Serikali yaunda timu ya wataalamu kupitia upya sakata la Tozo. Yasema zitarekebishwa ila hazitaondoka

Serikali yaunda timu ya wataalamu kupitia upya sakata la Tozo. Yasema zitarekebishwa ila hazitaondoka

Wakati mnapeleka muswada bungeni kwani mliunda kamati ya kufanya upembuzi yakinifu kuhusu tozo? Sasa mnaunda kamati ya kazi gani wakati tayari mnazo evidence za kutosha kabisa kwamba wananchi hawataki tozo maana ni mzigo kwao!

Kuna evidence gani zaidi ya hii?👇
View attachment 2355488

Mategemeo yalikuwa kupata trilioni 1.25 lakini iliyopatikana ni bilioni 360 tuu. Hakuna evidence nzuri kama hii, hiyo kamati italeta majibu ya kisiasa tuu kama yale ya Twaweza..

HATUTAKI TOZO.
Ndiyo shida ya uchaguzi wa 2020, akili ndogo iliyojaa jengoni na hazina Dodoma ndiyo imetufikisha hapa
 
Kamati za kutafuna tozo mkuu, wameshasema wao ni wanadamu jamii ya fisi mkumbuke 😆 😆
 
Ni ujinga mkubwa sana kung'ang'ania tozo, serikali itengeneze mazingira kipato cha mwananchi ili wapate kodi ya kutosha, ng'ombe ili atoe maziwa ya kutosha anahitaji malisho
 
Wakati mnapeleka muswada bungeni kwani mliunda kamati ya kufanya upembuzi yakinifu kuhusu tozo? Sasa mnaunda kamati ya kazi gani wakati tayari mnazo evidence za kutosha kabisa kwamba wananchi hawataki tozo maana ni mzigo kwao!

Kuna evidence gani zaidi ya hii?👇
View attachment 2355488

Mategemeo yalikuwa kupata trilioni 1.25 lakini iliyopatikana ni bilioni 360 tuu. Hakuna evidence nzuri kama hii, hiyo kamati italeta majibu ya kisiasa tuu kama yale ya Twaweza..

HATUTAKI TOZO.

Hakuna mtu anapenda kodi. Kwa wale ambao hawataki kodi na tozo watueleze pesa zinatoka wapi? Naunga mkono kwamba serikali inatakiwa kupunguza matumizi hasa kwenye magari lakini hizi pesa hazitoshi
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imekutana na Umoja wa Makampuni ya Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA), kujadiliana Changamoto na faida zilizopatikana kwa watoa huduma hao baada ya utekelezaji wa tozo zilizokusanywa na Serikali.

"Sote tumekubaliana na maelekezo tuliyopata kutoka serikalini ni kuwa Rais Samia ametuagiza tuangalie upya tozo hii na kuhakikisha kuwa tozo hii inabaki kuwa rafiki na haiwi mzigo kwa Watanzania" alisema Mafuru.

Serikali ya Rais Samia imeendelea kuwa sikivu na kuchukua hatua juu ya malalamiko ya wananchi hususani kwenye suala la Tozo, Lengo ni kuona watanzania wanaendelea kufanya biashara nchini na kuchangia pato la Taifa. Tangu kuanza kwa utekelezaji wa tozo hizo tayari serikali ilipinguza 30% kwenye tozo za simu zilizokusanywa katika mwaka 2021/2022
 
Tatizo sio tu Tozo, nikiunga kifurushi cha mbs 450 za Tigo saa kumi na mbili jioni leo nikatumia WhatsApp na JF tu usiku,kesho asubuhi Tigo wananitext mb zitaisha muda wake jioni hiyo
 
Nimeamua niwadhurumu Tigo, Tsh laki mbili wanayonidai,nitavunja sim card kwakuwa sina watu wa kunitafuta kwa namba hiyo
 
Hatuitaki
Tozo ni kodi mara mbili. Mfanyakazi wa kima cha chini anafanya kazi anapokea ka-mshahara kake, wazazi wake kijijini wanaumwa, anapowatumia fedha zinakatwa! Upande wa pili watawala wanafanya matumizi ya kifahari na ufisadi kwa kwenda mbele huku wakizidi kukamua maskini.
 
Kitendo cha kuleta tozo za kwanza za Simu yakaibuka malalamiko wakarudi tena wakaenda kupitia upya then wakashusha, alafu baada ya mwaka mmoja wakaja tena na tozo nyingine ila style ileile ya mwanzo then wanarudi kupitia upya ila washushe makato haina tofauti na ile ya kuteua kada wa CCM kuwa Mkurugenz wa TPDC alafu baada ya watu kukushangaa unafanya nn ukarudi tena kutengua uteuzi wako ni ishara kuwa hutabiriki! Na hutabiriki sio kama uko vizuri lah ila unaonesha wewe hujui nini unafanya mpaka watu wakulalamikie.

Kama kiongozi unatakiwa ujue hiki ninachoenda kufanya kitaleta matokeo gani kwa wananchi, sio kila siku unajaribu tu! Inshort hatukuamini cos tushajua huna unachojua we unaitikia tu. Naongea nawewe Chief
 
  • Tozo za miamala ya simu zilileta vilio mwaka jana; zikapinguzwa. Wakati bado maumivu tunayasikilizia, wameleta matozo tena benki.
  • Kurudia mchakato ule ule kunatengeza maswali
 
Hapa ndipo watu wanamkumbuka Hayati JPM alikuwa.ana slove matatizo papo kwa papo. Kwenye hili la tozo tusingepoteza muda ni kupunguza au kufuta basi haina haja ya kamati watu wanajitengenezea posho tuu za bure.
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imekutana na Umoja wa Makampuni ya Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA), kujadiliana Changamoto na faida zilizopatikana kwa watoa huduma hao baada ya utekelezaji wa tozo zilizokusanywa na Serikali.

"Sote tumekubaliana na maelekezo tuliyopata kutoka serikalini ni kuwa Rais Samia ametuagiza tuangalie upya tozo hii na kuhakikisha kuwa tozo hii inabaki kuwa rafiki na haiwi mzigo kwa Watanzania" alisema Mafuru.

Serikali ya Rais Samia imeendelea kuwa sikivu na kuchukua hatua juu ya malalamiko ya wananchi hususani kwenye suala la Tozo, Lengo ni kuona watanzania wanaendelea kufanya biashara nchini na kuchangia pato la Taifa. Tangu kuanza kwa utekelezaji wa tozo hizo tayari serikali ilipinguza 30% kwenye tozo za simu zilizokusanywa katika mwaka 2021/2022
Hivi kuna mtu anaona umuhimu wa hawa wabunge wetu?
 
Back
Top Bottom