Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Mkuu GENTAMYCINE umejaribu kuelezea vizuri kwa muono wako lakini tujaribu kuona kwa upande mwingine basi ukoje.
Ni kweli system ikikuhitaji huwezi kabisa kuchomoka maana inao watu trained wanaojua wana fanya nini.
Lakini system yaweza kutumika Mara mbili, issue official ambayo lazima inapangwa kiuweledi na inafahamika kwa wahusika Wa jambo hilo kwa mkakati kamili na kuna LA pili jambo ambalo halina maslahi ya taifa hivyo linafanyika kiharamu kwa kutumia baadhi ya wahusika Wa system kutekeleza.
Na uharamu huo ndio unao sababisha mambo Ku backfire hadi kuleta sintofahamu ndani ya system hadi wakati mwingine mambo ya "utata" kama yale ya kuhamishianaTabora. Hilo LA siri na haramu ndio laweza kuwa lilitumika kwa Lissu kwa system ile ile kwani Lissu sio tishio kwa taifa na hata ndani ya system anao wafuasi wanaojua umuhimu wake na kumuunga mkono utapangaje kwa uwazi kumdhuru?
Lingine ni ukimya, serikali zote ulimwenguni litokeapo jambo lenye kuichafua ni haraka sana kuweka wazi uchunguzi wake kujisafisha. Lakini mbona hii imeufunga uchunguzi pamoja na mambo ya wazi kabisa ikiwamo kuondelewa ulinzi, CCTV camera na mengineyo?
Kubaki na kusema dereva dereva ni argument isiyo na mashiko hata kidogo katika issue iliyochafua nchi kwa kiasi kikubwa. Tukubaliane tuu kuwa serikali imeshafunga siku nyingi file LA Lissu kwani majibu inayajua na kama ni kwavile ni inside job basi ni wazi serikali hii haitufai hata kwa dakika moja. Inashindwa kichukua hatua? Yaani mie nikimuua mke wangu watasema hayo ni mambo yetu ya ndani?
Don't waste your time n energy, hilo jamaa lina low IQ km kichaa jiwe na yuko kazini yaani genge la buku7
 
Mayala=njaa
Baada ya Jerry murro kuula pasco ameona fursa na wakt sahihi Wa kutafuta cheo,huyu ni tumbo linatoa hoja sio akili,umeangusha tasnia ya habari
Huyu jamaa mm sijawai kumwelewa kabisa. Nimnafiki sana .
 
Kwakweli paschal siku hizi sio paschal kama wa zamani yaani umetoa sababu za kwanini wasingetumia akili zako kujinasua baada ya kubaini watu walokuwa wanawafatilia?

Jambo la dereva kuhojiwa na polisi nakuunga mkono ila la kwanini dereva hakupatwa hata na risasi moja hiyo hoja haikubaliki kuna ajali huwa tunazishuhudia au kusikia kuwa abiria wote wamepoteza maisha ila mtoto mdogo au mtu mmoja ndio kanusurika


Nazani pointi yako kubwa katika bandiko hili ni hili andishi lako👇👇👇


Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya kuendelea na uanaharakati na kuishi kwa mashaka, au uamue kupunguza makali na kuishi kwa amani.
 
Muuaji hutumia risasi moja au mbili kwisha kazi, target ni moyo au kichwani.
Muuaji huyu alikua anajifunza kuua kwa kutumia mwili wa lisu hahahahah risasi 38.Yani hata ktk movie sijawahi ona wingi wa risasi ka huu.Hili tukio liingizwe Guinness World Records.
 
Kwakweli paschal siku hizi sio paschal kama wa zamani yaani umetoa sababu
Post hizi ni nzuri ikiwa uko kwenye utafiti na unakofanyia utafiti huo hawakujui. Jamaa kachemka mno yaani namuona kwa mbaali anavyoanza kufaidi neema za waovu kwa faraja za kutoka kwenye biblia. Napata shida sana kusoma hii post halafu anasema anamuombea Tundu. Daaaaaah.
 
Eti valid questions...nyoo, dereva wa Lissu ndiye aliyeamuru ulinzi wa Site 3 pale Area D uondolewe? Dereva wa Lissu ndiye aliyeng'oa CCTV Camera kwenye makazi ya viongozi baada ya Lissu kushambuliwa? Dereva wa Lissu ndiye aliyezuia wabunge wa CCM akiwemo na Spika Ndugai kufika hospital kumjulia Lissu hali? Dereva wa Lissu ndiye aliyezuia Bunge lisimtibu mbunge wake siyo?

Pumbavu kabisa!
Vipi kama dereva alishirikiana na waliotoa camera na ndio maana badala ya kumwambia tusimame au twende polisi akamwambia twendelee na safari?Au nyie humo vichwani hamnaga reasoning kabisa?
 
NA KWANINI WAFANYE TUKIO PRECISELY 10 MINUTES BAADA YA SPEECH YA MAGUFULI KUHUSU ACCACIA ????
Hivi kwa siku ile unafikiri ilikua rahisi Kiki ya magufuli kuhusu Tanzanite izimwe kirahisi?
 
Paskali tangu anehojiwa na bunge naona pia kuna kazi maalumu alipewa.Angalia tu trend ya mabandiko yake humu. Alifanyiwa brain programming /ccontrol na Malumumba.
 
ukweli ni ukweli tuu Mh.Lissu alishatoa taarifa kwa Bunge na kwa Police kwamba kuna watu wanawafuatilia sio kila kitu mnatia siasa sasa Hapa Bavicha wanahusikaje kwa mfano
 
Dereva wa lissu yupo ubelgiji. Kwa maelezo ya Lissu hawajakataa kuhojiwa, Ila hawataki ahojiwe TZ kwa sasa sababu si salama. Maisha yana nafasi kubwa sana. Sijui ukweli kuhusu lissu na madai yake, Ila kama yeye aliyenusurika ana wasi wasi juu ya uhai wa dreva kama ataingia TZ, na anaamini yupo sahihi basi ni sawa akiendelea kuishi bila ukweli kujulikana kwa sasa. Sijasikia maelezo ni kwann ni vigumu kuwahoji wakiwa huko walipo. Ila kwa sasa ngoja dreva aendelee kuivuta pumzi ya MUNGU mpaka itakapopatikana njia sahihi. BTW hakuna sababu ya kuingia risk kwenye maisha ya mtu ambaye anaweza kuwa si mkosaji bali ni dreva tu. Aendelee kuishi, serikali inaweza endelea na uchunguzi na endapo ikijiridhisha kuwa anahusika kuna taratibu za kumpata. Wabelgiji si maadui, watatusikiliza watamleta.
Hahahahah nyinyi watu mnafurahisha sana,So Lisu na huyo dereva hawatarudi Tz?Huo usalama wa kuhojiwa ni upi?Yani hawatak kuhojiwa Tz kisa Usalama?So serikali iwafuate huko?Sijawahi ona muathirika wa janga flani anaweka mashariti tena ya kipuuzi jinsi gani asaidiwe.Huwa nashangaa sana nkimsikia lisu et ka serikali ka inataka kunihoji kwanini isije kunihoji au kutafuta njia za kumhoji.Hivi nani anayetakiwa aangaike kuhakikisha haki inapatikana kati ya lisu na serikali? Hivi kuna kitu inapoteza kwa kutomhoji lisu?Ni maajabu lisu kupata mda wa kufanya press conference Kenya lkn sio mda wa kupigania haki yake Tz.Hizi ni siasa uchwara
 
Kabla ya kutoa hio dhana yako ningekuomba ujibu Masuala 3 tu:-
1. Kwa nini siku ya tukio hapakua na Mlinzi Bungeni
2. Jee kwanini Picha za Camera ulinzi hazijuilikani zilipo?
3. Kwa nini Serikali ikatae uchunguzi huru ukishirikisha vyombo vya Kimataifa?
''Huwezi kuhatarisha maslahi ya nchi ukaachwa ukasavaivu '' mwisho wa kunukuu.unaikumbuka hii kauli mkuu. Ilitamkwa asubuhi ya saa tano ya siku ya shambulio la lissu. Akili kichwani mkuu.
 
Post hizi ni nzuri ikiwa uko kwenye utafiti na unakofanyia utafiti huo hawakujui. Jamaa kachemka mno yaani namuona kwa mbaali anavyoanza kufaidi neema za waovu kwa faraja za kutoka kwenye biblia. Napata shida sana kusoma hii post halafu anasema anamuombea Tundu. Daaaaaah.

Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya kuendelea na uanaharakati na kuishi kwa mashaka, au uamue kupunguza makali na kuishi kwa amani.

Hiyo ndio point yake paschal
 
NI UJINGA WA KIWANGO CHA LAMI

1. Kuamini kwamba serikali ilihitaji makomandoo wengi tena wenye AK47 kumuondoa Lisu uhai. Kimsingi JASUSI mmoja tu mwenye mafunzo haba kabisa anatosha kumuondoa Tundu Lisu duniani, Tena bila mpuuzi mwingine yeyote yule kujua.

2. Kuamini kuwa pale bungeni MAJASUSI walishindwa kumuwekea sumu kwenye kiti akakalia KAMA AMBAVYO ILISEMEKANA D.R MWAKYEMBE ALIWEKEWA NA MAMVI (Na mpaka leo bado haijajulikana)

3. Kuamini kuwa wangeshindwa kumsubili barabarani wakamsukumia roli la taka ikawa ajali kama ile ililoua watalii kule Arusha

4. Kuamini kuwa Majasusi (TISS) walikosa dawa ya usingizi ya kupulizia ambayo wangeweza kwenda nyumbani kwake wakapuliza kisha wakamchomba syringe ya sumu na wakati wezi tu wa kijingajinga huku mtaani wanayo na wanatumia kuiba majumbani

5. Kuamini kuwa Majasusi (TISS) walikosa food poison ya kumuwekea dereva wa Lisu ili akilewa na kuzidiwa barabarani gari lipinduke.

6. Kuamini kuwa Majasusi (TISS) walishindwa kubuni A silent assassination method waje kumsubiri nyumbani na kupiga kelele nama AK47 ...UPUUZI.

Mimi sijawahi kwenda hata JKT lakini nina uwezo wa kubuni mbinu zaidi ya 50 za kum-eliminate MBOWE ukiachialia mbali Tundu Lisu..

TUNDU LISU hana ulinzi wa kuwapa shida watu wa TISS kama wanania ya kumuondoa.
Eti serikali iamue kumuondoa lisu ianze kumfuata fuata kuanzia Dar hadi Dodoma.hahahahah, hawa watu wanafikiri serikali ni kikundi cha wanywa kahawa.Yani serikali impe mtu AK 47 na marisasi kibao kumuua lisu tu?Kuna njia nyingi sana za kufanya tukio bila kuacha alama.Fuatilia vifo vya akina chacha,Komba,Filikunjombe nk.Hivi inasemekana na kazi ya mikono ya watu lkn kupata ukweli ni ngum sana.
 
Vipi kama dereva alishirikiana na waliotoa camera na ndio maana badala ya kumwambia tusimame au twende polisi akamwambia twendelee na safari?Au nyie humo vichwani hamnaga reasoning kabisa?
Nenda kanywe supu kwanza! Asubuhi inahitaji kujiweka vizuri kwanza
 
Back
Top Bottom