Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Sasa kwanini hamumkamati dereva?
 

Kaka Paskali nashukuru sana kwa umahiri wako wa uandishi na kuangalia suala hili kwa jicho la 3D. Hii sasa ndio aina ya uandishi unaostahili na sio kwa hili tu bali kwa mambo yote yenye utata wa hivi.

Ila ngoja nikuambie, andika uwezavyo, hoji upendavyo lakini jambo hili liko wazi hata kwa mtoto mdogo kuona uhalisia ulipo. Labda kama umeandika ili kupata uhalali wa zile mada zako zilizopelekea kuitwa Dodoma. Naheshimu maoni yako na chochote kinachokupa mashaka, lakini kwa hili liko wazi mno.
 
Jiulize tu risasi 38 mtu hajafa? Utauhoji kwanini asife?
 
Sasa kwanini hamumkamati dereva?
Sina mamlaka hayo.
Nadhani mpaka sasa una uhakika ningekuwa nayo ningeshamhoji siku nyingi.
kwa namna yoyote ile unavyoliangalia hili shambulio, huyu dereva ni shahidi muhimu sana. Hao ambao hawajatumia madaraka yao kumfata na kumhoji ninawaangalia na kusema "hiiii"

Katika dhana nyinyine, Sidhani kama Lissu angeshambuliwa ndani ya gari la serikali akiwa katika safari za kamati za bunge kisha dereva akamlaza kifudifudi kama unavyodai ungechukua msimamo huu endapo serikali isingechukua hatua madgubuti kumhoji na kupata ushahidi wa dereva
 
Mkuu hii issue haitaji akili kubwa hivyo kung'amua nani kahusika, hata mtoto wa standard one anajua nani alitaka kumuua Lissu..

"haiwezekani ukawa msaliti halafu ukasurvive, askari wakiwa vitani mmoja akawasaliti wanajua nini cha kufanya"
 
Pascal,huna hoja zilizo jaa critical thinking? Maana unaacha kabisa kugusa sehemu zilizobeba logic badala yake unazunguka kwenye vijihoja muda wote ili tu uweze kupata uteuzi.Deus de amor.To every action there is an equal and opposite reaction. Heri kufa na fikra hai kuliko kuishi na fikra mfu.
 

Kwa hili una hoja ya msingi. Lakini hili lingewezekana kwa jeshi linalofanya kazi kwa weledi na sio jeshi linalotii amri toka juu kuliko sheria zisemavyo. Kwenye nchi za kiafrika hasa zenye chembechembe za udikteta ni nadra sana jeshi la polisi kuwalinda wakosoaji wa serekali. Hili kubali kataa lakini habari ndio hiyo.
 
Hajatumia critical thinking.
 
Watoto hutenda mambo yote kwa mapokeo badala ya uyakinifu.Lakini ikitokea mtu mzima hatumii uyakinifu,basi huo ni ulemavu.
 

Nani alikuwa anamtafuta dereva, dereva amewahi kumuia mtu dictator? kutetea shambulio lile kwa kutumia hali ya Dereva ni kuzuia risasi na debe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…