Pre GE2025 Shabiby: Mkipewa Uwaziri mnaanza kuweka mipango ya kuwa Rais

Pre GE2025 Shabiby: Mkipewa Uwaziri mnaanza kuweka mipango ya kuwa Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
..Shabiby anazungumza utadhani nchi yetu ni mali ya Raisi.

..kinachosikitisha na kutia aibu ametoa kauli hizo ktk mkutano wa hadhara.
Mkuu hivi unaweza kuwaonea aibu watanzania ambao ni mithili ya robot?watanzania hawahawa ambao serikali inajenga choo cha shule halafu wanafurahi mpaka wanalia?watanzania hawahawa ambao kila raisi anaekuja wanaambiwa ni chaguo la Mungu?
 
Waziri ana nafasi ya ubunge kama mwakilishi wa wananchi na nafasi ya uwaziri ambaoe kutekeleza maagizo ya Raisi katika Wizari yake ya kuhakikisha miradi inayokwenda kwa wananchi inakamilika hivyo mbunge wa Gairo kwa kauli
yake yupo sahihi.
 
Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby amesema “Ubaya wenu nyie mawaziri mkishapewa Uwaziri mnajiona mnaweza kuwa Rais, naacha kazi za Uwaziri mnaanza mipango ya kuwa mtakuwaje Rais, mnasahau aliyekuteua amefanya hivyo ili ufanye kazi zake akupende, umtumikie yeye.”

Amesema hayo katika mkutano na Wananchi Wilayani Gairo wakati wa ziara ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Tunayetakiwa kumtumikia wa kwanza ni Rais halafu wanakuja watu wengine, lakini mnajisahau, kuna mawaziri nawajua, wameshamaliza vikao vyote wamebakiza Mabalozi wa nyumba 10.

Usicheze na mtu aliyeshika mpini, aliyeshika mpini ni Rais ambaye ndiye huyohuyo Mwenyekiti wa Chama.

View attachment 3051075
Naomba kuuliza, hivi watu kama kina Shabiby miaka nenda rudi huwa ni wabunge, je, wao huwa hawautaki uwaziri au hawana vigezo?
 
Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby amesema “Ubaya wenu nyie mawaziri mkishapewa Uwaziri mnajiona mnaweza kuwa Rais, naacha kazi za Uwaziri mnaanza mipango ya kuwa mtakuwaje Rais, mnasahau aliyekuteua amefanya hivyo ili ufanye kazi zake akupende, umtumikie yeye.”

Amesema hayo katika mkutano na Wananchi Wilayani Gairo wakati wa ziara ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Tunayetakiwa kumtumikia wa kwanza ni Rais halafu wanakuja watu wengine, lakini mnajisahau, kuna mawaziri nawajua, wameshamaliza vikao vyote wamebakiza Mabalozi wa nyumba 10.

Usicheze na mtu aliyeshika mpini, aliyeshika mpini ni Rais ambaye ndiye huyohuyo Mwenyekiti wa Chama.

View attachment 3051075
Ama kweli kumekucha jmn
Kumbe haya mambo ni serious kiasi hiki
 
Back
Top Bottom