Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Ni kosa ambalo linaweza kuja kusababisha ajali nyingi sana. Attention span ya ubongo wa mwanadamu ina ukomo wake. Kwa tunaofundisha tunajua kuwa huwezi kumfundisha mwanafunzi mfululizo kwa saa mbili ukaamini kuwa kweli umefundisha, kila baada ya dakika hamsini umpe mapumziko hata ya dakika nne tu ili kujenga upya attention span yake.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeruhusu Mabasi ya abiria kufanya usafirishaji wa Saa 24, baaada ya kujiridhisha kiusalama, mwamko wa wananchi, huduma za mawasiliano pamoja na miundombinu ya usafirishaji.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi, Jumanne Sagini wakati anaongea na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na kusema kuwa wamefikia maamuzi hayo baada ya Serikali kuimarisha shughuli za uchumi wa wananchi wake wa maeneo ya mjini na Vijijini.
Akiongeza kuwa wamezingatia maoni ya Wadau mbalimbali wakiwemo Wabunge, wamiliki wa mabasi, madereva wa mabasi, wasafiri, Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla.
Aidha, Serikali imetoa maagizo kwa wadau wote wa usafirishaji kuzingatia Sheria, Kanuni na utaratibu wa leseni zao.
Pia madereva wametakiwa kuthibitishwa na LATRA, ambayo itatoa ratiba za safari kwa saa 24, TANROADS kuhakikisha ubora wa miundombinu, Serikali za Mitaa kuhakikisha zinasimamia usalama wa abiria kwenye huduma wanazosimamia pamoja na Jeshi la Polisi kusimamia Usalama wa watu na mali zao.
Dereva wa basi akikaa kwenye usukani kwa zaidi ya masaa mawili mfululizo usiku kuna chance kubwa sana ya kuangusha basi hilo na kuua watu. Wakitaka kuhalalisha safari za masaa 24 basi waweke utaratibu wa kuwa na madereva wawili kwenye basi pamoja na kitanda cha dereva kupumzikia kama ambavyo marubani wa safari ndefu wanavyokuwa watatu kwa ajili ya kuepeana zamu za kuendesha chombo.