Serikali yayafungulia magazeti ya MwanaHALISI, Tanzania Daima na Mseto

Huyu ndiye alikuwa Kiherehere cha kufanya uchafu wote ule , huyu alishirikiana na kundi lake kuhujumu kila vyombo vya habari vilivyokuwa tofauti na matakwa ya aliyemtuma , huyu alichangia kuficha kila habari kuhusu chochote ikiwemo Corona .

Ni lazima huyu ajadiliwe hapa ili labda atajitokeza na kuwataja wote waliokuwa wanamtuma , walio hai na Waliokufa , hatuwezi kuwa na viongozi kwenye utumishi wa Umma wenye makandokando kama ya Dr Abbas .Ajiuzulu arudi mitaani ajifunze uungwana .

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO
 
Agizo la Rais siyo sheria!!

Inatisha kuona kiongozi serikalini akisema agizo la Rais ni sheria.

Banana republic stuff.
Tumezoea sana kufanyia kazi mawazo, maoni, ushauri, karipio nk! Banana republic and a half!!
 
Kweli kabisa mkuu,nilisitisha kabisa kununua magazeti!Lakini sasa nitanunua.Maana yale wasiyopenda yaandikwe yataandikwa.Tunataka kujua ukweli au hata kuona mtu/chombo kinahoji juu ya mambo magumu kama Nani alimpiga risasi Tundu,nini kilitokea juu ya miili ya watu waliokuwa wanaokotwa baharini/mitoni?Ni kweli inspector Swila anaumwa? Ilikuwaje "covid 19" wakaingia bungeni? Vyombo vya habari vya kawaida vimeshindwa kuhoji mambo haya
 
Samia atawale miaka mia 100✓
 
Wale waliofunga watalala na viatu kwa aibu🤣🤣🤣
 
Basi Mwanahalisi itaanza na madudu ya Makonda, Tanzania daima itakuwa inaweka yaliyojiri mahakani kesi ya mbowe na kifuatilia ugonjwa wa afande Swila

Ha ha ha
Huyu aliyepo aliponzwa na sakata la kumfuatilia aliyekuwa kinara wa himaya ya mzizima. aliandaa tume kumhoji baada ya kuvamia kituo sogozi na askali. lkn kabla ya kuweka wazi taarifa ya tume, akatumbuliwa usiku mmoja kabla ya kukamilisha kazi hiyo. sasa na yeye lazima afanye malipo au malipizi kwa huyo mtu.
 
Kuna watu niliwamiss saaana kwa makala zao ambazo unasoma bila kuachia hadi mwisho, kuna zile taarifa za kipelelezi ulikuwa ni utamu mtupu; Nyaronyo Kicheere, Joster Mwangulumbi, Saed Kubenea, Majid Mjengwa, Chahali etc na sometime baba lao TUNDU ANTIPAS MUNG' WAI LISSU ni mwendo vitasa, angalau nitaanza kusoma magazet.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…