Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Hizo zilizolala ziamshwe...hapa unaongelea bandari ya kisasa zaidi ya DAR
Kwa hili naipongeza serikali ya Magu
Wachina wangeithibit bandari ya bagamoyo for 40 yrs,
Wangefanya hujuma sana kwenye bandari ya Dar na Tanga ili mizigo mingi ipite kwao
 
Na kesho tunaenda bagamoyo kwa azam sea link nauli 2500 sasa sijui kama wamesutisha au ndo tunaenda kuzindua
 
Kwa hili naipongeza serikali ya Magu
Wachina wangeithibit bandari ya bagamoyo for 40 yrs,
Wangefanya hujuma sana kwenye bandari ya Dar na Tanga ili mizigo mingi ipite kwao

Wao wanajenga hawadhibiti, kama unashindwa kudhibiti ni wewe si kazi yao hiyo.
 
Kipindi cha jamaa wa kule ilikoelekea njia iliyokata kulia pale Msolwa,Ilikua miaka kumi ya mavuno kwa manyang'au wa dunia na makuwadi wao wa hapa nchini.
 
Bei ya ardhi Bagamoyo itashuka sasa

Hapana itaendelea kupaa.

Hizi pwani zimebarikiwa huwezi kushindana nazo hata chembe. Ukiiua bandari utakuta kuna mafuta na mi gas ya kufa mtu.

Hapo sasa.
 
Nionavyo mimi...hoja nyingi ni one way trafic....! Hebu tutumie two way trafic tuone inakuwaje hasa!
 
Hizi legacy za kulazimisha zitatufikisha pabaya ooohoo .......asante magu
 
Hii project haikuwa ya kujenga bandari tu...bali ni pamoja na kuboresha eneo la viwanda vya processing ili tuuze bidhaa nje.
Ahadi ya Magufuli ni Tanzania ya viwanda sasa kama mradi unaohusiana na viwanda unakatwa na sisi tunaanza kuchekelea eti Mkwere anakomolewa basi watanzania wana Tatizo kubwa la udumavu wa akili.

Tusijadili kwa chuki dhidi ya mkwere bali tujadili kwa utaalamu
 
Last edited:
Habari za faraja sana hizi japo team JK wanatotoa povu sana hapa
 
seems to be a very smart guy. .nakubaliana na suggestions zako 100 percent..reli ujenge ya standard gauge from Tanga ipite arusha mpaka singida I kutana na reli ya dar -mwanza-kigoma same as ile bandari ya Mtwara
 
HAKIKA hii habarii ni njema sanaa sanaa..

Serkali ya JPM IBARIKIWE, tunashkuru sana sanaa..
 
hakuna usanifu pale

Ila ilikuwa ni kuipendelea bagamoyo...kwa maslahi binafsi...najua unayajua
 
Kuan haja sasa mikataba mingi iwekwe wazi. Maana huu mradi nakumbuka ilisemwa kuwa wachina wanafund 100% isipokuwa Tanzania itoe ardhi... Na pia mkataba ulizuia uendelezwaji fulani wa bandari ya Dar es Salaam...
 
Watanzania tuna safari ndefu sana-- siumi maneno, this's MISTAKE! Nitarudia tena na tena, hapa serikali ya Magufuri itakuwa inakosea sana! Bandari ni zaidi ya meli kufunga gati bali container terminals! Bandari zote duniani zinapimwa kwa uwezo wake wa kuhudumia makoentena. Dar es salaam hakuna eneo linaloweza kutufikisha miaka 50 ijayo! Sisi watu wa Kurasini tunaifahamu vizuri hii! Kurasini ya miaka ya 80 sio ya miaka ya 90 na Kurasini ya miaka ya 90 sio ya miaka 2000! Kurasini yote imeisha kwa ajili ya Bandari na sooner or later watahamia Mtoni manake hata Mivinjeni nayo imebaki historia!

Pamoja na Kurasini na Mivinjeni ku-RIP lakini bado bandari ya Dar es salaam haipokei mzigo mwingi wa angalau kulinganisha na Mombasa. Pamoja na Mombasa kupokea mzigo mwingi kuliko sisi lakini nao wameshaona bandari ya Mombasa haitawafikisha miaka 50 ijayo na ndo maana wanaanzisha grand project kule Lamu! Kama lengo la serikali ni kuipanua zaidi bandari ya Dar es salaam basi wafanye declaration kabisa kwamba Temeke yote iwe ni eneo la bandari ya Dar es salaam!!

Kwamba waimarishe bandari ya Mtwara hii ni mistake nyingine! Unless kama tunadanganywa kuhusu gas boom huko Lindi na Mtwara lakini kama ni kweli basi itakuwa taabu sana siku za usoni kuifanya bandari ya Mtwara kuwa multi-purpose... yaani ku-accommodate gas and petroleum shipping lines together with other cargo shipping lines. Sehemu nyingi duniani, bandari zinazo-accomodate meli za mafuta zinakuwa na separate habors coz' ile mimeli ni mikubwa mno!

At least ningewaelewa kama wangesema mradi wanauhamishia Tanga lakini Dar es salaam au Mtwara... hili ni kosa la kiufundi!
 
Hayo ndio maamuzi yanayompaisha Mhe Maghufuli. Aende tu polepole na hili la walala hoi wa mabondeni and for sure tutamsujudu.
 
Alleluya!!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…