Shaka Hamdu Shaka: Tumepunguza ada ya usajili wa "Online TV" kwa 95% kutoka TZS 1M hadi shilingi Elfu 50

Shaka Hamdu Shaka: Tumepunguza ada ya usajili wa "Online TV" kwa 95% kutoka TZS 1M hadi shilingi Elfu 50

photo_2022-04-21_09-01-24.jpg
 
View attachment 2193845
===
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi & Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka amempongeza Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na kifua cha kuvumilia kukosoa na kukosolewa.

Aidha Ndg Shaka Hamdu Shaka amempongeza zaidi Rais pamoja na Waziri aliyemteua Mhe Nape Moses Nauye kwa kushusha gharama za kusajili "Online TV" kutoka TZS 1,000,000 ( milioni moja) ya awamu iliyopita hadi TZS 50,000 ( elfu hamsini ) ya sasa kwa kutambua kuwa kwasasa duniani " Mitandao ni Ajira".

Wakati huohuo,
Amempongeza sana Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Pamoja na Waziri Nape Moses Nauye kwa kuvifungulia vyombo mbalimbali vya Habari vilivyofungiwa kwa muda mrefu kwani Vimerudisha ajira kwa Watanzania wanyonge na vimeongeza wigo wa kupata habari na wanahabari.

Aidha, Shaka Hamdu Shaka ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita kwa kutekeleza kisawasa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020|25 hasa kifungu cha 125,kinachosisitiza Uhuru wa habari na wanahabari kwa WATANZANIA wote "Na ndio sababu leo watu wanakosoa na wanabaki kuwa salama " alilisisitiza bwana Shaka Hamdu Shaka.

Ndg Shaka Hamdu Shaka ameyasema hayo katika Uzinduzi wa Jengo la Studio za kisasa za Televisheni ya TBC2 pamoja na kipindi kipya cha "Jambo Tanzania", Mikocheni Jijini Dar es Salaam Jumanne 19 Aprili, 2022.
Hongera sana Ndg Shaka Hamdu Shaka,

Unafanya Kazi nzuri sana katika Taifa hili,


Appreciated 🙏🙏🙏🙏
 
Je nyinyi wapiga mapambio mnaupiga mwingi majumbani kwenu?

Hivi ni ukosefu wa ajira ndio unawaletea UCHAWA au Njaa iliyopitiliza?
 
Mbio za Panya

Wafuasi wa Lumumba mm hapo ndio huwa siwaelewi... Yaani tozo ya awali mliweka nyie(Mkashangilia),,Leo tena nyie wenyewe mmeifuta(Mnashangilia)... as if kuna kitu kipya mmeongeza..

Mnatengeneza tatizo,, halafu mnalitatua.. then mnajiona Wakombozi...


Mtazamo tu...

Hao ccm ndio wale " mmeshiba ndio, mnanjaa ndio"
 
Ilani yao ndio inatekelezwa.... waliahidi kujenga mazingira rafiki na wezeshi kwa ustawi wa tehama ili iajiri watu wengi zaidi ndicho kilichotokea....sasa unawaondoleaje pongezi...ikiwa wameahidi na kutekeleza!!!

Walioweka milioni moja walikuwa wanatekeleza nini? Mmeona hakuna mtu anawashobokea ndio mkaona isiwe tabu acha mshushe bei.
 
Je nyinyi wapiga mapambio mnaupiga mwingi majumbani kwenu?

Hivi ni ukosefu wa ajira ndio unawaletea UCHAWA au Njaa iliyopitiliza?

Naona sukuma gang Msoga line wanakutesa vibaya! Safari hii mabush star kazi mnayo kwa maborn town.
 
Hapana Mkuu,, hakuna ubaya wowote kwa kilichofanyika....

Nilichosema ni kwamba aliyeweka watu walipe Millioni Moja,, ndio leo aliyetoa na kubaki Elfu hamsini..

Nani wa kusifiwa hapo na ni nani wa kumchukia..???
😍😍🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom