Yaani hapo tayari keshachambua mpira!! Mimi ningetarajia atuchambulie takwimu zilizijiri katika mechi ya kwanza hapa Dar, halafu azitumie kutuambia ni kwa namna gani Orlando ni wazuri kuliko Simba.
Ukweli ni kwamba achilia matokeo baina yao kwenye mechi, takwimu za mchezo huo hazikuonesha makali yoyote ya timu hiyo hata kuipa nafasi ya kusonga mbele. Ilizidiwa karibu maeneo yote!! Kamaq itasonga mbele si kwa sababu yenyewe ni bora zaidi, bali ni matokeo tu kuwa upande wao!! Ubora wa timu huonekana kwenye btakwimu za mchezo na si vinginevyo!!
Kama Simba itasonga mbele Shafii atasema "mimi sikusema hatasonga mbele bali nilisema hatabeba ubingwa wa Confederation cup"!! Kama isiposonga mbele atasema "si nilisema, hapo hakuna kitu" Ikitokea Simba ikabeba kombe la CAF atasema " mimi nilisema hawezi kubeba ubingwa wa Africa yaani champions league". Hawa ni wambeya wa soka hitaji lao kubwa ni kuganga njaa!! Ukimpa buku anakusema vizuri nk!!