Serikali yayafungulia magazeti ya MwanaHALISI, Tanzania Daima na Mseto

Huyu ndiye alikuwa Kiherehere cha kufanya uchafu wote ule , huyu alishirikiana na kundi lake kuhujumu kila vyombo vya habari vilivyokuwa tofauti na matakwa ya aliyemtuma , huyu alichangia kuficha kila habari kuhusu chochote ikiwemo Corona .

Ni lazima huyu ajadiliwe hapa ili labda atajitokeza na kuwataja wote waliokuwa wanamtuma , walio hai na Waliokufa , hatuwezi kuwa na viongozi kwenye utumishi wa Umma wenye makandokando kama ya Dr Abbas .Ajiuzulu arudi mitaani ajifunze uungwana .

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO
 
Habari njema sana, nitaanza tena kununua magazeti. Itakuwa burudani kubwa kuwasoma tena akina KONDO TUTINDAGA, NARONYO KICHEERE, SAED KUBENEA, na wengineo. Hawa jamaa huwa hawaogopi kabisaaa kufukua kinyesi, mizoga na yooote yaliyoooza na kuvunda ila yamefichwa!!
Kweli kabisa mkuu,nilisitisha kabisa kununua magazeti!Lakini sasa nitanunua.Maana yale wasiyopenda yaandikwe yataandikwa.Tunataka kujua ukweli au hata kuona mtu/chombo kinahoji juu ya mambo magumu kama Nani alimpiga risasi Tundu,nini kilitokea juu ya miili ya watu waliokuwa wanaokotwa baharini/mitoni?Ni kweli inspector Swila anaumwa? Ilikuwaje "covid 19" wakaingia bungeni? Vyombo vya habari vya kawaida vimeshindwa kuhoji mambo haya
 
Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, leo Alhamisi amesema atatoa leseni za kuanza kuchapishwa kwa magazeti ya MwanaHALISI, Tanzania Daima, Mseto na Mawio “Kifungo kimetosha. Kikubwa kazi iendelee,” amesema Nape.

"Agizo la Rais ni Sheria,leo nitatoa leseni kwa Mwanahalisi,Mawio,Mseto,Tanzania Daima ambayo yalikuwa yamefungiwa, tuanze kwa kufungua ukurasa mpya Ili tumalize kabisa jambo hili,kifungo kimetosha " Amesema Waziri Nape

======

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Leseni zitatolewa kwa Magazeti manne yaliyokuwa yamefungiwa. Magazeti hayo ni Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima

Ameeleza hayo Jijini Dar es Salaam leo Februari 10, 2022 katika Kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari na kusema, "Kifungo kimetosha"

Aidha, amesema Serikali inalenga kuboresha mahusiano kati yake na akieleza, "Rais ameelekeza kupitiwa #Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu zinazosimamia Sekta ya Habari na kuona namna ya kuzifanya ziwe rafiki na sio kikwazo katika shughuli za Wanahabari"

Amesema Serikali itatumia Bussra kuhakikisha mambo yanaenda sawa, na kwamba nia ya Serikali ya Awamu ya Sita ni njema hivyo watengeneze mahusiano na maridhiano mazuri, pia washikamane kwa pamoja

Ameongeza, "Najua tulipotoka, wakati mwingine safari ya mabadiliko sio rahisi na inaweza kuchukua muda. Inapochukua muda haimaanishi safari imesimama maana ni rahisi kutuhumiana kutosonga mbele. Wakati mwingine unasafiri unakwenda unakutana na jiwe, ukikutana na jiwe using'ang'anie kulipasua, rudi hatua moja nyuma nenda kushoto au kulia unaenda mbele. Ukirudi hatua moja haimaanishi umeamua kuacha safari, bali unatafuta njia nzuri ya kuendelea na safari"

Zaidi, soma: Gazeti la MwanaHALISI lafungiwa kwa miaka miwili, wahukumiwa kwa kuandika habari za uzushi kuhusu Mwakyembe na Makinikia

Samia atawale miaka mia 100✓
 
Wale waliofunga watalala na viatu kwa aibu🤣🤣🤣
 
Basi Mwanahalisi itaanza na madudu ya Makonda, Tanzania daima itakuwa inaweka yaliyojiri mahakani kesi ya mbowe na kifuatilia ugonjwa wa afande Swila

Ha ha ha
Huyu aliyepo aliponzwa na sakata la kumfuatilia aliyekuwa kinara wa himaya ya mzizima. aliandaa tume kumhoji baada ya kuvamia kituo sogozi na askali. lkn kabla ya kuweka wazi taarifa ya tume, akatumbuliwa usiku mmoja kabla ya kukamilisha kazi hiyo. sasa na yeye lazima afanye malipo au malipizi kwa huyo mtu.
 
Screenshot_20220210-115009.jpg
 
Kuna watu niliwamiss saaana kwa makala zao ambazo unasoma bila kuachia hadi mwisho, kuna zile taarifa za kipelelezi ulikuwa ni utamu mtupu; Nyaronyo Kicheere, Joster Mwangulumbi, Saed Kubenea, Majid Mjengwa, Chahali etc na sometime baba lao TUNDU ANTIPAS MUNG' WAI LISSU ni mwendo vitasa, angalau nitaanza kusoma magazet.
 
Back
Top Bottom