Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Sioni hata mmoja wenu akijenga hoja zenye mashiko kwanini dereva asiwe suspected. Wengi mnaishia kuhitimisha serikali haiwezi kwepa ktk hili.Mimi sikatai,hoja yangu kwanini dereva asiwe pamoja na serikali ktk kufanya huu unyama?Hoja za camera wala walinzi sio kigezo cha dereva kutohusika au serikali kuhusika hakumaanishi dereva hawez husika.Tuwe rational tu ktk kufikir,

Unajua kwanini nimekupa ushindi, nimegundua umeishiwa na hoja sasa unalazimisha tuingie kwenye ubishani. Nimekuambia bayana sio dereva tu kwenye ushahidi, bali hata Lissu anapaswa kuwa shahidi kwani yuko hai na kwenye shambulio alikuwepo. Sasa naona akili imehama umekuwa kama umekariri kwamba kila anayezungumzia hili jambo akiwa upande wa Lissu anagoma dereva kuhojiwa.
 
Ni taahira tu na mjaa laana anayeshindwa kujua JIWE ndo anataka kumuua LISSU. Ana Chuki kwake kaliiiii hata kesho kuna sheria mpya inapelekwa bungeni kuhusu TLS kuwadhibiti kina LISSU wakati mwenyewe bado anapigania uhai wake
 
Jana nilifanikiwa kusoma alichokiandika Pascal Mayalla kuhusu Dereva wa Tundu Lisu nilijiuliza maswali mengi bila majibu ila mchana wa leo nikagundua kitu ambacho kimekuwa faida kubwa kwa wote wanaonyoosha na kutumia taaluma zao vibaya kuhusu Tundu Lisu.

Moja>>> Wengi wanaonyoosha kalamu zao vibaya juu ya Tundu Lisu wengi wamepata teuzi mbalimbali.

Mbili>>> Wengi wanaonyoosha kalamu zao vibaya juu ya TL wanaonekana ni wazalendo na wapo katika wakati mzuri wakisubili teuzi.

Tatu>>> Wanafanya mambo yao bila wasiwasi kwa sababu wanaonyesha kuunga mkono juhudi za chama tawala.

NNE>>> kwa sasa ukimtuhumu TL unajipatia umaarufu na jina lako litaonekana hata kwa waheshimiwa unajitengenezea mazingira bora.

NI FAIDA KUMTUHUMU TUNDU LISU HATA MIMI NAJIPANGA SEMA SIJAJUA NIMTUHUMU ALIJISHAMBULIA.?
 
Shida ya kuwa na Maadui wengi ndio hii mwisho wa siku inakuwa ni ngumu sana kugundua aliekudhuru ikitokea umedhurika, lwenye hili la Lissu wengi wanahisi waliotekeleza hilo tukio ni watu wa System, hamna mwenye uhakika zinabakia kuwa ni hisia tu hamna mwenye uhakika,

Baadhi ya wahalifu huwa wanasubiria ukwaruzane na mtu ili atekeleze uovu wake anatumia hii advantage ili akishatekeleza lile tukio mtu wa kwanza kuhisiwa awe ni yule uliyekwaruzana naye mara ya mwisho aonekane ndo katekeleza hayo maovu, pengine ndo kinachotokea kwenye saga la TL
 
Kabla ya kutoa hio dhana yako ningekuomba ujibu Masuala 3 tu:-
1. Kwa nini siku ya tukio hapakua na Mlinzi Bungeni
2. Jee kwanini Picha za Camera ulinzi hazijuilikani zilipo?
3. Kwa nini Serikali ikatae uchunguzi huru ukishirikisha vyombo vya Kimataifa?
kwanini wameendelea kumficha dereva yule..kuna usiri
 
The fact that serikali ilisitisha uchunguzi kuhusu sakata hilo kabla hata ya kuanza let alone kujitahidi angalau kuwadanganya hata wachumia tumbo na vinyonga kama Paskali, raises more questions than it answers and therefore any claims, allegations and fingerpointing over the involvement of Lissu's driver or CDM and party leader Mbowe in the attempted murder of TL is hogwash, fictitious and frivolous to say the least!
Paskali tafadhali jieshimu angalau kidogo, do not add salt to injury! Let this matter rest, ukweli wa sakata hilo utabainika in due cause, stop playing arbiter for those devils who tried to assasinate TL
.
 
kwanini wameendelea kumficha dereva yule..kuna usiri

..dereva hajafichwa.

..alikuwepo Nairobi kwa miezi 3+ hakuna aliyejisumbua kwenda kumhoji.

..sasa hivi yuko Ubelgiji na hakuna aliyeonyesha nia ya kutafuta namna ya kumhoji.
 
Kabla ya kutoa hio dhana yako ningekuomba ujibu Masuala 3 tu:-
1. Kwa nini siku ya tukio hapakua na Mlinzi Bungeni
2. Jee kwanini Picha za Camera ulinzi hazijuilikani zilipo?
3. Kwa nini Serikali ikatae uchunguzi huru ukishirikisha vyombo vya Kimataifa?
...kwa nini unauliza kwa nini !?
 
mimi ni kijana wa miaka 30 nadhani ki tamaduni za kiafrica sitakiwi kumuita Pascal mpumbavu maana amenizidi umri na mimi kama baba yangu.
acha niamini mtu mzima ninae muamini ameteleza tu.
 
Umeelezea upande unaokufurahisha, lakini issue ya kutoka kwenye attempt ya kuuawa hasa kwa silaha inawezekana, Lissu siyo mtu wa kwanza, alishambuliwa Pope John Paul wa II tena akiwa ameangaliana na muwaji lakini akufa, sembuse lissu aliyekuwa kwenye gari? Ni Mungu tu ndiye anayepanga ufe au upone.
 
Wanabodi

Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
Shambulizi la Lissu, Wanaomdhania Dereva Anahusika, Sio Wajinga!, Wana Hoja za Msingi!. Jee Anahusika?.
Si maanishi kuwa dereva wa Lissu anahusika, bali mazingira ya tukio, yanahalisha watu wenye udadisi kujiuliza maswali kihusu tukio lenyewe, hivyo kuhisi uhusika wa dereva wa Lissu, sio jambo la ajabu, tena uhusika wenyewe sio lazima uwe expressly but impliedly kwa negligence iliyopelekea Lissu kuwa reached na watu wasiojulikana na kushambuliwa, wakati alikuwa na uwezo wa kumuepusha na shambulizi hili.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka?, halafu what happened?!. Kwenye mambo ya assignment, anaweza hata akatumika mke wako aliyekuzalia wanao, sembuse itakuwa dereva tuu mliotoka nae mbali!.
Baadhi ya maswali ni haya...
  1. Kwa vile Lissu aliwahi kuripoti kufuatiliwa, kupitia press conference, kwa nini hakuripoti polisi?!.
  2. Baada ya Chadema kupokea taarifa ya Mnadhimu wake kufuatiliwa, walichukua hatua gani?.
  3. Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.
  4. The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.
  5. Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
  6. Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.
  7. Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.
  8. Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
  9. Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.
  10. (Mimi niliwahi kuwa mwanajeshi wa JWTZ hivyo kuna kitu nakijua kuhusu hizi AK47 ndani ya jeshi letu, lakini vitu vingine ni siri za usalama wa taifa letu, sina uhakika mtu asiyepitia JWTZ, ana uwezo gani kuijua AK 47!.)
  11. Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
  12. Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.
  13. Maswali haya yameendelea kwa msaada wa mwana jf huyu

  14. Bunduki iliyotumika waliiona ni AK 47 iliyokuwa na full magazine (risasi 40) ambayo ilimimina risasi zote 40 at close range. Kati ya hizo 17 zilizama kwenye miguu, mikono na kiuno cha Tundu Lissu.
  15. Risasi zilimiminwa kutoka upande wa kulia wa gari ambao ni upande wa dreva lakini dreva hakupatwa na risasi hata moja na alipata hata fursa ya kuteremka kwenye gari na kwenda ku take cover kwenye magari yaliyokuwa yamepaki eneo hilo. Assailants walikuwa upande wa kulia wa gari, hivyo risasi zilizama zaidi kwenye mguu wa kulia, paja la kulia, mkono wa kulia, kiuno upande wa kulia na kutokea tumboni na mkono wa kushoto. These are the documented medical forensic clues
  1. Hapa nimechoka sijui ulikua unamaanisha hivyo au mimi nashidwa kuisoma hii picha.
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    20.7 KB · Views: 39
Kila mtu anaeuliza au kuhoji kuhusu kufikiwa kwa Uchunguzi wa tukio la kushambuliwa mbunge wa JMT mheTundu lissu,
Au kuna mtu yeyote aliyetiwa kizuizini mpaka sasa kutokana na tukio hilo.

Huwa wanakuja na jibu jepesi tu eti kwa nini dereva wake amefichwa.

inachekesha hivi ata kama mkipewa dereva ndio mtajua wahusika wa lile tukio?

Kama tu hamjui ata majina ya walinzi ambao walitakiwa kuwa zamu siku ile hivi mkipewa huyo dereva ndio mtajua.?

Kama tu mmeshindwa kung'amua ata kwa kuhisi mtu aliyejitolea kutoa camera za cctv eneo lilipofanyika tukio ndio mna imani kwamba mkipewa dereva wa lissu basi na hizo CCTV zitaonekana .


Even mimi Zero Iq nimefikiria na kuona hiyo ni kama kuruka mkojo wako na kutaka kukanyaga mavi ya Rashidi je nyie wenye kutoa hilo jibu mtakuwa na Iq ya Aina gani?
Hata hizo CCTV au walinzi wangekuwepo lkn mtu wa kwanza kuhojiwa ni Dereva. Kwa vyovyote vile huwezi mtoa Dereva ktk hili.
 
Back
Top Bottom