Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Kuruhusu usafiri kwa saa 24 ni kutengeneza bomu ajali zitakuwa nyingi
Huo ni Ushamba na Woga wa Maendeleo, nchi nyingi tu za Africa Mabus yanasafiri saa 24..

Saa 12 asubuhi kuna Bus.
Saa 4 asubuhi kuna Bus.
Saa 7 mchana kuna Bus

Ni hivyo hivyo kwa masaa 24, serikali inatakiwa kuhakikisha kila bus linakua na Madereva 2 kwa route ndefu full stop...!
 
Kisababishi kikubwa cha ajali barabarani ni malori. Malori yamekuwa mengi sana, halafu yapo yanayoenda mwendo wa konokono lakini mengine yanaenda mwendo panya, breki za ghafla. Changamoto wanayoipata madreva wa magari ya abiria ni kulazimika Ku overtake msululu wa malori mara wakati huo huo akiyakadria yanayokuja face to face.
Giza la usiku linaleta hatari ya kuyaparamia malori yaliyoegeshwa barabarani bila kuweka alama stahiki.
Hii sgr ikamilike tu, RAIA tutumie train, tuyaache malori yatambe barabarani.
 
Madereva wa Tz mchana kweupe wanashindwa kufuata mwongozo wa taa za barabarani mpaka awepo askari wa usalama barabarani (trafiki), kweli watafuata sheria za barabarani usiku wa giza, hapa tunajipangia kuongeza takwimu za ajali mbaya za barabarani.
Yakiwakuta hakuna kuwaonea huruma

Ova
 
Cha muhimu madereva wapate muda mwingi wa kupumzika kabla ya safari zao

Baadhi ya madereva itawachukua muda kuzoea kuendesha usiku

Usiku madereva wenyewe wazoefu wa malori huwa ni kawaida kukuta wamechochora kuingia vichakani au kuhama site yake kuingia upande wa pili kwa sababu ya usingizi

Huwa matukio hayo hayaripotiwi kwa sababu ni gari za mizigo
 
Hapo nimeelewa Mkuu
Tena wangekuwa wanapigwa faini hata 5m ili kuwakomesha wasirudie.
 
😂😂😂😂😂😂kinachosubiriwa hapa ni swala la muda tu. Kibuyu kitaitika
 
Duuh pole aseeh...... Mm nipo ndani akn nilivosoma hii km ndo tumevamiwa
 
Hivi unajua mjinga mmoja barabarani anaweza kusababisha ajali hata kwa mtu mwenye akili zake timamu.

Ndiyo maana nikasema safari za usiku wataua watu wengi sana chanzo inaweza kuwa hayo malori speed au barabara mbovu jumlisha magari mabovu.

uhai ukitoka harudi
 
Mbona hapo Rwanda huwa tunasafiri usiku, kwanini iwe shida kwa Tanzania. Hapo Kenya tangu 1990 wanasafiri usiku mpaka Leo. Nadhani tuangalie uhitaji kuliko madhara. Halafu sio kila basi litasafiri usiku, ni baadhi tu.
Swala siyo kuendesha usiko bali ni muda ambao Dereva anakaa kwenye usukani. Rwanda Inalingana na mkoa wa Mororgoro ampao kutoka mpakani mpaka mpakani ni mwendo wa saa moja tu, siyo sawa na kusafiri Dar hadi Bukoba kwa masaa takriban 30.
 
Zamani tulisafiri usiku..mpaka waziri mkuu Malecela alipo amuru vinginevyo....
 

Wewe ukisafiri mchana inatosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…