Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Uchunguzi Huru wa kimataifa ungetupa majibu yasiyoacha shaka kwa pande zote tatu,Watuhumiwa,CHADEMA na Familia ya Lissu.
Vipi hapa ndani hakuna uwezekano wa kufanya uchunguzi na majibu yakapatikana?Unataka kusema hili tukio ni complicated sana kiasi tuhitaji vyombo vya nje?Itakua nchi kweli kila katukio basi watu wajifiche kwenye uchunguz wa nje?Shida kila kitu ni siasa uchwara na hili halina tofaut ya kuacha kumpeleka muhimbili na kumpeleka Nairobi, Utaona hakukua na hoja zzt za mcng
 
Paschal Mayalla, tambua kuwa kushambuliwa kwa Lisu Dereva wake anajua, haiwezekani ajue wanafuatiliwa aendelee tu nyumbani bila kuchukua tahadhali, lakini ikumbukwe pia Antipas anao uadui mkubwa toka huko A.Kusini baada ya kesi aliyokuwa akiishughulikia kama Wakili ambako alipewa documents mbalimbali zilizosaidia na baada ya malipo hakurudisha fadhila kwa waliomchomolea documents.
 
Paskali paskali paskali, unataka kuniudhi.Nimekukosea nini paskali.
Wewe utaendelea kulamba miguu lkn nakuhakikishia hutopata uteuzi kamwe
tapatalk_1533809764586.gif
 
Somehow you have a point....ubaya watu wanasikiliza upande mmoja na kuelemea upande huo.
Ila ukisikiliza pande zote, ni bonge ya conspiracy theory!
No way, issue iko open sana ile. They want to silence him he is pain in their a.. thats why. Kama unakumbuka siku ile kulikuwa jambo linaendelea kweny jumba lenye tausi. baada tu ya kumalizika na hili likatokea. Sema ni ushamba tu ndio maana halikufanikiwa Pascal nampendeaga kitu kimoja anapenda kuishughulisha akili yake kuwaza kwa sauti lkn anajua fika nini hasa ..... kwa hili la Lissu ni Karma peke yake ndio itatenda yake lets wait n see. Pole yake Lissu na hakika ni mzalendo kwa nchi yake kwa 100% yote aliyoyasema naona yanaenda kutimia ni swala la muda.
 
Vipi hapa ndani hakuna uwezekano wa kufanya uchunguzi na majibu yakapatikana?Unataka kusema hili tukio ni complicated sana kiasi tuhitaji vyombo vya nje?Itakua nchi kweli kila katukio basi watu wajifiche kwenye uchunguz wa nje?Shida kila kitu ni siasa uchwara na hili halina tofaut ya kuacha kumpeleka muhimbili na kumpeleka Nairobi, Utaona hakukua na hoja zzt za mcng
Hapa ndani uwezekano wa kufanya uchunguzi upo lakini kwa mujibu wa Lissu mwenyewe ambaye ni mhanga wa huo unyama,mtuhumiwa wake wa kwanza ndio hao unaotaka wafanye uchunguzi.Huhitaji kuwa na Phd kujuwa huo uchunguzi utakuwa wa magumashi.
 
Mkuu sioni mkielezea kwa hoja zenye mashiko mkielezea kwanini dereva asiwe suspected zaid ya maelezo mengi ya kutafuta sympathy. Lieleze jukwaa kwanini dereva asitiliwe shaka?Kwanini dereva asiwe kati ya hao waliotoa camera au walinzi?

Mkuu inaonekana umejibu watu wengi mpaka hujui nilikuambia hiyo jana. Nakubali kabisa dereva ni shahidi, awe namba moja au mbili kwangu hiyo sio tatizo. Na sio dereva tu, hata Lissu ni shahidi tena anapaswa kuwa namba moja kwani ndiye aliye shambuliwa na bado yuko hai na aliona hilo shambulio.

Lakini kama ni huyo dereva alikuwa hapo Kenya, Lissu alisema waende wakawahoji wote na wako tayari. Tulio wengi tunafahanu jeshi letu halifanyi kazi kwa weledi kwani linaamini kwenye matumizi ya nguvu. Linachotaka ni huyo dereva aje apewe kipigo ili limuwekee maneno mdomoni kwa nia ya kufunika kombe. Ni kipi kililifanya jeshi letu lisiende hapo Kenya kumuhoji? Kipi kinashindikana kwenda hapo ubeligiji kumuhoji dereva na huyo Lissu? Mbona kamati ya kina Mwakyembe ilienda mpaka US kupata ukweli wa richmond? Misuli hii mada imejaza watu kibao wa system, kila mmoja anarusha kete yake, ni kipi haya maoni hayafanyiwi kazi?

Narudia tena, Shambulizi lile ni aina ya siasa chafu kutokea hapa nchini, tutakuwa watu wa ajabu kufumbia macho uovu ule kisa aliyefanyiwa huo unyama hakuwa mshabiki wa utawala uliopo. Hakuna haja ya kupoteza muda kwa kuokoteza utetezi dhaifu ili kubadili ukweli ule. Tufungueni ukurasa mpya na iwe mwisho wa siasa za majukwaani kujibiwa kwa mashambulio ya risasi.
 
Pascally unajidhalilisha kujaribu kmtetea kichaa, umebugi, na unajipunguzia heshima
 
Uchunguzi gani ufanyike na kukamilika bila kumhoji Dereva wa Lisu? Uchunguzi gani ufanyike kwa kuelekezwa na Ufipa jinsi ya kuendesha huo Uchunguzi?
 
Bwana mkubwa alifanya usaliti mbaya sana. Hilo huwa hawapendiki kuliongelea.

Umelishwa propaganda na ukazimeza vizuri. Sasa hivi hapa ulipo unazitapika tu. Hilo suala linaloitwa usaliti ni aina ya siasa za kijinga zilizofanywa na awamu hii ili kulindana kisiasa. Mikataba ya wizi iliyoingiwa wanafahamika ni kina nani waliingia. Katika hao hakuna aliyechukuliwa hatua bali Lissu aliitwa msaliti ili kukidhi haja ya kisiasa. Mikataba tuliyoambiwa ni ya wizi mpaka leo ni siri, na hakuna yoyote aliyechukulia hata baada ya kutajwa kwa majina. Kama kuna mahali Lissu alisaini mikataba hiyo ya wizi tuonyeshe hapa tuujue usaliti wake.
 
Mengi yameelezwa lakini nikwambie wauaji hawakutegemea ku feli kwa hio hawakuwa na haja ya kujipanga dodoma kwa sababu alinusurika inachukua muda kupanga plan b na bila shaka kama angepelekwa muhimbili wangekuwa wametoka kwenye shock na kujipanga,lakini kuna mwenendo upande wa bunge la ccm na spika ndugai unaoonyesha dhahiri kuwa wangefurahi Tundu Lissu angekufa,jambo la kwanza kukataa bunge kumlipia matibabu eti kwa sababu hakufuata taratibu sasa sijui walitaka azinduke akachukue pf3 .....upuuzi tu.pili serikali kupiga marufuku maombi ya kumuombea na kupiga marufuku t shirt za lissu kwa kifupi jina la Lissu likawa adui wa vyombo vya dola sasa wananchi wakiinyoshea vidole serikali wanafuata mantiki ya kawaida sana
 
Hii mada haina maana ni ya kutusanifu tu na huyu mtoa mada amekuwa na tabia fulani hivi ya kuwa "Erratic, Enigmatic and at the same time Hypocritical".

Shambulizi la Lissu liko wazi sana na inavyoonekana hao hao waliomshambulia ndio wale wale wanaowatumia hawa akina Mayala ili kujaribu kuchanganya watu akili.

Kibaya zaidi hawa the Mayallas, wako radhi kutumika kwa namna yoyote ile ili kuupotosha umma ili mradi tu yeye apate "Riziki" na maisha yaendelee na ndio maana kauli za utata toka kwa rais na hata reaction ya serikali kuhusiana na hii sakata, hawezi kuzizungumzua kabisa..!!!
 
Umelishwa propaganda na ukazimeza vizuri. Sasa hivi hapa ulipo unazitapika tu. Hilo suala linaloitwa usaliti ni aina ya siasa za kijinga zilizofanywa na awamu hii ili kulindana kisiasa. Mikataba ya wizi iliyoingiwa wanafahamika ni kina nani waliingia. Katika hao hakuna aliyechukuliwa hatua bali Lissu aliitwa msaliti ili kukidhi haja ya kisiasa. Mikataba tuliyoambiwa ni ya wizi mpaka leo ni siri, na hakuna yoyote aliyechukulia hata baada ya kutajwa kwa majina. Kama kuna mahali Lissu alisaini mikataba hiyo ya wizi tuonyeshe hapa tuujue usaliti wake.
Shida yako wewe, umejawa na tabia chafu, roho ya korosho, kwako wewe kuona mwingine kakamatwa ni faraja, wakati wakikamatwa wale unaowapenda unawatetea, je tuambie nani alitajwa? Wataje kwa majina hapa, kila mmoja na tuhuma yake, vinginevyo wewe tindo ni li-,Chadema.
 
Uanze
Uchunguzi gani ufanyike na kukamilika bila kumhoji Dereva wa Lisu? Uchunguzi gani ufanyike kwa kuelekezwa na Ufipa jinsi ya kuendesha huo Uchunguzi?
Uanze na kamera na walinzi nani aliwaondoa na kwa faida ya nani halafu tutafika tu kwa dereva na lissu mwenyewe
 
Kazi ya Pascal hapa system inamtumia kama litmus paper
Task yake ni kutest public reactions

Nafikiri unanielewa kama katibu wa Bunge alivyo waelewesha wanzake
 
Pasco, siamini kama shambulio dhidi ya Lisu, limefanywa na watu wasiojulikana. Haiwezekani polisi kushindwa kufahamu hata aina ya bunduki iliyotumika wakati risasi zilizotoka kwenye bunduki ziliokotwa eneo la tukio, haiwezekani kamera za CCTV ziondolewe, haiwezekani walinzi wote was SUMA na Polisi wasiwepo wote kwa pamoja wakati tukio linatokea, haiwezekani.

Vv
 
Kuna vitu vingine vinaweza kukufanya kuwa mvivu wa kufikiri, ukikubali kuingia ktk mtego wa waaiojulikana hutaweza kujua uhalisia. Kazi inayofanywa na wasiojulikana kwa sasa ni kuhakikisha suala hili linaangukia wanakotaka wao wasiojulikana, na inaelekea wanapata ushindi ktk hili, hawa ni mabingwa wa kucheza na akili za watu ili kuhakikisha ukweli halisi haupatikani, lkn yote kwa yote unapojaribu kumhusisha dereva wa Lissu jiulize maswali yafuatayo :-
1. Dereva wa lissu ana uwezo wa kuondoa CCTV cameras zilizokuwepo maeneo ya tukio?
2. Kama dereva anafahamu chochote je kwanini siku hiyo walinzi wote hawakuwepo eneo la tukio?
3. Kuna pande mbili zinarushiana mpira, je kwanini mamlaka hazitaki uchunguzi huru?
4. Kuna suala la kuhojiwa dereva wa lissu kwa sheria za kimataifa, je kwanini halikufanyika hilo?
Haya yakipatiwa majibu nadhani mjadala wa dereva wa Lissu utafungwa.
 
Paskali,

Kwa bandiko hili u DC unakuhusu 100% ila ningeomba kujua yafutayo

1. Wale walinzi wa area D pale Dodoma walipelekwa wapi siku ya tukio?
2. Zile kamera za pale kwa naibu spika kazing'oa nani na ziko wapi?
3. Nani aliizuia serikali kwenda nairobi kumuhoji dereva wake?
4. Nani aliizuia serikali kwenda Ubelgiji kumuhoji dereva wake?
5. Kwa nini uchunguzi huru hauruhusiwi?
6. Kwa uzoefu wako wa Jeshini(JWTZ) na ramani ya Dodoma,Wahuni kama unavyowaita wewe wakiwa na AK 47 waliwezaje
kulitoroka jeshi letu bora kabisa Afrika mashariki na ya kati????
 
Shida yako wewe, umejawa na tabia chafu, roho ya korosho, kwako wewe kuona mwingine kakamatwa ni faraja, wakati wakikamatwa wale unaowapenda unawatetea, je tuambie nani alitajwa? Wataje kwa majina hapa, kila mmoja na tuhuma yake, vinginevyo wewe tindo ni li-,Chadema.

Tofauti yangu mimi na ww, ww una elimu kubwa, mimi nina elimu ndogo ila najitambua na ninafahamu ninachongea. Kwenye ripoti ya Prof. Ossoro watu kama Chenge, Karamagi, Yona nk walitajwa kwa majina kwa kuiingiza nchi kwenye mikataba mibovu. Na rais akaagiza wakamatwe na uchunguzi dhidi yao uanze mara moja. Je hilo limewahi kufanyika? Hunimidu kwa hoja, hapa ukija ujipange.
 
Back
Top Bottom