…