Shairi: Aikael Mbowe, Freeman Mwamba wa Tanzania

Nusu mbili zimekwisha, rasmi sasa u punga,
Vina unasahihisha, kwa 'scheme' ya kuvunga?
Kama ndiko kujishasha, ni sawia na kudanga!
Buku saba yote kwisha, sasa washindwe wenyewe!
Tumewapeleka EDA,mitano mtasubiri
Mtapoteza makada,mtaionja shuburi
Watahama makamanda,sisi tutawasitiri
Duri na dawiri zari,Tuipambe CCM.
 
Tumewapeleka EDA,mitano mtasubiri
Mtapoteza makada,mtaionja shuburi
Watahama makamanda,sisi tutawasitiri
Duri na dawiri zari,Tuipambe CCM.

Mitano yote ya wizi, vya halali mwaviweza?
Kwamba nyie ni mijizi, bado mwajisifu faza?
Kwamba ni majamba-wazi, nini cha kujipongeza?
Shubiri ionjwe vipi, kwetu tunajitolea!
 
Mitano yote ya wizi, vya halali mwaviweza?
Kwamba nyie ni mijizi, bado mwajisifu faza?
Kwamba ni majamba-wazi, nini cha kujipongeza?
Shubiri ionjwe vipi, kwetu tunajitolea!
Nani amewaibia,sera zenu ndiyo mbovu
Vurugu kwenu tabia,mnahusudu maovu
Lissu kawaharibia,kwa siasa mbovumbovu
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM
 
Nani amewaibia,sera zenu ndiyo mbovu
Vurugu kwenu tabia,mnahusudu maovu
Lissu kawaharibia,kwa siasa mbovumbovu
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM

Uliwahi kusikia, mwizi kakiri kuiba?
Akiweza kukimbia, hukomaa kama Luba!
Kwamba tulisinzia, kutoona mkiiba?
Lissu amewaumbua, ni bora mkachutama!
 
Acheni kulalamika,mwende mjitafajari
Msome kuelimika,siasa zisizo shari
Mje mmekamilika,tujenge nchi ya heri
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM
 
Acheni kulalamika,mwende mjitafajari
Msome kuelimika,siasa zisizo shari
Mje mmekamilika,tujenge nchi ya heri
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM

Acheni kujidanganya, nchi mmeichafua,
T-zedi kilichanganya, Dunia ika tambua,
Itakuwa kudanganya, kwamba hapa tunakua!
Duniani tunanuka, tuna vibaka wa kura!
 
Silabi hazitoshi kwenye kibwagizo "Hongera sana Mbowe, ........." Silabi moja inapungua. Kibadilishe kibwagizo chako kiwe hivi: Hongera sana e Mbowe, wewe ni mtu makini"
Na mimi pia niliwahi kusoma Kiswahili, lol!
 
Acheni kujidanganya, nchi mmeichafua,
T-zedi ilichanganya, Dunia ili tambua,
Itakuwa kudanganya, kwamba tunakua!
Duniani tunanuka, tuna vibaka wa kura!
Nchi inasonga mbele,macho yenu makengeza,
Mtaumia milele,vyote mtavipoteza
Tanzania inogile,watakuja kututuza,
Duri na dawiri zari,Tuipambe CCM
 
Silabi hazitoshi kwenye kibwagizo "Hongera sana Mbowe, ........." Silabi moja inapungua. Kibadilishe kibwagizo chako kiwe hivi: Hongera sana e Mbowe, wewe ni mtu makini"
Na mimi pia niliwahi kusoma Kiswahili, lol!

Alijikwaa malenga, uzuri hakuanguka,
Kwamba hakuweza lenga, ni gwiji huyu kumbuka!
Beti saba kazipanga, kwa hakika mtukuka,
Mizani iliyo paa, haimkwepi kombora!

Cc: missile-of-the-nation
 
Mbowe kawahenyesha CCM miaka kwa miaka hadi wakaanza kushambulia mali zake!!

Mwamba wa siasa za Tanzania.
 
Nchi inasonga mbele,macho yenu makengeza,
Mtaumia milele,vyote mtavipoteza
Tanzania inogile,watakuja kututuza,
Duri na dawiri zari,Tuipambe CCM

Mbona kote ni kusonga, wende hasi au chanya?
Kwamba dereva mjinga, si full kujichaganya?
Ajuwe wapi kupanga, sembuse hata kufanya?
Kote kweli ni kusonga, hata kama Wenda hasi!
 
Mbona kote ni kusonga, wende hasi au chanya?
Kwamba dereva mjinga, si full kujichaganya?
Ajuwe wapi kupanga, sembuse hata kufanya?
Kote kweli ni kusonga, hata kama Wenda hasi!
Umetisha ile mbaya!! ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘
 
Mbona kote ni kusonga, wende hasi au chanya?
Kwamba dereva mjinga, si full kujichaganya?
Ajuwe wapi kupanga, sembuse hata kufanya?
Kote kweli ni kusonga, hata kama Wenda hasi!
Sisi tunasonga chanya,nyinyi mnakuja hasi
Makubwa tunayafanya,tunaenda mwendo kasi,
Si Bukombe si Makanya,kote huko kwetu sisi
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM.
 
Sisi tunasonga chanya,nyinyi mnakuja hasi
Makubwa tunayafanya,tunaenda mwendo kasi,
Si Bukombe si Makanya,kote huko kwetu sisi
Duri na dawiri zari,tuipambe CCM.

Senzighe nyumbani wapi, Chatto au usukuma?
Makubwa hayo ni kupi, Au kwenye lile chama?
Kipaumbele ni kipi, ndege au wakulima?
Haya ya vyuma kukaza, leo ndiyo kusikia?
 
Wanawake mashoka unaowaona hapa ni kwasababu walipewa nafasi na CHADEMA hapa sitosema Chama chetu kinakandamiza Wanawake, kina Mfumo Dume, tupo hapa kwasababu tulipewa nafasi, Halima Mdee yupo hapa kwakuwa alijengwa, changamoto zinakuwepo ili zitatuliweโ€ -Mzee MDEE

Nakala ifike kwa Job Ndugai.
 
Ni Sawa! mtizamo wako but huwezi kutudanganya! Tunataka maendeleo,tunataka Amani
 
Senzighe nyumbani wapi, Chatto au usukuma?
Makubwa hayo ni kupi, Au kwenye lile chama?
Kipaumbele ni kipi, ndege au wakulima?
Haya ya vyuma kukaza, leo ndiyo kusikia?

Senzighe nyumbani wapi, Chatto au usukuma?
Makubwa hayo ni kupi, Au kwenye lile chama?
Kipaumbele ni kipi, ndege au wakulima?
Haya ya vyuma kukaza, leo ndiyo kusikia?
Kwangu mimi ni Unguja,Nyumbani kwao Hussein
Hata bara ninakuja,kuongea ya chamani
Tunapanga yenye tija,vyote ndani ya ilani
Siraaj ng'aza siraati,tuondokwe na ghururi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ