Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi

Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
"Shambulizi la Lissu, wanaomdhania dereva anahusika, sio wajinga!, wana hoja za msingi!" Swali ni Jee Dereva Anahusika?

Si maanishi kuwa dereva wa Lissu anahusika, bali mazingira ya tukio, yanahalalisha watu wenye udadisi kujiuliza maswali kihusu tukio lenyewe, hivyo kuhisi uhusika wa dereva wa Lissu, sio jambo la ajabu, tena uhusika wenyewe sio lazima uwe expressly but impliedly kwa negligence iliyopelekea Lissu kuwa reached na watu wasiojulikana na kushambuliwa, wakati alikuwa na uwezo wa kumuepusha na shambulizi hili.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
JE, DEREVA WANGU AMEFICHWA WAPI???
Kuna wajinga wanaoelekea wametumwa na 'watu wasiojulikana' kueneza maneno ya kijinga kwamba dereva wangu anafahamu siri za kushambuliwa kwangu. Kwamba alitoroshwa na sasa amefichwa na CHADEMA na Mwenyekiti Mbowe, n.k.

Nimekuwa na dereva huyu tangu mwaka 2002, akiwa kijana wa miaka 19. Katika miaka yote hii, amekuwa ni sehemu ya familia yetu. Ninamfahamu fika. Ninafahamu alivyo mwaminifu kwangu. Hawezi na asingeweza kufahamu njama za kuniua mimi halafu asiniambie. Mara baada ya kushambuliwa kwangu, 'watu wasiojulikana' walianzisha minong'ono ya chini chini kwamba wakimpata dereva wangu basi 'wamemaliza maneno' juu ya kushambuliwa kwangu.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka?, halafu what happened?!. Kwenye mambo ya assignment, anaweza hata akatumika mke wako aliyekuzalia wanao, sembuse itakuwa dereva tuu mliotoka nae mbali!.
Baadhi ya maswali ni haya...
  1. Kwa vile Lissu aliwahi kuripoti kufuatiliwa, kupitia press conference, kwa nini hakuripoti polisi?!.
  2. Baada ya Chadema kupokea taarifa ya Mnadhimu wake kufuatiliwa, walichukua hatua gani?.
  3. Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.
  4. The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.
  5. Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
  6. Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.
  7. Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.
  8. Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
  9. Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.
  10. (Mimi niliwahi kuwa mwanajeshi wa JWTZ hivyo kuna kitu nakijua kuhusu hizi AK47 ndani ya jeshi letu, lakini vitu vingine ni siri za usalama wa taifa letu, sina uhakika mtu asiyepitia JWTZ, ana uwezo gani kuijua AK 47!.)
  11. Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
  12. Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.
  13. Maswali haya yameendelea kwa msaada wa mwana jf huyu
  14. Hata kama wangemuhoji huko Nairobi au Ubeligiji angesema hayo hayo ambayo amekuwa akiyasema kwenye social media na vyombo vingine vya habari kila mara ambayo hayana msaada wo wote wa kuwanasa hao assailant wake.
    [*]Kwa dalili zo zote dreva wake ni suspect number one.
  15. Bunduki iliyotumika waliiona ni AK 47 iliyokuwa na full magazine (risasi 40) ambayo ilimimina risasi zote 40 at close range. Kati ya hizo 17 zilizama kwenye miguu, mikono na kiuno cha Tundu Lissu.
  16. Risasi zilimiminwa kutoka upande wa kulia wa gari ambao ni upande wa dreva lakini dreva hakupatwa na risasi hata moja na alipata hata fursa ya kuteremka kwenye gari na kwenda ku take cover kwenye magari yaliyokuwa yamepaki eneo hilo. Assailants walikuwa upande wa kulia wa gari, hivyo risasi zilizama zaidi kwenye mguu wa kulia, paja la kulia, mkono wa kulia, kiuno upande wa kulia na kutokea tumboni na mkono wa kushoto. These are the documented medical forensic clues.
  17. Majeshi yetu hayana bunduki za AK 47, yana SMG badala yake ambayzo full magazine zake ni risasi 30. Bunduki za AK47 zinamilikiwa na majambazi yanazozipata kutoka kwa wanajeshi wa Burundi wanaokimbilia Tanzania ambao huwa wanaziuza kwa bei ya shillingi 20,000 tu!! Silaha hizi ndizo zilitikisa huko Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
  18. Hakuna mwanajeshi ye yote (aliyepata mafunzo ya kijeshi) ambaye ampige mtu (adui) risasi 38 from an AK 47 gun at a close range halafu mtu huyo asalimike!! Never on earth. Kwanza atahitaji risasi moja tu na atafumua kichwa au moyo. Hivyo it is so obvious kwamba assailants wa Tundu Lissu walikuwa ni wahuni tu wa mitaani wasiojua kutumia bunduki. Yaani risasi 38 zote zinakosa target (kichwa au moyo) zinaishia kupiga makalio na hewa!! Hili halihitaji askari wa Scotland yard kulitambua. Swali ni nani aliwakodi hawa wahuni wasiojua shabaha? Kwa nini dreva wa Lissu akawa mkimbizi nchi za nje? Nini kakimbia? Kwani hata polisi wetu wakienda kumhoji huko kwani atasema lo lote la maana? Huko hawawezi kumu arrest. Alipaswa kuwa behind bars ili aeleze vizuri. Tundu Lissu alipaswa kujua hili. Mara nyingi kikulacho unacho nguoni mwako. Eti ninamuamini sana. Mbele ya pesa kunakuamini mtu? Yaani apewe shillingi million 500 aache kukumaliza? Yaani Tundu Lissu hajui kwamba "Money is the source of all evils in this world?"
  19. Hospitali ya serikali ya Dodoma na madaktari wa serikali wa Dodoma hospital ndiyo waliookoa maisha yake. Kama serikali ilikuwa na mpango wa kumuua, ingalishindwaje kumumalizia hapo hapo kwenye hospitali yake ya Dodoma humo humo operation theatre? It was so simple eg hiyo damu aliyopewa hangeipata au angalipewa incompatible blood ambayo ingalimumaliza hapo kwa hapo! Lazima aishukuru serikali kwa kuokoa maisha yake badala ya kuilaumu. Upinzani haupaswi kuwa wa aina hii. Tujifunze kwenye nchi zilizotutangulia.
  20. Bunduki kama AK 47 au SMG ikiunguruma si mchezo. Kwa askari yo yote trained, hata kama naye ana bunduki ya aina hiyo hiyo lakini kashutikizwa, reaction ya kwanza ni ku take cover. Atalala chini na ku craw hadi mahala salama. Hapo ndipo atatafuta kuona adui/ maadui walipo na kutafakari kama anao uwezo wa kupambana nao au kuomba reinfocement au kutokomea kabisa kwenye eneo hilo. Trained soldier hakurupuki tu kuanza kurusha risasi ovyo ovyo anapositukizwa na milio ya risasi. Hivyo kwa jinsi tukio lilivyotokea hapo usingalitarajia askari waliokuwa karibu na eneo hilo kuwa wangaliweza kuanza kujibu mapigo kwa muda huo mfupi uliotumika kabla ya majambazi hayo kutokomea kusikojulikana. Dreva wa Lissu aliyaona live na alitaja hata aina ya gari yalilotumia na plate namba zake. Polisi walikamata magari kadhaa ya aina hiyo lakini dreva huyo alikataa kwenda kuyatambua na hivyo yakabidi yaachiwe kwani hakuna shahidi aliyejitokeza. Shahidi muhimu alikuwa Nairobi akidaiwa anapata tiba ya kisaikolojia. Sasa hivi Lissu anasema dreva huyo yuko masomoni Ubeligiji. Sijui anasoma digrii gani hapo Leuven University teaching hospital anapotibiwa boss wake. Jamani aacheni kutufanya wajinga. Pascal yuko sahihi kabisa.
  21. Huko nyuma niliisha wahi kuzungumza haya kuhusu dereva wa Lissu.
Wanabodi,
Angalizo: Hili ni bandiko la swali kuwa Jee dereva wa Mhe. Tundu Lissu atatiwa mbaroni jijini Nairobi na kuletwa nchini kuhojiwa kuhusu shambulio la Lissu?.

Nimesoma taarifa hii ya IGP Simon Sirro kuhusu kutumwa kwa makachero wawili wa Jeshi letu la polisi kwenda jijini Nairobi kumhoji Lissu na dereva wake kuhusiana na shambulizi la Lissu.

Taarifa yenyewe ni hii

Jeshi La Polisi Linastahili Pongezi, Kwa Kuwa Jeshi Rafiki Kuliko Polisi Wote Duniani!.

Kumbe siku hizi, polisi wetu wakitaka kufanya uchunguzi wa kijinai, huwa wanasubiri kwanza ruhusu ya wahusika, ndipo wafanye uchunguzi, shambulizi la Lissu limetokea miezi Zaidi ya mitatu imepita bila taarifa zozote za uchunguzi wa tukio hilo, IGP Sirro anasema mwanzo waliwaomba Chadema, wakakataa!, kumbe uchunguzi wa kijinai siku hizi watu wanaombwa kuhojiwa, ukitaa hauhojiwi, lakini sasa Chadema wamesema wako tayari, hivyo ndia sasa watu wametumwa kwenda kuhoji!. Inawezekana polisi wetu ndio the most friendly police force dunia nzima!. Uhalifu ufanyike, tena jinai ya kutishia maisha ya mtu, Tanzania na Kenye tuna mkataba wa ushirikiano kwenye uhalifu, polisi wetu walishindwa nini kumhoji dereva wa Lissu huko huko Nairobi siku zote hizi?!, kumbe walikuwa wanasubiri ruhusa ya Chadema!. Big up sana kwa polisi wetu.

Makachero Wawili ni Kufanya Mahojiano Tuu, au ...
Japo taarifa inaeleza kinachokwenda kufanywa na makachero hao ni mahojiano tuu, lakini kwa sisi wasoma trends za in between the lines za taarifa hii, atakayefanyiwa mahojiano Nairobi ni Mhe.Tundu Lissu tuu, lakini dereva wake anapaswa kutiwa mbaroni huko Nairobi na kurejeshwa nchini kama mhalifu kuja kuhojiwa nyumbani.

Dereva Atahojiwa Nairobi au Atarejeshwa Nchini Kuhojiwa Nyumbani?.
Kitakacholitia nguvu jeshi la polisi kumtia mbaroni dereva wa Lissu, ni sababu zile zilizotolewa na Chadema kwa nini dereva huyo amefichwa Nairobi, ni kwa sababu ya usalama wake kufuatia ndiye mtu pekee aliyewaona wauaji kwa sura, hivyo wanaweza kumuwinda ili kupoteza ushahidi, hivyo Jeshi letu la polisi, litaamua kumlinda dereva huyo kwa kumuweka mahali salama.

Trend Reading ni Nini?
Trends Reading ni uwezo wa kusoma mienendo fulani ya kitu kilichotokea nyuma, kukiwianisha na kitu kilichotokea sasa, hivyo kujua kitu kitakachofuata baadae.

Lengo la uzi huu ni kukupa wewe mwana JF ile jf advantage ya be the first to know kuwa hatimaye dereva wa Lissu atatiwa mbaroni ili jeshi letu la polisi liuthibitishie umma wa Watanzania kuwa something is being done kwenye uchunguzi wa shambulio la Lissu.

Jee Trends Reading ni Kuingilia Uchunguzi wa Kipolisi?.
Jibu ni hapana, trend reading hii sio kuingilia uchunguzi kwa sababu it is presumed dereva wa Lissu has no hands kwenye tukio hilo hivyo hana sababu yoyote ya kujificha asihojiwe, na kukaa kwake Nairobi ni kwa usalama wake, hivyo atatoa ushirikiano wote unaotakiwa na jeshi letu la polisi.

Lakini kama shambulio hilo ni inside job na dereva huyo has a hand, trend reading hii kuwa anafuatwa kutiwa mbaroni, kumpelekea kuzidi kujificha ili asitiwe mbaroni na kuhojiwa, this being the case, kutaacha maswali mengi bila mujibu kuwa kama hahusiki kwa namna yoyote, kwa nini ajifiche?.

Jee Trends ni Lazima Zitokee?.
No, trends sio lazima zitokee, inawezekana kabisa lengo la polisi kwenda jijini Nairobi ni kumhoji tuu na sio kumu arrest kuisaidia polisi.

Hitimisho.
Mahojiano haya yatahitimisha mbio za sakafuni kati ya polisi na dereva wa Lissu, ambaye anasemekana ndio shahidi muhimu kuliko wote, aliyekwamisha kuendelea kwa uchunguzi wa tukio hilo. Tunawatakia Polisi Wetu Mahojiano mema na Tundu Lissu na Dereva wake, Watanzania wana kiu ya kusikia something is being done kuhusu uchunguzi wa tukio hili, kulikopelekea sisi wengine kubuni conspiracy theories kuhusu hawa watu wanaoitwa 'watu wasiojulikana'.

Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!.

Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!.

Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?!

Paskali
.
Mpaka sasa the situation ya shambulio la Lissu as it is, limefanywa na watu wasiojulikana. Serikali yetu imeshindwa kuwabaini, lakini sisi watu wa media, tunaweza kusaidia kama nilivyosema hapa.
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
Hitimisho.
The only defence ya Dereva wa Lissu has nothing to do na hiyo shooting, ni uzito tuu wa serikali yetu kufanya upelelezi wa tukio hili na kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!.

Lakini kwa vile wasiojulikana ni hawa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya kuendelea na uanaharakati na kuishi kwa mashaka, au uamue kupunguza makali na kuishi kwa amani.

Pole Sana Mhe. Tundu Lissu, Get Well Soon.
P.
Rejea

  1. Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums
  2. Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?! - JamiiForums
  3. Tundu Lissu: Polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kunihoji nikiwa Kenya au kwingineko nje ya mipaka ya Tanzania - JamiiForums
  4. Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli! - JamiiForums
    TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe! - JamiiForums
  5. Bandiko la 5 Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?! - JamiiForums
  6. Bandiko la 6 Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums
  7. Bandiko la 7 https://www.jamiiforums.com/threads...je-tukahukumiwa-karma-ndio-pekee-hutoa-hukumu
  8. Bandiko la 8 Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums
  9. Bandiko la 9 Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija - JamiiForums
  10. Bandiko la 10 WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
  11. Bandiko la 11 Siku ya Sheria: No mention of Tundu Lissu!, Je ni amesahaulika tu kutajwa, amepuuzwa au ameepukwa?!. - JamiiForums
  12. Bandiko la 12 Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi! Je, anahusika? - JamiiForums
  13. Bandiko la 13 Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela! - JamiiForums
  14. Bandiko la 14 Je, Tundu Lissu anaichafua nchi yetu au anasema ukweli wa kilichomtokea? Je, Serikali yetu iwe Proactive kusema ukweli au Reactive kumjibu? - JamiiForums
 
Hata Mungu alijua kuwa Yesu atasulubiwa ili aliacha yatimie ili sisi tukombolewa.

Kupitia shambulio la Lissu, hata sisi tutakombolewa (sometimes Mungu huruhusu mambo fulani yatokee kwa malengo maaalumu).

Kumbuka wangekuwa na nia wasingeshindwa kwenda kuwahoji hospitalI ya Nairobi.

Jiulize tu angekuwa ni kigogo wa serikali alieshambuliwa kama huyo dereva wasingemfuata kumuhoji hata kama angekuwa yuko Ulaya.
 
Kabla ya kutoa hio dhana yako ningekuomba ujibu Masuala 3 tu:-
1. Kwa nini siku ya tukio hapakua na Mlinzi Bungeni
2. Jee kwanini Picha za Camera ulinzi hazijuilikani zilipo?
3. Kwa nini Serikali ikatae uchunguzi huru ukishirikisha vyombo vya Kimataifa?
 
Back
Top Bottom