Hilo ni dua la kuku, Kamwe mwewe kumpataAliyasema kaburu, kule Afrika Kusini,
Kuja nyie kuwa huru, yafuteni akilini!
Hata nyie makimburu, makwenu ni jalalani!
Alikotoka Kabundi, hakika mtarajea!
Hilo ni dua la kuku, Kamwe mwewe kumpata
Ikulu ni marufuku,Tusipakane mafuta,
Kweli mnayo shauku,yalojengwa kuyafuta,
Hamtapata kitu Ng'o,mtakaa msubiri.
Malenga acha utani, eti na Mbowe ni Simba!
Ni simba katika nini, hebu nieleze mwamba,
Simba alianza lini, au bure wampamba,
Mbowe akiwa simba, simba watakuwa nini?
Kama ni kwenye siasa, nadhani wamuonea,
Wauhitaji msasa, ujifunze kuongea,
Kisiasa Mbowe tasa, karibu tatokomea,
Mbowe akiwa simba ,simba watakuwa nini?
Ukisema Mbowe mbuzi, unayo sapoti yangu,
Hili liko wazi wazi, japo litie utungu,
Namna alivyonasa, apitwa na nungunungu,
Mbowe akiwa simba, simba watakuwa nini?
Mshindi hatutafuti,ya nchi tunayajengaKuwa nimekuwa kimya, si kwa kuwa umeshinda,
Huhitajika mayaya, vyote huanza makinda,
Mmekalia ubaya, siasa siyo ununda!
Shingo mlivyoshupaza, hekima yenu i wapi?
Hekima yenu i wapi, hii nchi yetu sote,
Mnang'ang'nia kipi, hapa mbona kwetu wote,
Mmekuwa wafupi, kutoona pande zote,
Shingo mlivyoshupaza, hekima yenu i wapi?
Mkuu pesa is nothing, ukinzani wa kifikra una baraka za Mungu....yaani nachelea kusema ni law nature. CHADEMA ni taasisi iliyo katika hiyo law. CCM ni chama mfu!Umaja wa Ulaya huchangia Bajeti ya Tanzania na moja ya mashariti yao makubwa ni razima bunge liwe na vyama vya upinzani ndiyo maana Ndungai kuwanunua covid 19 kienyeji kwa njia haramu za kishetani akiamini uwepo wao Bungeni utawasaidia kupata pesa za misaada toka ulaya
Mshindi hatutafuti,ya nchi tunayajenga
Wote sisi dikuruti,wanafunzi wa malenga
Lengo si kupiga shuti,wala lengo si kupinga
Shingo zetu zi laini,shida yenu wakorofi.
Hekima yetu amani,nchi kuweka pazuri
Kung'ang'a sasa nini,kwetu sote ninakiri
Twaona hadi kusini,pande zote tu mahiri
Shingo zetu zi laini,shida yenu wakorofi.
Mliwahi kusikia, wito wa maridhiano?
Mliwahi zingatia, tuone si mashindano?
Kukata watu mikia, mhodhi vyote vinono,
Sikizeni toka kwetu, kujiona hamuwezi,
Yalimshinda tumbili, hakuliona la kwake,
Tusemayo ni kamili, twawaona kwa makeke!
Huitafuta halali, siyo kwa maneno yake!
Mwuungwana sikiliza, huwezi wewe jiona!
Mliwahi kusikia, wito wa maridhiano?
Mliwahi zingatia, tuone si mashindano?
Kukata watu mikia, mhodhi vyote vinono,
Sikizeni toka kwetu, kujiona hamuwezi,
Yalimshinda tumbili, hakuliona la kwake,
Tusemayo ni kamili, twawaona kwa makeke!
Huitafuta halali, siyo kwa maneno yake!
Mwuungwana sikiliza, huwezi wewe jion
Kaka ninakusalimu ,salaaam alaykumuKwani kuna shida gani, maridhiano na nani ?
Ushindi ni wa tufani,mwataka mpewe nini,
Mkakae mashambani,mzalishe ya tumboni,
Acheni kutaka dezo,Mmeshindwa tulieni
Acheni kutaka dezo, mmeshindwa tulieni
Siasa siyo mchezo,ni kazi ya kiumeni
Hatutaki matatizo,Nyie kwanza pataneni
Bila kujirekebisha,mtaishia kunawa.
Kwani kuna shida gani, maridhiano na nani ?
Ushindi ni wa tufani,mwataka mpewe nini,
Mkakae mashambani,mzalishe ya tumboni,
Acheni kutaka dezo,Mmeshindwa tulieni
Acheni kutaka dezo, mmeshindwa tulieni
Siasa siyo mchezo,ni kazi ya kiumeni
Hatutaki matatizo,Nyie kwanza pataneni
Bila kujirekebisha,mtaishia kunawa.
Beti umeparanganya,hauna muelekeo,Hatafutwi mshinda, yalikuwa ni ya nani,
Mara tena mmeshinda, eti nao wa tufani?
Kura zenu za kusunda, na kubeba mabegini?
Yakumbuke usemayo, siyo kuwa mbayuwayu,
Ya shingo kuwa laini, yalikuwa nayo yako,
Iingie akilini, haya pia ni ya kwako?
Ukiingia vitani, tumia risasi zako,
Yakumbuke usemayo, siyo kuwa mbayuwayu,
Umeshindwa kukumbuka, ulisema ya kupewa?
Ni kwa vipi tutafika, mafuta umeishiwa,
Mara useme haka, mara huyu mara hawa,
Yakumbuke usemayo, siyo kuwa mbayuwayu,
Kaka ninakusalimu ,salaaam alaykumu
Mimbari hii muhimu,Sasa iwe ya kudumu
Malumbano ni matamu,Yanatupa ufahamu
Siasa hujenga mwili,tunatoa ya moyoni
Beti umeparanganya,hauna muelekeo,
Mambo umeyachanganya,umekabwa koromeo?
Umechoka kudanganya,usiku hadi machweo
Watu waongo waongo,Haram kuridhiana.
Waalike huko bara , hili jambo la muhimuAlaykum Salamu, zimenifika kwa simu,
Naafiki ni muhimu, kulifanya la kudumu,
Kurumbana bila damu, si ndiyo ubinadamu?
Wapo wengi watalamu, kwa hakika litanoga!
Waalike huko bara , hili jambo la muhimu
Visiwani tutafura,kwa vina vilo vitamu
Na hii si biashara,ni kujenga ufahamu,
Siasa hujenga mwili,tunatoa ya moyoni.
Wallahi nimefurahi,haijapata tokeaWabara tuko imara, kumbukumbu na mantiki,
Siyo siasa uchwara, kwenye haki hatutoki,
Wala huu si mkwara, janja janja hatutaki,
Tujadili ya nchini, siasa huchangamsha!
Mengi yamekwishapita, jahazi lasonga mbele,
Kwa staha tumepita, kimya pasipo kelele,
Ya nini kusita sita, enyi malenga wa kale,
Tujadili ya nchini, siasa huchangamsha!
Siasa huchangamsha, tujadili ya nchini,
Wepesi watachemsha, wabaki wale makini,
Hii siyo kujichosha, na matusi ya wahuni,
Tujadili ya nchini, siasa huchangamsha!
Pana chaguzi zimepita, na mazagazaga yake,
Pana hata za ukuta, vuguvugu za makeke,
Pana waliojikita, ni hadi kieleweke,
Tujadili ya nchini, siasa huchangamsha!
Mheshimiwa missile,usitue peni chini,
Senzige wa zenji kule, uongezee watani,
Ukomavu ule ule, haki iwepo nchini,
Tujadili ya nchini, siasa huchangamsha!
Tunao magwiji wengi, wakiwamo wenda kimya,
Yupo Makanyaga Kingi, mfalme wa kule mbeya,
Yupo binti yake mangi, Lowassa bingwa wa kaya,
Tujadili ya nchini, siasa huchangamsha!
Hapa niongeze nini, Senzige kumuuitika?
Hata bila kalimani, wamwelewa huyu kaka,
Ya siasa tuyaghani, tukisaka miafaka,
Nimefikisha ujumbe, na mjumbe hauwawi!
Wallahi nimefurahi,haijapata tokea
Na tena niwasabahi,wale mtaitikia
Si Pemba wala si Bahi ,Mola atajaalia
Mwito wa Brazajei,ufike mikoa yote.
Mwito mtaoitika,muandike yenye tija
Wengi watanufaika,na kuwatia faraja
Muandike ya hakika,yalo mema kuyataja
Mwito wa Brazajei,ufike mikoa yote.
Mawaziri nawajua,walokuwepo zamaniAlisema Museveni, hatosubiri karamoja,
Ya kuwa sisi twendeni, bila shaka watakuja,
Watukutie njiani, tutasafiri pamoja,
Kwa kipyenga cha Senzige,Jahazi nanga twang'oa.
Jahazi nanga twang'oa, tunayo mengi mezani,
Una ya kukokotoa, ya red u kitanzini,
Mawaziri alotoa, awajua visiwani?
Kwa kipyenga cha Senzige, tayari tumeshang'oa.
Kama namba mtasoma, kama tusomavyo sisi,
Awamu hii ya neema, labda kwa makasisi,
Kanda yetu ya Musoma, pia pande za busisi!
Kwa kipyenga cha Senzige, Tunayeya safarini.
cc: missile-of-the-nation, Makanyaga,
Jane Lowassa, father-of-all
Mawaziri nawajua,walokuwepo zamani
Wapya sijawajua,itawapima mizani
Wakishindwa kutatua, tutawaacha gizani
Tumepuliza kipenga,Mje tujenge kwa vina,
Brazajei wasikia,kumekucha visiwani
Weshatia yao nia,Kiapo serikani
Mambo wameyaridhia,wazalendo karibuni
Hussein amewaita,nao wameitikia