Gai da seboga
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 515
- 1,015
Habar zenu mabibi na mababu.
Mwaka jana 2020 mnamo mwezi wa tisa Mheshimiwa Rais John Magufuli alitoa kibali cha ajira mpya za walimu 13,000 kwa shule za Sekondari na Msingi, ambapo katibu wa tamisemi alitangaza majina elfu 8 mwezi wa kumi na moja mwishoni na walimu hao kutakiwa kuripoti kuanzia December 1 mpk 14.
Baada kama wiki moja mbeleni walikuja tena kwenye press kwa waandishi wa habari kueleza sintofahamu zilizotokea katika awamu ya kwanza ya majina 8000 ya walimu, press ile ilihudhuriwa na makatibu wakuu wa wizara tatu yani kulikuwepo na katibu mkuu wa tamisemi, katibu mkuu wizara ya elimu pamoja na katibu mkuu wizara ya utumishi. Kupitia press hiyo walitoa tamko la wazi kuwa majina elfu 8 ilikuwa ni awamu ya kwanza hivyo imebaki majina elfu 5000 awamu ya pili ambayo wataitoa muda si mrefu, wakatoa sababu za kutoa ajira hzo kimakundi eti ni katika kupunguza kusiwe na malimbikizo ya madeni kwa walimu hao.
Baada ya wiki tatu tena mbeleni kulikuwa na tukio la katibu mkuu wa tamisemi kukutana na wakuu wa shule za msingi ambapo katika hutuba yake alisisitiza kuwa kuna shule zaidi ya 2500 hazikupelekewa walimu awamu ya kwanza hivyo watapeleka na hiyo awamu ya pili ya majina 5000 yaliyobaki watawapangia walimu maeneo yenye uhaba zaidi hasa vijijini.
Majuzi hapa Mheshimiwa Raisi Magufuli akapigilia nyundo wakati yupo katika ziara yake huko bukoba akasema wazi kuwa zimetolewa nafasi za walimu elf 8 hivyo watamalizia elfu 5 ili kupunguza changamoto za ufundishaji.
Sasa imeshatimia miezi mitatu lakini Tamisemi bado wako kimya tu, kwako Mheshimiwa Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jaffo ni lini utaachia hayo majina elf 5 ajira za walimu awamu ya pili?? Vijana mtaaani wanateseka sana mpaka wanatia huruma, vijana wanaongoza kuwa na msongo wa mawazo utafikiri ni wazee kwa kukosa kazi.
Mbaya zaidi leo bunge limeanza wawakilishi wetu huko bungeni (wabunge) wanauliza maswali mengine ya miundombinu, umeme, afya, maji, lakini wanasahau kuhoji hili la ajira ambalo kibali chake kimeshatolewa na mhe Raisi??!!
Mh jafo aachia hayo majina ili walau keki ya taifa vijana waifaidi wote.
~Gai da Seboga