Pre GE2025 Shabiby: Mkipewa Uwaziri mnaanza kuweka mipango ya kuwa Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
..Shabiby anazungumza utadhani nchi yetu ni mali ya Raisi.

..kinachosikitisha na kutia aibu ametoa kauli hizo ktk mkutano wa hadhara.
Mkuu hivi unaweza kuwaonea aibu watanzania ambao ni mithili ya robot?watanzania hawahawa ambao serikali inajenga choo cha shule halafu wanafurahi mpaka wanalia?watanzania hawahawa ambao kila raisi anaekuja wanaambiwa ni chaguo la Mungu?
 
Waziri ana nafasi ya ubunge kama mwakilishi wa wananchi na nafasi ya uwaziri ambaoe kutekeleza maagizo ya Raisi katika Wizari yake ya kuhakikisha miradi inayokwenda kwa wananchi inakamilika hivyo mbunge wa Gairo kwa kauli
yake yupo sahihi.
 
Naomba kuuliza, hivi watu kama kina Shabiby miaka nenda rudi huwa ni wabunge, je, wao huwa hawautaki uwaziri au hawana vigezo?
 
Ama kweli kumekucha jmn
Kumbe haya mambo ni serious kiasi hiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…